Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

asante kwa maelezo yako. Una uhakika gani kama habari hii ni ya kupikwa ilihali hauko nyumbani Tz? je ukigeukiwa na kuambiwa kuwa habari uliyotoa wewe ndio ulipika?

I dont know ila kama maelezo ya PM ni kweli, basi Chacha ni mtu hatari sana, hafai kuwa kiongozi!

Hebu nipatie hiyo habari ambayo si ya kupikwa!

Mama
tuachane na hiyo habari tuongee kwa uwazi zaidi

Mama mie nafikiri tuhuma zidi ya chacha kutoka chadema zinajitosha kabisa kumufuta jamaa uanachama wewe unaona je? ktk hilo??

Na kwanini unadhani chadema wanasita kumfukuza uanachama wakati jamaa baada ya kusimamishwa uongozi na kuonywa na uongozi bado anaendelea na mikakati ileile ya kukiharibu chama??
 
Mimi nimeshakubali mkuu

Lakini kwa vitendo vya CHACHA kuendelea kua mwanachama na mbunge wenu ni hatari sana ,HUyu anastahili kutimuliwa uanachama na kuchukuliwa hatua za kisheria

Sio mbunge wetu. Mbunge wa watu wa tarime. CHADEMA wamemsimamisha tu umakamu mwenyekiti watu wote mmewajia juu. Je, wangemfukuza uanachama na kumpeleka polisi je? Nitaendelea kuwapatia habari zaidi kadiri ninavyoendelea kuzipata lakini kwa ujumla mpaka sasa mkakati wa Rostam kujisafisha ni mkali zaidi kuliko wa Lowassa, Karamagi, Chenge na Mkapa. Akifanikiwa kutengeza 'mashujaa' wengi zaidi CHADEMA, kama chama kitaamua kuwafukuza uanachama yeye amepanga kuwagawa nusu- nusu kuwapeleka CCM na kuanza kuishambulia CHADEMA, na nusu watabaki kuwa wanachama wanaoendelea kutetea haki yao ya uanachama mahakamani kwa kuichafua CHADEMA. Katika kundi hili kwa sasa yuko Mzee Yusuph Halimoja, yeye ndiye aliyetumwa kwa mara ya kwanza kuleta hoja ya makundi katika CHADEMA wakati huo akiwa afisa wa mafunzo. Baada ya kile kikao cha kwanza cha Kempinsiki, wakati CHADEMA inaelekea katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti ambapo Chacha aligombea kwa kutumia vipeperushi vya kuita CHADEMA kuwa ni chama chenye ufisadi wa ukabila na ruzuku ambayo yeye alilenga kuuondoa na kuibadili CHADEMA kutoka kuwa NGO, tayari chama kilitaka kuchukua hatua kumwengua kama mgombea kwa kusema uongo na kukiuka maadili ya chama kuhusu ufanyaji wa kampeni safi. Lakini kuona hivyo, kwa ushauri wa wakina Rostam na Ballile ikakubaliwa Chacha Wangwe aje na mkakati wa kusema kuwa anazushiwa yote hayo kwa kuwa Mwenyekiti Mbowe anagombea wake. Na njia ya kufanya hivyo ikawa na kwa Mzee Halimoja kuandika waraka kwa wajumbe wa Kamati kuu na Baraza Kuu la CHADEMA kuwa CHADEMA ina kundi la Mbowe na kwamba Mbowe amepewa majina ya watu 14 wanaomuunga mkono Chacha ili kama akishindwa waondolewe. Mkakati huu ulifanya kazi vizuri kwani ulifanya wajumbe wa Kamati kuu waiishie kumpa onyo Chacha kwa kufanya kampeni za kukipaka matope chama lakini hawakuchuja jina lake kuepusha Chacha kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa amechujwa kuwa alikuwa akigombea akiwa na sera ya kupinga ukabila na ufisadi katika matumizi ya ruzuku. Mwenyekiti Mbowe kama sehemu ya demokrasia ingawa halimoja hakuwa mjumbe wa Kamati Kuu akamwelekeza Dr Slaa aje alete mbele ya Kamati Kuu barua yake kuhusu ukabila, ubaguzi na makundi aliyoyaeeza ili Kamati Kuu ichukue hatua zinazostahili. Mzee Halimoja akaja kueleza madai yake kuwa Mwenyekiti ana makundi. Ndipo Kamati Kuu ikampata ataje ni wakina nani katika makundi hayo, akashindwa kutaja hata jina moja. Akaambiwa ataje basi majina ya hao watu 14 alioambiwa kuwa watafukuzzwa kwa kumuunga mkono chacha akashindwa vile vile. Badala yake akamuomba Mzee Shilembi na Chacha wange ambao walikuwa wajumbe wa kikao wamsaidie kuifafanua barua yake. Kamati kuu ikaona kwamba kwa kuandika barua na kuisambaza ikiwemo kwenye vyombo vya habari juu ya madai ambayo hakuwa na uhakika nayo, na kukiuka itifaki na maadili Sekretariati ya chama ikaagizwa ichukue hatua za kinidhamu kwa kuwa ndio ambayo ilimchukua kama mtumishi. Dr Slaa alichukua uamuzi wa kusitisha utumishi wake kwa kuwa tayari alishakuwa na malalamiko mengine. Sasa huyu Rostam Aziz hakumrudisha CCM aliamua ambakize CHADEMA aendelee kusumbua kwa ndani kwa kuwa bado ni mwanachama ingawa si mjumbe wa Kikao chochote. Katika Kikao hicho cha kamati kuu Mzee Halimoja aliingia katika kikao cha Kamati Kuu na Tape recorder. Hiyo ilikuwa ni mwaka jana. Mwaka huu Mzee Halimoja amekuwa msatari wa mbele pamoja na Ballile kuandaa nyaraka zote za Chacha na pia amekuwa mstari wa Mbele kuandika makala za Kumsahmbulia Mbowe na CHADEMA kupitia Mtanzania akijtambulisha kuwa ni mwanachama. Pia aliandika waraka kwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Dodoma ya Juni 28 kuwataka wamchukulie hatua Dr Slaa, wapuuze taarifa ya Kamati ya Wazee na Wazingatie taarifa ya Kamati ya Mziray. Huyu ndiye daraja la kuvujisha Siri za CHADEMA kwenda kwa Kaborou. Ingawaje Chacha Wangwe amekiri Mwenyewe kwenye Vyombo vya Habari kuwa alivuka bahari alikwenda nyumbani kwa Kaburu Kigamboni kukutana naye na akahalalisha kitendo hicho, lakini mara kwa mara nyaraka za CHADEMA amekuwa akimpa Mzee huyu nyaraka za siri za chama aende nazo kwa Kaborou kwa ajili ya kutoa ushauri. Kaborou amekuwa muhimu kwa Chacha kwa kuwa anawafahamu vilivyo wajumbe ambao yeye alikuwa akiwatumia katika mikakati yake ya kuhujumu CHADEMA wakati akiwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.

