Kibongo bongo inaaminika kua ili uwe mwanaume basi inatakiwa uwe sahbiki wa mchezo wa mpira.
Upande wangu kama Me nimejitahidi sana kuangali mpira ila nimeshindwa kabisa. Nina mpenda na kumshabikia messi tu (sio Barcelona) ila sijawahi kaa dakika 90 kuangalia akicheza mpira.
Kwenye mpira japo sio mfuatiliaji sana ila nawapenda na kuawakubali zaidi watu waiwili tu Ronaldinho na Messi. Hawa naamini ndio binaadamu wenye uwezo mkubwa wa kucheza mpira. Ronaldinho namuweka namba moja ndio binaadamu anayeweza kuchezesha/kuuchezea mpira na Kuufanya vile atakavyo (kwa mujibu wa clip za YouTube nilizowahi tizama)
Messi namuweka namba 2 ndio binaadamu anayejua kucheza mpira kuliko yoyote yule hapa duniani....Binafsi nampenda sana Dinyo, Yupo Cool. Kila mtu anampenda hua hachukii. Ukuwa Cool and Kind you won my Heart.
Kuna clip nitaweka link Dinyo anafanya vitu nilivyokua naona kwenye muvi ya Shaolin Soccer.. Kasimama kwenye boksi la 18 halafu anapiga mpira unagonga mwamba kisha unamrudia anapiga tena meamba zaidi ya mara tano (sio kubahatisha). Nyingine kapiga danadana zaidi ya 50 akiwa kafunga kitambaa usoni.
Sidahani kama messi anaweza fanya haya.
Kama upo stressed au bored wala usiende kunywa pomba..Nenda YouTube then tafuta Clip za Dinyo utafurahi kwa bei sawa na bure
Live long Ronaldinho
My Ambition siku moja nikutembelee nikupe heshima yako. Either ukiwa hai au kwenye kaburi lako (kama utatangulia)
View attachment 1429176