Ni kweli.
Worldcup 1998 zidane alicheza mechi mbili za makundi, mechi ya pili akala red card hivyo akakosa mechi ya tatu ya makundi na mechi ya 16 Bora dhidi ya Paraguay. Hivyo zidane alicheza na Italy(giant) robo fainali (hapa aling'ara sana), nusu against croatia(alicheza kawaida sana) na fainali against Brazil (hapa alicheza mpira wa sayari nyingine?
Euro 2000 kama unakumbuka zidane hakucheza vizuri kwenye makundi mpaka France walimaliza washindi wa pili nyuma ya Holland. Robo wakakutana na Spain ya akina Raul na Guardiola (zidane alisimamisha dunia), nusu fainali akakutana na ureno ya figo( moja ya mechi bora zidane alizowahi kuperform) fainali akakutana na Italy.aliperform vizuri sana.
Worldcup 2002 France waliishia makundi.
Euro 2004 france mechi ya kwanza akaanza na England (giant).mechi ikaisha kwa France kushinda 2-1 magoli ya france yote akifunga zidane.ila zidane alishindwa robo fainali na Greece(small ) na kutolewa
World cup 2006 .mechi ya kwanza na South Korea draw( first yellow card). Ya pili na uswisi draw (second yellow card).mechi ya tatu akawa suspended against Togo.ufaransa akashinda.uliibuka mjadala mkubwa sana nchini ufaransa kwamba mechi mbili za kwanza zidane ndie alikuwa anaiangusha timu hivyo mechi ya 16 Bora na Spain asipangwe. Kocha akasema siwezi kucheza na Xavi, Iniesta, Fabregas na Alonso katikati bila Zidane wataniua.kumbuka may Xavi na Iniesta walitoka kuchukua UCL na Barca, Fabregas ametoka kucheza fainali ya UCL na Barca na Alonso mwaka mmoja uliopita aliwapa ubingwa liverpool wa UCL dhidi ya Ac Milan.hivyo Spain walikuwa na viungo waliokuwa kwenye fomu balaa kwahiyo france walilazimika kumpanga zidane.
Kilichofuata France 3-1 Spain.goli la tatu anafunga Zidane.
Robo fainali na Brazil anatoa assist kwa Henry
Nusu na Ureno anafunga goli moja Zidane.
Fainali France anafungwa na zidane anastaafu.
Conclusion:
Linapokuja suala la big match sijawahi kumuona mchezaji wa level ya Zidane.
Sent using
Jamii Forums mobile app