Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
ro7 lazima ahame
ro7 lazima ahame
Pia Ronaldo alikuwa na Historia ya Hat Trick 23 La Liga huku Messi akiwa na 21. Ila kwa sasa wote wapo sawa.
Nampenda sana Messi, hana madoido ya kijinga uwanjani, anachoangalia yeye ni namna gani anaweza akasaidia timu ikapata ushindi ndani ya Uwanja mda wowote.
Nimemuona Ronaldinho akiwa Barca ila kwa Messi hapana aiseee.
Cristiano umri unaenda, Messi ndo kwanza ana 27. Messi ana nafasi kubwa ya kuweka Record nyingi zaidi hapa duniani.
Real wamekuaje tena, walianza vizuri ila baada ya kupigwa pigwa na Atlet baasi kila kitu kikaanza kufa taratibu.
Wasipokuwa makini ndo basi tena
Halafu Penaldo huwa ana magoli mengi kupitia penalties...
Hii ipo misimu karibia yote aliyocheza Madrid...
Hadi sasa kwa msimu huu kati ya hayo magoli 28 ya Penaldo, magoli 8 ni kupitia matuta wakati Messi katika magoli hayo 26 ana magoli 2 tu ya matuta...
Hivyo katika open play, Messi kascore zaidi ya Penaldo aka Crynaldo...
Hapo bado sijataja 13 assists za Messi huku Penaldo akiwa na 10 assists...
Mpaka dakika hii mimi nahesabia Barca wana asilimia 100% ya kombe moja mkononi yaani Copa del Ray.
Madrid hawana matuamini ya Kombe lolote lile, kwenye Lig muda wowote anatoka pale kileleni.
Na mwezi ujao wanapoenda Camp Nou, Barcelona hawawezi kuwaacha.
UEFA anaweza akasogea kimtindo ila sio kuchukua kombe.
Ronaldo mwaka huu habebi Kombe lolote lile akiwa na Madrid na wala kiatu cha dhahabu kubeba kwake ni ngumu sana ijapokuwa alikuwa na mwanzo mzuti. Kutoka magoli 14 mpaka mawili si mchezo.