Rostam Aziz akanusha kununua hisa Yanga

Rostam Aziz akanusha kununua hisa Yanga

Hadrianus

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2020
Posts
2,112
Reaction score
5,229
IMG_20200910_182920_630.JPG
 
Sasa mishahara itakuwaje tena na GSM huwa anawasajilia wachezaji kwa mikataba ya miezi sita sita na mishahara kulipa ni Yanga! Hapo namuona Tuisila na Sarpong wakienda Simba mwakani
 
Mfanyabiashara maarufu na mwanachama wa klabu ya Yanga,Rostam Aziz amesema tetesi za kutaka kununua hisa katikaklabu ya Yanga ni za kupuuzwa.

'NIMESHANGAZWA na taarifa zinazoendelea kusambazwakatika mitandao ya kijamii zinazodai niko tayari kuwekeza fedha kiasi cha dola za Marekani milioni 13 na hivyo kununua asilimia 29 ya hisa katika klabu ya Yanga ambayo mimi ni mwanachama wake.

Napenda kutumia fursa hii kutahadharisha umma na wanaYanga wenzangu kwamba, taarifa hizo hazina ukweli wowote. Taarifa kwamba nimetangaza uamuzi huo katika kikao.

Nilichofanya na viongozi wa Yanga ni za uongo. Msimamo wangu kuhusu uendeshaji wa klabu yetu uko bayana kwamba, mimi si muumini wa Yanga kuuza hisa. Wana Yanga tunapaswa kuwa makini na usambazaji wa taarifa za namna hiyo katika mitandao ambayo imekuwa inatumika kuzusha kila aina ya habari.' - Rostam Aziz

Chanzo: Clouds digital
 
Rostam azizi ni mmoja ya watu wanaopinga mabadiliko ndio waliokua nyuma ya marehem mzee akilimali mwenyewe alishawai sema sasa mi binafs nilishangazwa kabdilika ghafla
 
Back
Top Bottom