mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Linaweza kuwa tukio la kushtua na kushangaza, lakini ndio hivyo limeshatokea. Familia ya Mzee Wilson Ogeta (89) hadi sasa imeshindwa kufanya mazishi ya baba yao aliyefariki dunia Januari 10, mwaka huu.
Kwa siku 234, mwili wa Mzee Ogeta umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Utegi wilayani hapa. Hatua hiyo inatokana na kuibuka kwa mgogoro wa ardhi baina ya familia hiyo na mtu anayetajwa kununua ardhi ya mzee huyo, ambaye hata hivyo, Mwananchi halijafanikiwa kumpata kuzungumza naye.
Wakizungumza na Mwananchi kijijini kwao Nyambogo wilayani Rorya, wanafamilia wameiomba Serikali na mamlaka zake kuingilia kati mgogoro huo ili wapate kuuhifadhi mwili wa mpendwa wao kama ilivyo desturi za Watanzania.
Wanafamilia hao walisema mgogoro huo umewaathiri kisaikolojia, kiuchumi na kuwazidishia machungu yasiyokwisha.
Msemaji wa familia hiyo, Isaya Goro alidai kuwa mzee huyo alianza kuugua mwaka 2016 na kupatiwa matibabu kwenye hospitali mbalimbali na Januari 10, mwaka huu alifariki dunia.
Alidai kuwa baada ya kufariki taratibu za msiba zilindelea kama kawaida na kupanga kumzika kwenye mji wake uliopo kijijini hapo, lakini wakiwa katika harakati za maandalizi ya mazishi Januari 15, mwaka huu walipokea hati ya zuio la mahakama likiwataka kusitisha shughuli zote za maziko
“Tukiwa tunajiandaa kuchimba kaburi hapa nyumbani tulipata stop order (zuio la mahakama) tukitakiwa kutofanya kitu chochote katika ardhi hii kwa madai kuwa ni mali ya mtu mwingine na si ya marehemu,” alidai.
Aliendelea kuwa baada ya kupata zuio hilo familia iliamua kwenda mahakamani kwa nia ya kutengua zuio hilo ili waweze kuendelea na mazishi, lakini uamuzi ukawa tofauti, kwani walishindwana wakaamua kwenda kuuhifadhi mwili wa marehemu katika Hospitali ya Utegi wakati wakiendeleza mapambano ya kudai haki.
Familia hiyo ilikata rufaa kupinga uamuzi huo wa mahakama ya wilaya ambapo rufaa hiyo ilianza kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Julai 18, mwaka huu na kutolewa hukumu Julai 22 ambayo pia ilimpa ushindi mnunuzi wa eneo.
Baada ya hukumu hiyo familia haikuwa na namna ya kufanya isipokuwa kuacha mwili kuendelea kuwepo mochwari, huku wakiangalia namna ya kufanya kwa kuwa hawakuwa wametenga eneo lingine kwa ajili ya mazishi.
“Lakini kama unavyoona hadi leo (jana) hatujazika na hatujui nini cha kufanya na tunaamini eneo hili ni mali halali ya marehemu, ingawa mahakama imetoa uamuzi kuwa eneo hili ni mali ya mtu mwingine. Tunaziomba mamlaka husika zitusadie ili tuweze kumzika ndugu yetu wakati huu ambao gharama zinazidi kuwa kubwa zaidi,” alidai Goro.
Akisimulia mgogoro wa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari zaidi ya 40 lilivyouzwa, Goro alidai kuwa mwaka 2016 walipata taarifa kuwa kijana wa kaka wa marehemu aitwaye Lawrence alimuuzia eneo hilo mtu mmoja ambaye hatutamtaja kwa sasa.
Baada ya kupata taarifa hizo, mzee Ogeta hakukubaliana na uamuzi huo kwa kuwa hakushirikishwa yeye wala mtu yeyote wa familia yake, hivyo akapeleka malalamiko katika Serikali ya Kijiji ambapo mnunuzi alitakiwa kumleta muuzaji ili athibitishe madai hayo, jambo ambalo halikufanyika.
Aliendelea kudai kuwa badala yake mnunuzi huyo aliamua kupeleka suala hilo Baraza la Ardhi la Kata ili aweze kutambuliwa kihalali na baraza hilo lilimthibitisha mnunuzi huyo.
