Wapendwa
Habari za uzima?
Nimepokea taarifa kutoka Mkoani Mara wilaya ya Rorya kata ya kowaki mtaa wa Labuor kwamba watu watano(5) wamesombwa na maji.
Kati ya hao wa 5, 3 ni wana wa kike( wanawake) na wawili(2)ni watoto.
Walikua wanavuka kutoka upande mmoja wa mto mori kwenda kwa ibada siku ya leo. Ila hawakuweza kufika upande wa pili kwa sababu ya mkondo mkubwa wa maji uliopelekea mtumbwi waliokua nao kuzama.
Hadi mda huu miili ya watu wa 4 inatafutwa wakati mtoto mmoja akipatikana amefariki.
Poleni Tanzania poleni waumini wa kanisa la sabato hapo kowaki-labuor huko duduu.
UPDATE
Watu watano wanadaiwa kufariki dunia baada ya mtumbwi uliokuwa unatoka kijiji cha Kowak kwenda kijiji cha Ruanda kata ya Kigunga Wilayani Rorya kuzama baada ya kubeba watu wengi kuliko uwezo wake
Akizungumzia tukio hilo lililotokea Mei 7, Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka amesema waopoaji wamefanikiwa kuopoa miili 4 huku jitihada za kuutafuta mwili 1 unaosadikiwa ni wa mtoto wa miaka 5 zikiendelea
Aidha amesema Serikali itatoa utaratibu rasmi wa namna ya kuvuka kwa usalama baada ya miili yote kupatikana na kuzikwa
UPDATES( 9/5/2022)
Jana walitolewa wanawake wawili, leo katolewa mwanamke mmoja. Hivyo miili iliyo opolewa imefika minne, mtoto mmoja wa miaka minne, wamama watatu bado mtoto mmoja wa miaka nane.
................
.................
TAARIFA MPYA YA MAREKEBISHO NI KWAMBA, WATU WALIOKUA WAKIVUKA MTO MORI KWA KUTUMIA MTUMBWI WALIKUA TISA NA NAHODHA WA MTUMBWI JUMLA KUMI.
KWA SABABU YA KASI YA MAJI, MTUMBWI ULIFUNGWA KAMBA, KAMBA IKATUPWA UPANDE WA PILI WA MTO ILI MTUMBI UPEWE SAPOTI NA VIJANA WALIOKUA UPANDE WA PILI.
MAJI YALIKUA NA NGUVU KUBWA NA MTUMBWI ULIKUA NA WATU WENGI JAMBO LILILOPELEKEA KAMBA ILE KUKATIKA.
BAADA YA KAMBA KUKATIKA VIJANA WALIOKUA WAMEISHIKILIA UPANDE WA PILI WALIKIMBIA. LAKINI NAHODHA ALIFANIKIWA KUOKOA ABIRIA WA 4. WATANO WAKASOMBWA NA MAJI.
KATI YA HAO WATANO, WA 4 WAMETOLEWA WAKIWA WAMEFARIKI NA ANATAFTWA HUYO KIJANA MMOJA WA MIAKA 8.
SANJARI NA HILO, KUNA MTU MMOJA PIA ALIZAMA UTEGI NA AMETOLEWA MTO MORI AKIWA AMEFARIKI HUKO KOWAKI.
TAARIFA ZAIDI ZINASEMA, KATI YA WATU WANNE WALIO OPOLEWA, MMOJA NI MAMA ALIEKUA NA MIMBA PAMOJA NA MTOTO WAKE AMBAO WOTE WAMEFARIKI.
LAKINI PIA, MTOTO MWINGINE ALIYEFARIKI PIA ALIKUA ANAVUKA NA MAMA YAKE. MAMA WA HUYU MTOTO ALIEKUA KABEBA MTOTO MWINGINE MGONGONI ALIOKOLEWA AKIWA HAI PAMOJA NA MTOTO WAKE. LAKINI MTOTO WAKE MMOJA HADI SASA NDIE HAJAPATIKANA, MTOTO ALIEKUA ANAWEZA KUTEMBEA. WAKATI MWINGINE ALIKUA KAMFUNGA MGONGONI.
DINI LA HAWA WATU NI WATU WANAOSALI JUMAMOSI, WANAKUA NA ALAMA YA MSALABA MWEKUNDU, WANAITWA JO-ROHO.