Rose Mayemba, Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Njombe akamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi. Aachiwa kwa dhamana

Rose Mayemba, Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Njombe akamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi. Aachiwa kwa dhamana

Rose Mayemba ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe anahojiwa na RCO wa Mkoa huo kwa tuhuma nzito za kumkashifu Rais wa Tanzania kwa kutweet mambo ya Katiba mpya mtandaoni....
Mmm hapana Rais ana wajibu kukemea viashiria uvunjifu amani....siosawa kumkashifu nasimama na Rais kwa hili
 
😀 Hatachukua round mtamfanyaje nyie nyumbu?. Mama yuko in a right track sasa miruzi yenu ilianza kumpoteza maboya. Tena anatakiwa akaze zaidi na zaidi.
Hivi viapo vina nguvu katika ulimwengu mwngine. Mwenzake yuko anapats haki yake huko aliko.

Hili liwe somo kwa watawala Ukiapa kulinda katiba usilete Usanii
 
Kakamatwa huyo dada yupo ndani bila sababu yeyote

Yale mambo ya kuwekwa korokoroni yameanza tena

Hayo niliyategemea kabisa, ogopa chama kilicho madarakani kwa wizi wa kura halafu kisikie kuna ajenda ya kuzuia viongozi kukaa madarakani bila ridhaa ya wananchi. Sasa hivi lile kundi la watu wasiojulikana ni lazima lirudi kwa kasi. Tunaodai katiba mpya tuidai bila kuchoka maana ni madai halali, hivyo wafaidika wa huu mfumo mbovu lazima wafanye ukatili kukataa jambo hilo..
 
Yaani tunataka kweli kurudi kule kule?
----
Update: 1
JamiiForums imezungumza na RPC Mkoa wa Njombe na amethibitisha kuwa Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Njombe Rose Mayemba amekamatwa kwa Mahojiano zaidi baada ya kuweka ujumbe kwenye mtandao wa kijamii uliomhusisha Rais. RPC amesema kuwa kosa lake lina dhamana na ataachiwa nje ya dhamana.

Update: 2
Rose Mayemba amepata dhamana baada ya kutoa maelezo kwa muda wa saa mbili na kutakiwa kuripoti Ofisi ya RCO Njombe siku ya Jumatatu saa 2:00.


Ujumbe unaodaiwa kumuingiza matatani Rose Mayemba
View attachment 1845997
Pambana dada hakika usirudi nyuma kuusema ukweli.
 
Mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Njombe mh Rose Mayemba ameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena ofisini kwa RCO siku ya Jumatatu.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
#KaziIendelee
#NchiKwanza
#UtiiWaSheriaBilaShuruti
#Mh.RaisSSHHoooyeee
 
Wewe ndiyo hufai !! Kosa la huyo dada liko wapi ?! .

Police watamharibia mama CV muda usio mrefu
 
Kutokana na N'TU na N'TU jaribu wewe uone.
 
Back
Top Bottom