Ronaldo: Vini Jr alistahili kushinda tuzo ya Ballon d'Or

Ronaldo: Vini Jr alistahili kushinda tuzo ya Ballon d'Or

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Nyota wa Ureno na Klabu ya Al Nassr, Cristiano Ronaldo ametamka hadharani kwamba, Vinicius Jr alistahili kushinda tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu. Ronaldo amezungumza hayo mbele ya wahudhuriaji wa tuzo za Globe Soccer.

"Kwa maoni yangu [Vinicius Jr alistahili kushinda, ilikuwa sio haki, alistahili kushinda na ninasema hapa mbele yenu nyote. Walimpa Rodri, alistahili pia lakini nafikiri walipaswa kumpa Vinicius kwa sababu ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa na alifunga bao kwenye fainali. Mambo mengine hayana umuhimu pale unapostahili, unapaswa kumpa anayestahili. Ndio maana nazipenda hizi tuzo Globe Soccer, mnafanya tuzo zenu kwa haki." - Cristiano Ronaldo

Soma, Pia:

Rodri ashinda Ballon d’Or 2024, kiungo mkabaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo

Majina ya Vinicius Jr na Jude Bellingham yaondolewa kwenye Viti vyao katika Hafla ya Ballon d’Or usiku huu
 
Kushnehi, babu atulie na penati zake.
Anahis Madrid ndo timu ya dunia, haina wakina Modric, Tony, Benzena na Ramos wakiwa kwny ubora wao, vimebaki vitoto vyenye utoto mwingi.
 
Huu ndio ukweli japo saizi haya makundi ya u team Messi vs Ronaldo yamechangia sana kuharibu thinking capacity ya watu.

Kwasababu ya kuendeshwa kihisia watu wanajikuta wanauacha ukweli kwasababu unaenda tofauti na hisia zao.
 
Ngoja nione kama Mo Salah ataipata hii tuzo, Allah anijaalie umri mrefu
 
messi,ronaldo,rodri wezi wa ballo d'or
 
Back
Top Bottom