GE2025 Rose Rwakatale achukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Mlimba, Morogoro

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kipindi kile alimgaragaza Magu aliingilia kati
 
Huyu alikuwa namba Moja katika kura za wajumbe lakini Magu alimpitisha yule dogo Kunambi!!
Magufuli amembeba mnoo Kunambi, kisa alikuwa mwanasheria mwandamizi wa CCM na mwisho akampa uDED hapo Dodoma mjini. Kunambi ni mtu wa Magufuli wa kufa na kuzikana, na kwa sasa ni adui mkubwa wa Samia.

Maisha huwa yanabadilika sana sponsor akikata moto.
 
Kwa Sasa hapa TZ kama unautaka ulinzi wa kulinda mambo yako lazima uwe na CCM , huu ni Ukweli mchungu ambao wafanyabiashara lazima tuujue, dawa chungu sanaaa lakini inabidi tuinywe. Wabunge karibu asilimia 98 unaowaona wapo kwaajili ya kulinda Mali zao, biashara zao, vyote vizuri vilivyo kwao aidha Kwa njia halali au haramu...Matajiri wengi wakubwa unaowaona TZ wako pamoja na CCM na wako tayari kutoa chochote kile wanachoombwa, tena si kuombwa bali wanatoa wenyewe Kwa hiari Yao. Dawa chungu sana hii. Kama taifa ndio tumefika huku Sasa, so sad.
 
Magufuli alimkataa huyo Rose kwa sababu zipi?
Upande mmoja kwa sababu Rose alihusishwa na kutoa rushwa sana huku akihushwa na utitiri wa deal chafu. Hivyo panga likamkuta.

Upande wa pili ni kwa sababu aliyetakiwa kupewa Ubunge alikuwa ni Kunambi, mtu wa karibu mnoo kwenye CCM ndani kwa ndani na Magufuli. Hivyo mbereko ikaamua.
 
Reactions: K11
Daah hatari sana.
Kuna msitari mwembamba sana kati ya umafia na utajiri.
Ukiona mtu ana ukwasi wa kutosha, kama wewe ni kapuku kaa nae mbali.
 
Hahaha ndio mambo CCM wanapenda hayo...
Imagine wazazi wanalipia pesa ndefu za school bus, alafu yeye anayatumia Bure , kwenda kubebea wahuni wa kwenye mwenge
 
kulinda himaya zake za kibiashara kupitia parliamentary and diplomatic status

Mengi yalisemwa kumhusu Pastor Mama Rwakatare wakati akiwa hai. Nilipoona hayo maandishi imebidi nitafakari kwamba dhima yake Rose kumbe sio kuwahudumia & kuwawakilisha wananchi wa Mlimba bali hayo maandishi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…