Ronaldo de Lima: Barcelona hawana Upendo na Wachezaji wa Kibrazil

Ronaldo de Lima: Barcelona hawana Upendo na Wachezaji wa Kibrazil

Ha h ha unategemea nini wakati yeye ni Madrid DNA kipindi alichocheza Barca alikua underground kama Paco Alcacer

Mkuu Unasema Underground Wakati Aliondoka Barcelona Akiwa Mchezaji Bora Dunianai na Kwa Wakati Huo Alihamia Inter Kwa Uhamisho Wa Rekodi Ya Kuwa Mchezaji Anaelipwa Pesa Nyingi Dunianai???

Kupenda Mpira Karibuni Kunawasumbua Kweli....

Kwa Kukusaidia tu Ni Kuwa RONALDO anakwenda Kombe la Dunia Mwaka 1998 Akiwa Ndiye ICON Wa Mashindano Kama Ni Top Star asiyekaribiwa na Mchezaji Yeyote yule...

Kabla Ya Kucomment Kwanza Uliza Wanaojua.
 
sio Wabrazil tuu hata ambao. sio. asili ya Catalumya wanatengwa na mwisho sanaondoka kwa fedheha.. ref Erick Abidal na Samuel Etto

Hata Yaya Toure tunajua Kilichomfika Barcelona! Aliondoshwa Akiwa na Uwezo...

Dany Alaves Kaondoshwa Barca Akiwa na Uwezo...

Rivaldo Akiwa Ni Mchezaji Bora Duniani Mwaka 1999/2000 Katengwa Na Barcelona na Kuondoshwa.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Ni chuki binafsi kabisa huyo mshamba, au zimemruka kidogo!!!__ Najua anaumia kuona Mwajentina/King Messi bado ni icon wa Barcelona na alitamani Neema ndio awe top pale kwa sasa__lakini bahati mbaya ama nzuri Messi mwenyewe bado anauwasha moto zaidi ya huyo bishoo neema wao, na sitaki kuona bishoo anafananishwa na King, hana hadhi. pili Gaucho starehe zilimponza na kiwango pia kilishuka sana likajinenepea hata kukimbia ni shida. na ifahamike kwamba "mchezaji mzuri ni pamoja na nidhamu" MESSI ni mfano bora kabisa wa kuigwa! Nimemaliza
 
Mchukue Mess, CR7, Ronaldinho, Neymay ukijumlisha uwezo wao utapata uwezo halisi wa Ronaldo de Lima-9.
 
Mshambuliaji gwiji huyu amefunguka maneno haya wakati akimshauri kijana Coutinho juu ya uhamisho wake kwenda pale Barcelona.

Ronaldo amefunguka na kusema Barcelona hawana upendo na wachezaji wa Kibrazil akiwemo yeye mwenyewe wakati akicheza ndani ya wababe hao wa pasi nyingi pale jimbo la catalunia,ameenda mbali zaidi na kutaja wachezaji kama Romario,Rivaldo na fundi Ronaldodihno na kusema wote hawa hawajaondoka vizuri pale Barcelona.

Pia ametoa mfano wa siku za Karibuni juu ya kijana Neymar na kusema naye hajaondoka vizuri pale Barcelona na kusema mpaka leo kuna kesi juu ya uhamisho wake kwenda kwa matajiri wa Paris PSG(Paris saint German).

Binafsi napenda soka zuri la Barcelona ila haya maneno ya Ronaldo de lima yameniacha na ukakasi kidogo tukumbuke kijana mwingine wa Kibrazil Paulinho yupo pale Barcelona na amekua akipewa muda wa kutosha tu wakucheza na wakali hao wa Katalunia.

Je maneno ya Ronaldo yanaukweli ndani yake au ni chuki binafsi tu?ni muda wa Coutinho kuamua mbivu na mbichi.
Maneno yana ukweli mwingi sana
 
Hata Yaya Toure tunajua Kilichomfika Barcelona! Aliondoshwa Akiwa na Uwezo...

Dany Alaves Kaondoshwa Barca Akiwa na Uwezo...

Rivaldo Akiwa Ni Mchezaji Bora Duniani Mwaka 1999/2000 Katengwa Na Barcelona na Kuondoshwa.
Hata Eto aliondolewa ili asiwe best scorer of all time pale Barca
 
Hata Eto aliondolewa ili asiwe best scorer of all time pale Barca
Si kweli mkuu

Eto'o hakuwa kwenye mipango ya Guardiola na alikuwa discarded na Pep ,..klabu huheshimu maamuzi ya mwalimu

Hata case ya man city toure alikuwa lulu city but vipi pep alivyochukua timu ?