Goro, ambaye marehemu ni baba yake mdogo, alidai katika baraza hilo mtu huyo anayedai kununua eneo hilo aliwasilisha nyaraka zake zikionyesha namna ambavyo mauzo yalifanyika na uamuzi uliotolewa ukampa tena haki ya umiliki wa eneo hilo.
Hata hivyo, anadai kuwa nyaraka hizo hazikuwa sahihi kwa kuwa zilikuwa na mkanganyiko, hasa upande wa ushahidi.
Aliendelea kudai kuwa kutokana na maamuzi ya baraza hilo waliamua kukata rufaa kwenda wilayani na kwamba, licha ya kuwepo kwa utata juu ya mashahidi wa mauziano, lakini pia baraza hilo lilitoa maamuzi kinyume cha utaratibu, akisema baraza la ardhi la kata lina uwezo wa kusikiliza shauri lenye thamani isiyozidi Sh3 milioni wakati shauri hilo lilikuwa na thamani ya zaidi ya Sh38 milioni.
Alifafanua kuwa wakati wakiendelea na shauri hilo hali ya mzee ilizidi kudhoofika na kufikia hatua akashindwa kuhudhuria vikao vya baraza hivyo, akamteua yeye (Goro) kumwakilisha katika shauri hilo kisheria.
Kwa upande wake, mtoto wa marehemu, Eliakim Wilson alidai kutokana na hali yao kiuchumi hivi sasa hawana namna ya kupata mahitaji, hasa chakula hivyo kuwalazimu majirani kujitolea kuwapa chakula kila siku.
“Hatuna sehemu ya kulima kwa miaka sita sasa, vilevile tuko kwenye maombolezo na msiba kwa zaidi ya miezi nane sasa. Kila kitu kwetu kimesimama na tunaishi kwa kusaidiwa na majirani,” alidai.
Alidai kuwa ununuzi na uuzwaji wa eneo hilo haukufuata taratibu kwa kuwa kila kitu kimefanyikia Dar es Salaam, huku wahusika wakiwa hawana taarifa.
“Wazazi wetu walikuwa wakiishi hapa na wala hawakuweka mipaka, walikuwa wakilima kwa amani kabisa na kila mtu alikuwa anajua anaishia wapi, lakini huyu ndugu yetu aliamua kuuza lote likiwemo la baba yangu,” alidai.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambogo, Johannes Charles alisema kwa uelewa wake eneo hilo ni mali ya marehemu Ogeta na amekuwa akilitumia kwa miaka mingi na suala la uuzaji wa ardhi Serikali ya Kijiji ingeshirikishwa kila hatua.
Pia, alieleza kushangazwa na uamuzi uliofikiwa na baraza la ardhi la kata ambalo amedai kuwa halikutafuta ukweli kutoka Serikali ya Kijiji na kuziomba mamlaka zifanye uchunguzi.
Baadhi ya majirani walisema kuwa walishangazwa na taarifa za kuwa eneo hilo linamilikiwa na mtu mwingine tofauti na mzee Ogeta, ambaye amekaa katika eneo hilo miaka yote ya uhai wake hivyo kuomba uchunguzi wa kina ufanyike.
“Wanamtesa tu marehemu bila sababu kwa uamuzi ambao umeleta madhara makubwa kwa familia, mamlaka zichukue hatua ili mzee wetu apumzishwe kwa amani,” alisema Anderikus Kateti.
Mgogoro huo uliwahi kuifikia Takukuru ambayo kamanda wa Mkoa wa Mara, Hassan Mossi alipoulizwa alisema walifanya uchunguzi na hawakuona tatizo hivyo akawashauri wanafamilia wakubailiane ili taratibu za mazishi ziweze kuendelea.
“Tuliona kuna nyaraka zote na hivyo hatukuona kama kuna jambo tunatakiwa kufanya zaidi ya kuwapa ushauri waende wakae pamoja kumzika marehemu,” alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka alisema baada ya kupata taarifa za mgogoro huo aliwaita ndugu wa marehemu na mnunuzi na kuzungumza nao na kukubaliana kutafuta eneo lingine ambalo familia itaona linafaa kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika leo.
Chanzo: Mwananchi
UPDATE
- Rorya: Mwili wa aliyekaa mochwari miezi nane azikwa