Rostam Aziz asema nipo tayari kuidhamini Yanga SC

Sawa Mkuu nitaileta yote ila hakuna sehemu aliposema yupo tayari kuifadhili Yanga,Rostam mwenyewe anapinga hilo suala yeye anasisitiza ni jukumu la wanachama kuchangia club yao!
Wapi nimeandika anataka kufadhili?
Hujui tofauti ya udhamini na ufadhili?

Rostam amesema anaweza kudhamini Yanga kupitia moja ya makampuni yake ila hayuko Tayari kufadhili maana kufadhili Ni mlango wa nyuma wa kumiliki kwa anavyo amini yeye.
 
baada ya maigizo ya mahakama ya mafisadi kufikia ukingoni, ufisadi kwenye chama changu CCM sasa umeshamiri rasmi na kwa gea kubwa kuliko awamu zote zilizotangulia.

fedha haramu sasa inatakatishwa kupitia futiboli.

nyie Yanga.... you're better than that bana!
 
hizo 51℅ mmeweka stake gan kama wanachama?...si mkubali tu moo ndiyo mmiliki sababu show nzima kasimamia yeye
49% zote ni za MO,hzo 51% zilizobaki sio za mtu mmoja zimegawanyika gawanyika humo ndo mana wanaona kama team kamiliki Mo
 
Simba wako kwenye uelekeo sahihi kama ilivyo sehemu kubwa ya dunia. Mambo ya ufadhili, udhamini sijui fadhila hayana nafasi. Timu zetu zimekuwa huko miaka nenda miaka rudi, sasa hivi ni uwekezaji tu, na pawepo bodi ya wakurugenzi washughulikie timu kibiashara.

Habari kubwa ni UWEKEZAJI, kila ajue nani anawekeza nini na anapata nini.
 
Huyo Rostam Naye Yupo Kwenye Orodha Ya Ng'ombe Waliokatika Mkia Machungani Akirudi Zizini Wenzake Watamjua Hana Mkia 😂😁😀😀😃😄😅
 
Mambo aliyoongea Rostam Aziz leo.

• Nimewaita hapa ili kuongelea swala la michezo hasa klabu ya Yanga SC.

• Nimepata Simu nyingi kutoka kwa mashabiki, wanachama na waandishi wa habari wakitaka kujua hatma yangu katika kuisaidia Yanga SC.

•Mimi ni mshabiki wa Yanga SC toka nikiwa darasa la kwanza japo nimekuwa kabatini siku zote hizo mpaka hapo majuzi nilipoamua kuujulisha umma.

•Sioni sahihi kwa timu kubwa na yenye historia ndefu kumilikiwa na mtu binafsi.

•Pia sioni uhalali kwa timu kubwa kama Yanga SC kuwa na mdhamini binafsi.

• Yanga ni timu kubwa yenye mashabiki mamilioni sioni sahihi wala sio haki kwa mtu mmoja kujimilikisha.

•Njia sahihi ni wanachama wote wawe na mamlaka kuiendesha timu yao.

•Njia nzuri ni kupitia michango, wadhamini kupitia makampuni,TV rights na gate collection na kuuza bidhaa mbalimbali zenye nembo yetu.

• Unapokuwa na mdhamini mmoja unainyima yanga kupata fursa ya wadhamini wengine.

•Nipo tayari kuendelea kuichangia timu yangu.

•Nipo tayari kuwapeleka nje viongozi wa Yanga SC ili wakapate mafunzo kutoka kwa wataalamu namna ya kuendesha klabu pia wakihitaji ntawaleta hapa hapa wataalamu.

•Tiba ya hili ni kutafuta njia endelevu ya kuendesha timu.

•Napenda kuona Yanga inafanikiwa kupitia umaarufu na idadi kubwa ya wanachama iliyonayo , kutomilikiwa na mtu mmoja kutatoa fursa kwa makampuni mengine mengi kuidhamini.

•Nami ntaangalia kupitia moja ya makampuni Yangu kutangaza bidhaa zake kupitia Yanga, pia nakaribisha makampuni mengine kufanya hivo.

•Ntaonana na viongozi wa Yanga SC ntawashauri mambo kadha wa kadha watakayochukua sawa na watakayoona hayafai pia sawa.
 
Kiukweli timu kumilikiwa na mtu mmoja ni shida pale anapopata matatizo. Nakumbuka kipindi Mo alipokuwa ametekwa mashabiki wa Simba walikuwa kwenye pressure kubwa.
 
Mdhamini tangu lini akataka kukaa na Hati ya Club?
 
Mo ni invester anamiliki 49% japo kwa nje watu wanaona Kama Kila kitu Ni Mo kitu ambacho si kweli Ni upotoshaji tu.

Unamiliki vipi klabu na 49% ?
Acha uongo.. MO hajatoa 20B tulizo kubaliana.. atapataje hiyo 49%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…