Rostam Aziz asema nipo tayari kuidhamini Yanga SC

Rostam Aziz asema nipo tayari kuidhamini Yanga SC

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Bilionea mfanyabiashara na mwanachama wa Yanga Rostam Aziz amesema yupo Tayari kuidhani klabu ya Yanga kupitia moja ya makampuni yake lakini sio kuifadhili au kuimiliki
Akiongea na waandishi wasl habari leo ofisini kwake jijini Dar Ess Salaam Rostam amesema
ROSTAM :"Niko tayari kuidhamini Yanga kuipitia moja ya makampuni yangu, lakini napinga kabisa suala la mtu mmoja kumiliki klabu yenye mamilioni ya watu. Suala la udhamini sawa lakini si ufadhili na umiliki."
Rostam pia ameongeza yupo Tayari kuwashauri viongozi was Yanga namna Bora ya kuingoza klabu katika uongozi endelevu
Rostam" viongozi wa Yanga wakija nitawashauri namna Bora ya kuingoza klabu katika uongozi endelevu."
Rostam amedai klabu ya Yanga Ni klabu ya wanachama na nijukumu la Kila mwanachama kuchangia, Rostam Tayari ameshatoa mchango wake wa milioni 200 Kama alivyoahidi
65289050_1198167323706820_272843531259740160_n.jpeg
 
Habari zimwende Mo anayeta aimiliki timu huku hataki kutoa pesa

Rostam na utajiri wake hapigi kelele huyo mo ndio anatupigia kelele!!
Mo ni invester anamiliki 49% japo kwa nje watu wanaona Kama Kila kitu Ni Mo kitu ambacho si kweli Ni upotoshaji tu.

Unamiliki vipi klabu na 49% ?
 
Hongera Rostam, Yanga changamkiemi fursa hiyo mtumieni Rostam vyema katika ustawi wa klabu.
Ila hapo naona karusha jiwe gizani kwa mikia likampata mooo
Kwani Mo anamiliki klabu gani?
 
Daaaaahhhh hizi siasa zinatupeleka pabaya
Hizi firigisu wanazotengeneza zikifanikiwa sitaki kusikia Simba wala Yanga.
 
Haya majitu ya yanga bure kabisa. Wanadhani kumchonganisha mo na wanachama kwamba anamiliki timu kutawafaidia kitu gani?

hivi wanajua maana ya uwekezaji au kununua hisa? Hau wana bwabwajatu?

pia nampongeza ndugu rasul kwa kuonyesha nia yakutaka kuisaidia timu ya yanga.

nijambo zuri kwa maendeleo ya soka letu. Mimi ni mwana simba ila sina akili za watu wa yanga ambao wanadhani simba ikiwa hoi ndio wao wataendelea wanashindwa kujua hakuna simba imara kama yanga ni dhaifu.

ipa bw rasul ajue bila kuweka mfumo kama wa simba wa kununua hisa namwakikishia pesa zake zitatafunwa na wajanja.
 
Mo ni invester anamiliki 49% japo kwa nje watu wanaona Kama Kila kitu Ni Mo kitu ambacho si kweli Ni upotoshaji tu.

Unamiliki vipi klabu na 49% ?
Usibishane na happiness ohooo! Huyo hakuna ajualo
 
Na huo ndio udhaifu anaotumia ndugu mwekezaji na kwa kuwa mashabiki wengi wa Simba wananjaa ya tumboni huwezi kuwasikia wakihoji
49% zote ni za MO,hzo 51% zilizobaki sio za mtu mmoja zimegawanyika gawanyika humo ndo mana wanaona kama team kamiliki Mo
 
Back
Top Bottom