Ronaldo de Lima abatizwa na kuwa Mkristo!

Duh! Sijasoma comments za akina FaizaFoxy na wenzake wale wa nyuzi zile. Ni mnyukano wa wakristo wenyewe kwa wenyewe, wengine hawaelewi kitu kuhusu ubatizo, wanapita kimya kimya. Ubatizo wa maji kidogo ulianza pale yule mfalme wa rumi alipokubali kuwa mkristo, wakambatiza kistarabu kwa maji kidogo kama kumuheshimu badala ya kumpeleka mtoni kumzamisha. Ikawa ni mapokeo hadi leo ingawa kuna madhehebu hayakubaliani na ubatizo wa maji ya kunyunyuziwa kidogo kichwani. Ubatizo halali ni kuzamishwa na kuibuliwa katika maji mengi. Maana yake ni kuuzika utu wa kale na kuibuka utu mpya, yaani unakuwa mtu mpya katika maisha mapya ya kikristo, sawa na kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
 
Sio ubatizo huo
 
Asante sana Mkuu... Nimejifunza jambo hapa maana ilikua inanipa ukakasi.. kumbe kuna jamii ina refer zaidi ubatizo wa Yesu kule mtoni na wanasahau kuwa mitume walipo pewa uweza waliendelea kubatiza hata nje ya hiyo mito

Thanks Brother [emoji120]
 
Inafikirisha sana.Ni sawa sawa na mtu anaposema kuongelea alafu akasema hata ukiingiza mguu mmoja tu kwenye maji ni kuogelea.Wakati maana na amntiki nzima ya mtu anayepiga mbizi lazima awe kwenye maji
Suala la ubatizo tukiacha ushabiki wa kidini liko wazi sana.Hata ishu ya kilevi inaweza kuwa debatable ila siyo ubazo.Kwanza neno lenyewe tu ubatizo.Ni kitu kilichotowezwa au zamishwa.
Shida moja tunapenda sanadini zetu kuliko uhalisia na ukweli wa mambo.Tuache ukatoliki,uprotestanti au upentekoste.Tuache maandiko yaongee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…