RONALDINHO atangaza kutundika daluga, ninakushukuru kwa niaba ya Dunia

RONALDINHO atangaza kutundika daluga, ninakushukuru kwa niaba ya Dunia

Huyu jamaa alikuwa ni entertainer aliifanya soka kuwa burudani, yaani akiwepo uwanjani unaburudika hata akikufunga unaridhika na kusuuzika roho. Yaani hata yeye mwenyewe alikuwa ana enjoy sanaa yake, sio mchezaji unakuwa serious kama unauwa nyoka. Yeye anakupiga chenga tobo kanzu anakupiga gori alafu anacheka.

Nilimpenda sana huyu jamaa amefanya miujiza mingi sana kwenye soka hasa ya kiburudani.
Hata ukiwa upo Timu pinzani utapenda awepo ili uone burudani ya mpira
 
Gaucho hana alichompita messi acheni mihemuko ya kijinga
Kwani messi keshaweka daluga juu kama vinjino, aweke daluga ndio tufanye comparison, lakini mnabishana na mtu aliyestaafu na mwingine bado yumo kwenye game, hakutakuwa na uwiano
 
images%282%29.jpg
images%281%29.jpg
images.jpg
 
Hakuna siku katika maisha yangu ya ushabiki Wa Man Uted niliyomchukia Fergie kuhusu sajili kama siku Gaucho alipotangazwa mchezaji Wa Barca na siyo Man United ambako alifika na kunywa chai kisha Fergie akasuasua.
 
Kipaji chake huyu kilikuwa cha hali ya juu. Sasa hivi hakuna mchezaji mwenye kipaji kama cha huyu mchawi wa soka.


Sana mkuu kwa kizazi chake cha soka basi alitesa hasa. Puyol Na Sergio Ramos walikuwa wana kazi kubwa kumzuia maana jamaa akiwa Na mpira utadhani kaupaka gundi
 
Kabisa Mkuu acha huyu aende zake.

Sana mkuu kwa kizazi chake cha soka basi alitesa hasa. Puyol Na Sergio Ramos walikuwa wana kazi kubwa kumzuia maana jamaa akiwa Na mpira utadhani kaupaka gundi
 
Ni mchezaji bora kwa mwaka 2005, is the most technical player of all time. Yajue mambo 10 yaliyokupita enzi zake

1. Alikua akimpitia/drive Messi kila siku kwenda nae mazoezini enzi akiwa Barca na ndi mpaka keo messi anatamani kua kama Gaucho kwa kua ameona vingi zaidi ya mim na wew

2. Amekusanya jezi nyingi kwa mtindo wa kubadilishana baada ya mechi

3. Akiwa na miaka 7 ndipo alipewa jona la ronaldinho

4. Malengo yake kwa sasa ni kuanza siasa, cjui labda anamekua boosted na Joji weah

5. Mara zote awapo Barcelona kabla ya match aligongonga sana papuchi, anasema alikua anajiskia vzr kesgo yake uwanjan

6. Ilikua asain man u kabla ya barcelona

7. Anataka kufanya Duo with David Gueta

8. Ameshashiriki kweny segment ktk moja ya muvi za kifaransa, pia kwa sasa anahulka ya kuact muvi

9. Alishawahi kua msemaji wa UN 2016, "Michezo kwa maendeleo na amani"

10. ....
Source:The 10 things you do not know about Ronaldinho!
 
Mbona nyingine ni kama za De Lima....i.e kunamna gani mabinti!
 
Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na vilabu vya PSG, Barcelona na AC Milan, Ronaldo de Assis Moreira Maarufu kama Ronadinho Gaucho amestaafu soka.

Licha ya Ronadinho kutocheza soka la kiushindani lakini toka mwaka 2015 amekua akicheza michezo ya mabonanza

Kaka na wakala wa mchezaji huyo Roberto de Assis Moreira amethibitisha kuwa umefika mwisho kwa fundi huyo wa kibrazil kucheza soka.

Ronaldinho alianzia soka lake katika klabu ya Gremio ya nchini kwao kabla ya kujiunga na Paris St-Germain mwaka 2001 na baadae kujiunga na Barcelona alikong'ara sana.

Katika msimu wa 2010 -2011 alijiunga na Ac Milan ya Italia kabla ya kurudi kwao na kujiunga na Flamengo mwaka 2011. Kisha alichezea vilabu vya Atletico Mineiro, na Queretaro ya nchini Mexico na kurudi tena kwao Brazil katika klabu ya Fluminense.

Tujikumbushe kidogo aliyokuwa wanafanya uwanjani Ronaldinho



Naaaaam!....huyu alikuwa mtu hatariii sana anapokuwa na mpira mguuni mwake, tutamkumbuka kama legend kwenye history of football, ebu weka na hii clip hapo kwenye post yako alipokuwa akifanya massive skills of destruction, demolition and humiliation hadi kufikia mwaka jana msimu wa 2017 kwenye premier futsal japo...umri umemuacha lakini bado anastaafu na kipaji chake murua ambacho ama kwa hakika hakipatikani kwa mwengine duniani isipokuwa yeye tu, nampa asante zangu kwa huduma yake ya soccer aliyotupatia washabiki wa mpira duniani, LONG LIVE THE WORLD BEST PLAYMAKER&TRICKSTER TO EVER LIVE & KING OF FOOTBALL!!!...All other Players are down to his talented feet indeed.

 
Back
Top Bottom