Roma Na Stamina (Rostam),Acheni kutembelea kiki ya Fiesta.

Roma Na Stamina (Rostam),Acheni kutembelea kiki ya Fiesta.

Halafu kuna jamaa wanakuambia Clouds kupitia Tigo Fiesta huwanyonya wasanii.

Kumbe kuna wasanii wanaishi kwa kuvizia Fiesta pekee.
 
Hey Mapeople,,,

Nimekuwa nikimfuatilia Roma na Stamina jinsi wanavyo Fanya mziki wao ni wazi kuwa wanafanya mziki kwa ajili ya Tigo fiesta na hawana malengo yoyote juu ya mziki wao.

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa hawa wasanii wanao jiita ROSTAM ni wazi utakuwa umegundua hili,Mara nyingi wamekuwa wakisubiri Fiesta itangazwe ndo wanatoa ngoma,Na ngoma zao zote zilizo Fanya vizuri kidogo ni zile wanazo zitoa kipindi kama hiki cha Fiesta.

Ni wazi kuwa Roma na Stamina bila Fiesta hakuna lolote,Na Fiesta ikiisha huwezi kuwasikia tena mpaka msimu mwingine.

Clouds achaneni na wasanii kama hawa ambao hawana malengo na mziki wao,Nilitegemea mtu akipata show za fiesta iwe kama platform ya kumsogeza mbele kiaina.

Clouds pigeni chini Roma na Stamina ili akili iwakae sawa ,Haiwezekani wawe wana achia ngoma kipindi hiki kwa kuamini Zita pigwa sana.

#Jimmy-The-Inimitable.
kila mtu afanye anachoweza
 
Back
Top Bottom