MIZANIA Ronaldo hajawahi kufunga goli la Offside

MIZANIA Ronaldo hajawahi kufunga goli la Offside

Taarifa hii imeachwa katika mizani ya wasomaji wapime uzito wa hoja za kila upande
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na Taarifa hii, wanadai Cristiano Ronaldo ana rekodi kwamba zaidi ya magoli 890 aliyofunga hakuna hata moja lililobainika kuwa na mashaka ya Offside. Je Kuna ukweli hapa?

Screenshot_20241027-100456.jpg

 
Tunachokijua
Cristiano Ronaldo ni mchezaji maarufu wa soka kutoka Ureno anayefahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kucheza na kufunga mabao. Ana historia nzuri ya kucheza na klabu kama Manchester United, Real Madrid, Juventus, na sasa Al-Nassr huko Saudi Arabia, pamoja na timu ya taifa ya Ureno.

Mnamo Agosti 8 ukurasa wa Instagram unaotumia jina la Ronaldo_Era7 ulichapisha andiko likiwa na Takwimu linalodai kuwa Ronaldo amefunga magoli 895 lakini hakuna goli Hata Moja lililokuwa na mashaka ya kuwa alikuwa Offside (Soma hapa).

Offside katika Soka inatokea pale ambapo mchezaji yupo karibu na goli la wapinzani kuliko mpira na mchezaji wa mwisho wa timu pinzani (isipokuwa golikipa) wakati mpira unachezwa kwake

Upi uhalisia wa hoja hiyo?
JamiiCheck imefanya ilufuatiliaji wa kimtandao kwa kutumia neno 'Ronaldo Offside Goal' ambapo majibu mengi yanaleta mchezo kati ya Real Madrid (akiwa na Ronaldo) na Bayern Munich uliofanyika tarehe 18 Aprili 2017 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League).

Katika mchezo huo, Ronaldo alifunga magoli matatu lakini goli la pili (kwenye video hapo juu) ambalo mwamuzi alilikubali liliibua mjadala na wengi wakidai halikuwa goli halali na ilipaswa iamuliwe kuwa offside.

Mashabiki na wataalam wengi wa soka walibishana kama kweli alikuwa kwenye nafasi ya offside au la wakati wa kufunga goli.

screenshot_20241029-062912_1-jpg.3137853

Mstari unaoonesha Ronaldo alizidi sekunde chache Kabla ya kufunga goli

Hata hivyo JamiiCheck inaliacha jambo hili kwenye mizania ya Wadau wake wasome na kutazama ili kutoa maoni yao.
Back
Top Bottom