Hoja yako naipinga
 
Hata Yaya Toure tunajua Kilichomfika Barcelona! Aliondoshwa Akiwa na Uwezo...

Dany Alaves Kaondoshwa Barca Akiwa na Uwezo...

Rivaldo Akiwa Ni Mchezaji Bora Duniani Mwaka 1999/2000 Katengwa Na Barcelona na Kuondoshwa.
Kwanini Toure aliondoshwa? Swali zuri mwalimu Guardiola alimuondoa Toure ,Toure hakuwa kwenye mipango ya Pep na ulaya timu huheshimu mipango ya kocha..Toure city si alikuwa lulu vipi Pep alivyotua city ? Toure kawekwa bench ..mpaka hapa point point yako nimei-crush problem sio Barca mwalimu Pep hakumtaka Yaya

2.Rivaldo aligombana na Van Gaal sababu kubwa ilikuwa position na Van Gaal akamweka mkeka Rivaldo na kusema hamtaki aondoke ,Rivaldo akatimkia Milan..Rivaldo saizi ni global ambassador wa Barca ila mpaka sasa Ana bifu na Van Gaal

Bado sijaona point yako mpaka sasa hivi
 
Hata Yaya Toure tunajua Kilichomfika Barcelona! Aliondoshwa Akiwa na Uwezo...

Dany Alaves Kaondoshwa Barca Akiwa na Uwezo...

Rivaldo Akiwa Ni Mchezaji Bora Duniani Mwaka 1999/2000 Katengwa Na Barcelona na Kuondoshwa.

Pedro, Sanchez, thiago, david villa, fabregas, ibrahimovic, wote wameondoka barca wakiwa na uwezo. Mbona hao hamsemi ni ubaguzi. Kwani barcelona hawaruhusiwi kuuza wachezaji weusi?...dani alves kacheza barca miaka karibu 10 ila juve katimuliwa baada ya msimu mmoja tu japo alikuwa beki bora wa uefa ila walishindwa kumvumilia. Barca waliokaa nae miaka 10 ndio wabaguzi?
 
Mshambuliaji gwiji huyu amefunguka maneno haya wakati akimshauri kijana Coutinho juu ya uhamisho wake kwenda pale Barcelona.

Ronaldo amefunguka na kusema Barcelona hawana upendo na wachezaji wa Kibrazil akiwemo yeye mwenyewe wakati akicheza ndani ya wababe hao wa pasi nyingi pale jimbo la catalunia,ameenda mbali zaidi na kutaja wachezaji kama Romario,Rivaldo na fundi Ronaldodihno na kusema wote hawa hawajaondoka vizuri pale Barcelona.

Pia ametoa mfano wa siku za Karibuni juu ya kijana Neymar na kusema naye hajaondoka vizuri pale Barcelona na kusema mpaka leo kuna kesi juu ya uhamisho wake kwenda kwa matajiri wa Paris PSG(Paris saint German).

Binafsi napenda soka zuri la Barcelona ila haya maneno ya Ronaldo de lima yameniacha na ukakasi kidogo tukumbuke kijana mwingine wa Kibrazil Paulinho yupo pale Barcelona na amekua akipewa muda wa kutosha tu wakucheza na wakali hao wa Katalunia.

Je maneno ya Ronaldo yanaukweli ndani yake au ni chuki binafsi tu?ni muda wa Coutinho kuamua mbivu na mbichi.
..Kwani upendo na kupewa nafasi ya kucheza kuna muingiliano upi?....Hawana Upendo ni kwamba Barca wanamtumia mtu kama big G hamuwezi kimaliza kwa Amani na Timu hiyo iliyojaa wabinafsi....Ronaldo yupo sawa 100%
 
Screenshot_2018-01-02-19-38-34.png
Halafu kuna lijamaa lililokunywa mbege linAtema shudu2......,c,hawa hapa wa brazuka wenzake.....,linataka aende Madridogs ama......,
 
Samuel Etoo alikuwa Mbinafsi na Pep kwa Falsafa yake hakutaka Mchezaji Mbinafsi akamuuza etoo akamreplace na zlatan
Baada ya kum replace na zlatan nini kilitokea je na zlatan alikua mbinafsi?
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom