Rose Mhando na Ngololo ya Diamond

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Wadau wa muziki wa Injili salaam.

Nimeona sehemu ya mahojiano ya msanii wa muziki wa Injili katika kituo kimoja cha Television na kama kawaida kuna wimbo wake mmoja ulichezwa. Katika video yake nimeona kidogo kama wachezaji wanaingiza staili ya ngololo ya Diamond.

Kwa mshangao wangu,kukawa na kikolezo katika wimbo cha maneno "wololo!"Wakiimba kama "ngololo!" Ya Diamond. Kwa vyoyote vile LAZIMA kuna mmoja wao kati ya Rose Mhando na Diamond mmoja kakopi kwa mwenzake!Ningesema huenda producer wao alikuwa mmoja lakini Rose ametengeneza SA wakati Diamond kafanya Kenya kama sikosei.

Hii imekaaje kutuletea ngololo kwenye gospel?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kama hujui kaa kimya!!
Aliekuambia diamond kafanyia Kenya nani?
Umasikin unachosha acha Rose atafute pesaa
 
Kama hujui kaa kimya!!
Aliekuambia diamond kafanyia Kenya nani?
Umasikin unachosha acha Rose atafute pesaa

Sasa mkuu nikikaa kimya nitajuaje?Wewe unayejua naomba unieleweshe.Sina tatizo na Rose Mhando kuhusu kutafuta pesa na hata kama anafanya hivyo kwa kuiga mitindo ya kidunia,kitu ninachotaka kujua,ni kwa nini kumekuwa na similarities kama hizo?je ni coincidence tu?!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ngololo ya diamond ame copy azonto ya nigeria amebadili jina tu. Hivyo ni vionjo tu si kwamba unaweza chukua popote pale. Kwani bongo flava ni nini...kuna mchanganyiko gani ndani yake.hata wasanii wa us wanacopy vionjo vya afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…