Ronaldo amwaga machozi baada ya kushinda ballon d' or...pele naye aangua kilio zurich

Ronaldo amwaga machozi baada ya kushinda ballon d' or...pele naye aangua kilio zurich

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka wa FIFA kwa mara ya pili katika historia yake, akimuangusha mshindani wake mkuu, Lionel Messi.
Nyota huyo babu kubwa wa Real Madrid alikuwa anakabiliwa na ushindani wa mbali kidogo kwa nyota wa Barcelona, Messi na wa Bayern Munich, Franck Ribery katika kinyang'anyiro cha Ballon d’Or.
Akiwa mwenye hisia kali, Ronaldo aliyekwenda jukwaani kuchukua tuzo yake akiwa ameambatana na mtoto wake wa kiume, Cristiano alishindwa kujizuia na kumwaga machozi wakati anapokea taji hilo.
article-2538773-1AA356E100000578-630_634x421.jpg

Namba 1: Cristiano Ronaldo ameshinda Ballon d'Or na kutajwa ndiye mwanasoka babu kubwa duniani



article-2538773-1AA353DB00000578-612_306x423.jpg

article-2538773-1AA3516800000578-254_306x423.jpg


Hisia: Ronaldo alishindwa kujizuia na akamwaga machozi jukwaani wakati anapokea tuzo ya Ballon d'Or



article-2538773-1AA3559100000578-447_634x447.jpg
Mshindi: Pele akiwa amemshika mtoto wa Ronaldo, Cristiano wakati Mreno huyo anapokea tuzo yake

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amepewa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 66 katika mechi 56 za klabu na nchi yake, Ureno mwaka 2013 hatimaye kuirejesha tuzo yake aliyoitwaa awali mwaka 2008.
Pamoja na kwamba Ronaldo hakutwaa taji kubwa mwaka 2013, alifunga mabao yote manne Ureno ikiitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya kombe la Dunia baadaye mwaka huu.
"Hakuna maneno ya kusema wakati huu," Ronaldo alisema, huku akifuta machozi. "Nataka kuwashukuru wenzangu wote na washirika pale Real Madrid, katika timu ya Ureno na familia yangu, ambako wako nami,".
"Wale ambao wananifahamu mimi, wanafahamu kwamba watu wengi wananisaidia: kocha wangu, rais wetu, na sitaki kusahau kumtaja Eusebio. Mpenzi wangu na mwanangu pia. Nasonga zaidi,".

article-2538773-1AA308A600000578-724_634x423.jpg
Ronaldo na mpenzi wake Irina Shark katika sherehe za tuzo




article-2538773-1AA2AB7E00000578-207_634x401.jpg
Washindani: Ronaldo, Lionel Messi na Franck Ribery kabla ya sherehe



article-2538773-1AA34C8C00000578-795_634x480.jpg
Gwiji Pele alipea tuzo katia usiku huo mjini Zurich





article-2538773-1AA34BD400000578-749_306x423.jpg

article-2538773-1AA34BD400000578-760_306x423.jpg


Mfalme wa soka: Gwiji wa Brazil, Pele alishindwa kujizuia kutoa machozi alipokuwa jukwaani
article-2538773-1AA3469600000578-180_634x443.jpg
Retied Jupp Heynckes ameshinda tuzo kocha bora wa mwaka wa dunia baada ya kuiwezesha Bayern Muich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya


article-2538773-1AA345C800000578-23_634x426.jpg
Mkali: Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Bao Bora la mwaka, maarufu kama Puskas



article-2538773-160845A3000005DC-30_634x423.jpg
Bao lake tik tak Sweden ikiifunga 4-2 England Novemba mwaka 2012 ndilo bao bora la mwaka



article-2538773-1AA366F300000578-131_634x436.jpg
Kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kike wa mwaka wa Dunia



article-2538773-1AA363D100000578-144_634x601.jpg
Wawili: Ronaldo na Angerer baada ya kutajwa wanasoka bora wa dunia




article-2538773-1A9FD5D300000578-397_306x423.jpg

article-2538773-1AA34E8700000578-22_306x423.jpg


Taji: Angerer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshinda Kombe la ubingwa wa Ulaya kwa wanawake

1389635335802_lc_galleryImage_ZURICH_SWITZERLAND_JANUAR.JPG
Katika zulia jekundu: Cristiano Ronaldo (kushoto) akiwa na mpenzi wake, Irina Shayk na mtoto wao wake wa kiume katika sherehe za tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or zilizo fanyika jana mjini Zurich, Uswisi.
1389634176168_lc_galleryImage_ZURICH_SWITZERLAND_JANUAR.JPG
Uso wa mbuzi: Lionel Messi na Antonella Roccuzzo waliwasili kwenye sherehe Ballon d'Or wakiwa wamekasirika

1389632520802_lc_galleryImage_ZURICH_SWITZERLAND_JANUAR.JPG
Franck Ribery naye alifika na mpenzi wake, mwanamitindo Adriana Lima





 
Huyu jamaa mwenyewe anamkubari Messi ndio maana tuzo nyingi ambazo ametajwa na Messi huwa haendi. Safari hii alijua atachukua sababu jamaa alikua majeruhi kwa muda mrefu.
 
Adriana Lima ni MPENZI wa Ribery?
Mmepeleka uGlobal Publisher hadi Zurich!
Mkiona mtu kasimama na mtu kwenye picha ni mpenzi wake!

Adriana ni mke wa mtu,kaolewa na Marko Jaric.A professional basketball player! A former Real Madrid player anayechezea Montepaschi sasa na ana watoto wawili na huyu manzi!

Sasa hii tabia ya uGlobal Publisher ya kutranslate kila picha ya watu wawili jinsia tofauti ni wapenzi ibaki huku huku +255
 
Afadhali. Kwa kweli ronaldo anastahili haswa tuzo hii, kwa kiwango alichoonesha kwa mwaka mzima! Mungu amzidishie
 
Huyu jamaa mwenyewe anamkubari Messi ndio maana tuzo nyingi ambazo ametajwa na Messi huwa haendi. Safari hii alijua atachukua sababu jamaa alikua majeruhi kwa muda mrefu.

mkuu Likwanda ni mwaka gani ambao MESSI alishnda tuzo hyo na CR7 hakuudhuria..

huu ushabiki wenu wa kijinga unawadhalilisha sana..
 
Last edited by a moderator:
mkuu Likwanda ni mwaka gani ambao MESSI alishnda tuzo hyo na CR7 hakuudhuria..

huu ushabiki wenu wa kijinga unawadhalilisha sana..
huyu jamaa analeta umbea,tuzo ambayo Ronaldo hakuhudhuria ni moja tu ya mwanasoka bora wa Ulaya (mwakajana) ambapo tuzo alichukua Ribery,sikumbuki kama kuna nyingine
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom