Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka wa FIFA kwa mara ya pili katika historia yake, akimuangusha mshindani wake mkuu, Lionel Messi.
Nyota huyo babu kubwa wa Real Madrid alikuwa anakabiliwa na ushindani wa mbali kidogo kwa nyota wa Barcelona, Messi na wa Bayern Munich, Franck Ribery katika kinyang'anyiro cha Ballon dOr.
Akiwa mwenye hisia kali, Ronaldo aliyekwenda jukwaani kuchukua tuzo yake akiwa ameambatana na mtoto wake wa kiume, Cristiano alishindwa kujizuia na kumwaga machozi wakati anapokea taji hilo.
Namba 1: Cristiano Ronaldo ameshinda Ballon d'Or na kutajwa ndiye mwanasoka babu kubwa duniani
Hisia: Ronaldo alishindwa kujizuia na akamwaga machozi jukwaani wakati anapokea tuzo ya Ballon d'Or
Mshindi: Pele akiwa amemshika mtoto wa Ronaldo, Cristiano wakati Mreno huyo anapokea tuzo yake
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amepewa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 66 katika mechi 56 za klabu na nchi yake, Ureno mwaka 2013 hatimaye kuirejesha tuzo yake aliyoitwaa awali mwaka 2008.
Pamoja na kwamba Ronaldo hakutwaa taji kubwa mwaka 2013, alifunga mabao yote manne Ureno ikiitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya kombe la Dunia baadaye mwaka huu.
"Hakuna maneno ya kusema wakati huu," Ronaldo alisema, huku akifuta machozi. "Nataka kuwashukuru wenzangu wote na washirika pale Real Madrid, katika timu ya Ureno na familia yangu, ambako wako nami,".
"Wale ambao wananifahamu mimi, wanafahamu kwamba watu wengi wananisaidia: kocha wangu, rais wetu, na sitaki kusahau kumtaja Eusebio. Mpenzi wangu na mwanangu pia. Nasonga zaidi,".
Ronaldo na mpenzi wake Irina Shark katika sherehe za tuzo
Washindani: Ronaldo, Lionel Messi na Franck Ribery kabla ya sherehe
Gwiji Pele alipea tuzo katia usiku huo mjini Zurich
Mfalme wa soka: Gwiji wa Brazil, Pele alishindwa kujizuia kutoa machozi alipokuwa jukwaani
Retied Jupp Heynckes ameshinda tuzo kocha bora wa mwaka wa dunia baada ya kuiwezesha Bayern Muich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Mkali: Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Bao Bora la mwaka, maarufu kama Puskas
Bao lake tik tak Sweden ikiifunga 4-2 England Novemba mwaka 2012 ndilo bao bora la mwaka
Kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kike wa mwaka wa Dunia
Wawili: Ronaldo na Angerer baada ya kutajwa wanasoka bora wa dunia
Taji: Angerer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshinda Kombe la ubingwa wa Ulaya kwa wanawake
Uso wa mbuzi: Lionel Messi na Antonella Roccuzzo waliwasili kwenye sherehe Ballon d'Or wakiwa wamekasirika
Nyota huyo babu kubwa wa Real Madrid alikuwa anakabiliwa na ushindani wa mbali kidogo kwa nyota wa Barcelona, Messi na wa Bayern Munich, Franck Ribery katika kinyang'anyiro cha Ballon dOr.
Akiwa mwenye hisia kali, Ronaldo aliyekwenda jukwaani kuchukua tuzo yake akiwa ameambatana na mtoto wake wa kiume, Cristiano alishindwa kujizuia na kumwaga machozi wakati anapokea taji hilo.
Namba 1: Cristiano Ronaldo ameshinda Ballon d'Or na kutajwa ndiye mwanasoka babu kubwa duniani
Hisia: Ronaldo alishindwa kujizuia na akamwaga machozi jukwaani wakati anapokea tuzo ya Ballon d'Or
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amepewa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 66 katika mechi 56 za klabu na nchi yake, Ureno mwaka 2013 hatimaye kuirejesha tuzo yake aliyoitwaa awali mwaka 2008.
Pamoja na kwamba Ronaldo hakutwaa taji kubwa mwaka 2013, alifunga mabao yote manne Ureno ikiitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya kombe la Dunia baadaye mwaka huu.
"Hakuna maneno ya kusema wakati huu," Ronaldo alisema, huku akifuta machozi. "Nataka kuwashukuru wenzangu wote na washirika pale Real Madrid, katika timu ya Ureno na familia yangu, ambako wako nami,".
"Wale ambao wananifahamu mimi, wanafahamu kwamba watu wengi wananisaidia: kocha wangu, rais wetu, na sitaki kusahau kumtaja Eusebio. Mpenzi wangu na mwanangu pia. Nasonga zaidi,".
Mfalme wa soka: Gwiji wa Brazil, Pele alishindwa kujizuia kutoa machozi alipokuwa jukwaani
Taji: Angerer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshinda Kombe la ubingwa wa Ulaya kwa wanawake
Katika zulia jekundu: Cristiano Ronaldo (kushoto) akiwa na mpenzi wake, Irina Shayk na mtoto wao wake wa kiume katika sherehe za tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or zilizo fanyika jana mjini Zurich, Uswisi.
Franck Ribery naye alifika na mpenzi wake, mwanamitindo Adriana Lima