Huyu Rose Mayemba Mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA namfananisha na Kamala Harris wa Marekani hapa Mdee na Bulaya wakasome
Nimesikiliza wanasiasa wengi sana hapa Tanzania na Africa huyu binti ni tunu na hazina ya Taifa.
Rose Mayemba nimempenda bure huyu dada.
===
Your browser is not able to display this video.
Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA Rise Mayemba , amesema kuwa kampeni ya No Reforms No Election siyo tu harakati za madai ya uchaguzi huru na haki, bali ni mapambano ya kurejesha rasilimali za nchi mikononi mwa Watanzania.
Akihutubia kwenye mapokezi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, wilayani Ikungi mkoani Singida, Mayemba alisisitiza kuwa kampeni hiyo inalenga kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na utajiri wa nchi kwa usawa.
"Hii ni kampeni ya kuondoa nchi kutoka mikononi mwa wachache na kuirejesha kwa wananchi wengi. Ni mapambano ya kuzinusuru bandari zetu, madini yetu na rasilimali za taifa ambazo zimeporwa na wachache," alisema Mayemba huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.
Aliongeza kuwa mchakato huo hautakuwa rahisi kwa sababu mfumo uliopo unanufaisha wachache, lakini akasisitiza kuwa Watanzania wakisimama kwa umoja wanaweza kufanikisha mabadiliko hayo.
"Kama keki ya taifa itagawanywa sawa, kila mmoja atapata haki ya kutibiwa hospitali wanazotibiwa wao na watoto wao, kusomesha watoto wao kwenye shule bora wanazosomesha watoto wao, na kufaidika na rasilimali za nchi hii," aliongeza.
Kampeni ya No Reforms No Election inahamasisha mageuzi ya mfumo wa uchaguzi ili kuhakikisha haki na usawa kwa vyama vyote vya siasa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu. CHADEMA na viongozi wake wameendelea kusisitiza kuwa bila mabadiliko hayo, hawatashiriki uchaguzi ujao.
Mapokezi ya Tundu Lissu wilayani Ikungi yamevutia maelfu ya wananchi na wafuasi wa CHADEMA, wakidhihirisha kuongezeka kwa mwamko wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Huyu anapaswa kuwa CCM tu mahali ambapo kumejaa akili kubwa. Anajiamini sana katika kuzungumza japo anazungumza mambo ambayo ndio kiu ya Rais Samia na CCM kuhakikisha kuwa Watanzania wanaishi maisha bora na yenye heshima na keki ya Taifa inagawiwa kwa Usawa.. Ndio maana leo tunaona Elimu bure tena Elimu yenye ubora na viwango vya kimataifa,ajira kwa vijana ili vijana wapate kulitumikia Taifa lao na kutoa Mchango wao kwa Taifa.
Huyu Dada ni lazima aingie ndani ya CCM kujiunga na Jeshi la Wazalendo.
Dada yangu huyo wa ihalula uwemba njombe, namkubali sana nilifanya nae kampeni ya lowasa ulipo tupo mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu, aondoke chadema wanamdharau sababu hatoki kaskazini