Ronaldo apewa jezi namba 7 na Cavani kuchukua namba 21 Manchester United

Ronaldo apewa jezi namba 7 na Cavani kuchukua namba 21 Manchester United

Jezi namba 7 pale katika viunga vya Old Traford Manchester United huwa inajulikana ni ya nani 😇 Ronaldo na tayari kachukua namba yake huenda Cavan akavaa jezi namba 21 ambayo anaitumia timu taifa na kwenye vilabu vingine alivyochezea.

Screen-Shot-2021-09-03-at-10.55.16.png

Mwanzo jezi namba 21 pale Man United alikuwa akiitumia Daniel James ambaye kwa sasa ameondoka na kujiunga na Leeds United.

Baada ya Cristiano Ronaldo kupewa jezi namba 7 katika klabu ya Manchester United ambayo alikuwa anaivaa Cavan sasa Cavani amechukua namba 21 aliyokuwa anaivaa Damiel James ambaye ameuzwa Leeds United.
Ronaldo ni noma kaisaidia timu yake ya Taifa kwa kufunga magoli 2 dakika za mwisho kwenye mashindano ya kufuzu kombe la Dunia na kukaa kileleni tena ugenini, hongera Sana.
 
Humo ndani atakuwa anacheza peke yake? Ni kama kule Juventus star yuko peke yake wengine ni vilaza vilaza

Nani kilaza pale juve? Dybala naye ni kilaza??

Juve kila mwaka anabeba ndoo za ndani hili mbona linajulikana mzehe,,, sema tu ameenda kujiongezea vikombe kupitia migongo ya wengine,,,
 
BAADA ya kukabidhiwa jezi yake aipendayo namba 7 sasa ingizo jipya ndani ya Manchester United, Christiano Ronaldo ambaye aliibuka katika kikosi hicho akitokea Klabu ya Juventus anatarajiwa kuanza kazi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United.
Mchezo huo ambao unapigiwa hesabu na mashabiki wengi duniani unatarajiwa kuchezwa Septemba 11 na itakuwa ni Uwanja wa Old Trafford.

Tayari Ronaldo amewasili ndani ya Jiji la Manchester kujiunga na timu hiyo baada ya kukamilika kwa utaratibu wa usajili wake na anarejea hapo baada ya kuitumikia timu hiyo kuanzia mwaka 2003 mpaka 2009.

Mbali na kushiriki Ligi Kuu England staa huyo amejumuishwa kwenye wachezaji ambao watashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu na anapewa matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho Ronaldo kucheza na Newcastle United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England alifunga hat trick na ubao wa Uwanja wa Old Trafford Januari 12,2008 ulisoma United 6-0 Newcastle.
 
Back
Top Bottom