Roma na Wenzako, Msithubutu kuwasaliti Wapiga Yowe Wenu!!

Roma na Wenzako, Msithubutu kuwasaliti Wapiga Yowe Wenu!!

Sitegemei kusikia chochote cha maana kutoka kwao hiyo kesho. Wameshapangwa hawana jipya, Fedha mwanaharamu sana inaweza kumfanya chochote mwenye njaa.
 
Anasema ye ni mzima anashuka kwenye gar anachechemea
 
Yani wewe unapost humu na io fake ID unataka mwenzako ajitoe muhanga.Roma awe mpole tu afanye kile watekaji wake wamemuelekeza wakirudi hawamwachi.
 
Bashite alisikia Roma kaanda bonge la nyimbo la kufichua maovu ya bashite. Sasa hapo atakuwa kampa kahela ili kuficha au walitishiwa kuwa ukitoa nyimbo yyte basi unauliwa.
Bashite ana kazi. Jambo dogo km hilo unakubali udhalilike
 
Asikwambie mtu wakikuteka wale watu hutokuja kusema hata siku moja! Hata siku moja, hapo kala vitisho vya kutosha. Unakumbuka Ulimboka? Uliwahi kusikia akisema lolote?
Angalia video ya Ulimboka hapo juu alisema kila kitu.
 
Alotekwa hashindwi kusema kweli msilete akili za kinyumbu ila uzuri wa tz wa leo si wajinga tunaelewa huu mchezo hautofika mwisho utagundulika.
Roma atekwe who is roma? kafanya kosa gani
Roma ni mtanzania kama mimi na wewe.
Ukichimama nchale, ukinana nchale, ukichema utweli nchale.
 
Watu wa ajabu sana Nyie.
Mnatengeneza picha ya kumpaka Matope RC Makonda kua ndie anahusika huku wasiwasi mkiwa nao kama picha itakwenda kama mlivyopanga.Aibu sana.

Sasa furaha yenu ni Roma na wenzie kusema Makonda aliwateka.
Asiposema hivyo matusi atakayokula mungu nisaidie [emoji23][emoji23]
Mungu anawaona vile na njama zenu za kitoto
 
Hamna kitu rahisi kama kumsakizia mwenzio awe mkweli huku Upo nyuma ya keypads ukijificha kwa ID fake huku ukisubiri ushangilie na kutoa matusi Ku release temper yako kwa maslahi ya mapapa yanayokinzana... Tanzania hii itakuwa nyuma kama mkia siku zote tusipokuwa serious.
 
Kitendo chenu cha kuficha ukweli wa mambo ulivyo, eti kwa sababu ya mapatano na watekaji;

Mosi.
Huku kutakuwa ni kuwasariti wale walioshinikiza kuachiwa kwenu, na ni dhambi mbaya sana!

Pili.
Kitendo cha kuficha ukweli wa mambo ulivyo;
Huko kutakuwa ni kuridhia ndugu zenu na jamaa zenu waendelee kutendewa kama ninyi au zaidi yenu, yaani kupotezwa kabisa kama Ben.

Tatu.
Kitendo cha kuficha ukweli wa yale yaliyowakuta;
Huko kutakuwa ni kuiridhia dhambi ya watekaji.

Nne. kitendo cha kudanganya ili kuficha dhamira ya watekaji;
Huko kutakuwa ni kumkosea Mungu aliyewatoa katika makucha ya simba wenye uchu wa nyama zenu.

Mwisho.

Roma mkatoriki, mnamkumbuka Dr. Ulimboka?

Nani ajuae huenda angeweka ukweli wa mambo yaliyomkuta wazi leo msingekuwa wahanga wa haya!

Narudia.
Semeni ukweli ili kuwatia moyo watetezi wenu kusudi waendelee kuwapambania wengine.
Semeni ukweli maana wasema kweli ni wapenzi wa Mungu.
Usiwatafutie matatizo wana wa wenzako, kama wakiamua kusema ni kwa hiyari yao na mustakbali wa maisha yao, Kwani Ulimboka ulishamsikia tena akisemasema? Hujui ugumu wa maisha.
 
Usiwatafutie matatizo wana wa wenzako, kama wakiamua kusema ni kwa hiyari yao na mustakbali wa maisha yao, Kwani Ulimboka ulishamsikia tena akisemasema? Hujui ugumu wa maisha.
Hujui madhara ya kulinyamazia hili?
 
Madhara wanayajua ndio nasema usiwalazimishe kusema unachotaka wewe.
Kunyamaza ni salama zaidi kuliko kuanzisha league ambayo ni wazi huwezi kuishinda. Fikiria mpaka mtu akuteke tena mkiwa zaidi ya mtu mbili na awapeleke anakojua yeye and then akuachieni kwa matakwa yake, hapo lazima utulie.
 
kuficha ficha kulimcost mdada mmoja alikuwa anatoka nje ya ndoa yake sasa kunasiku guest akakutana na mpangaji mwenzake na ni best wa mme wake, jamaa kesho yake akaomba mchezo kwa kigezo kwamba akikataa kumpa anamwambia mmewe, bidada akatoa siku ya kwanza, sasa jamaa kujua kuwa weakness yake ni hyo ndo kila siku akawa jamaa anadai tu mwisho wa siku bidada aliandika barua nzito na kujiua.

msema ukweli na muwazi ni mtu huru siku zote hata kama ukweli utakugharimu lakini kuna muda utakuwa huru
 
We jamaa kumbaffu sana, yaani mwenzio katoka ktk mental torture na hao watekaji wamewaacha kwa masharti kisha wewe unaeshinda mitandao unapiga kelele, watu ka nyie roma awapuuze afuate yake.
 
Back
Top Bottom