PM
 
Mama
tuachane na hiyo habari tuongee kwa uwazi zaidi

Mama mie nafikiri tuhuma zidi ya chacha kutoka chadema zinajitosha kabisa kumufuta jamaa uanachama wewe unaona je? ktk hilo??

Na kwanini unadhani chadema wanasita kumfukuza uanachama wakati jamaa baada ya kusimamishwa uongozi na kuonywa na uongozi bado anaendelea na mikakati ileile ya kukiharibu chama??

mimi hilo la kumfuta uanachama sioni kitu kabisaaaaa to be honest. Lakini kwa kufikiri nadhani its not the right time, they should have known better before! je walimpa uanachama kwa hiyo character yake iliyomwezesha kupata ubunge na kuwaangusha sisiemu? katika kumwangusha sisiemu walimshangilia pia?

Nilikuwa sijui kama chadema wanasita kumfukuza uanachama, hapa ndio unanihabarisha. Je kuna taratibu zozote zinatakiwa kufuatwa ili kumfukuza chama au wanaweza kukurupuka tu na kumfukuza? Je ikitokea chacha kuomba msamaha na kukiri makosa anastahili kusamehewa?
 
mimi hilo la kumfuta uanachama sioni kitu kabisaaaaa to be honest. Lakini kwa kufikiri nadhani its not the right time, they should have known better before! je walimpa uanachama kwa hiyo character yake iliyomwezesha kupata ubunge na kuwaangusha sisiemu? katika kumwangusha sisiemu walimshangilia pia?

Nilikuwa sijui kama chadema wanasita kumfukuza chama, hapa ndio unanihabarisha. Je kuna taratibu zozote zinatakiwa kufuatwa ili kumfukuza chama au wanaweza kukurupuka tu na kumfukuza? Je ikitokea chacha kuomba msamaha na kukiri makosa anastahili kusamehewa?

kweli ukurupukaji sio mzuri
Nadhani ni halimashauri moja tu kama sikosei chadema ndio wanaiongoza nayo ni hiyo ya Tarime ya chacha na nafikiri chadema wanafurahia kitu hiyo.

Mama
kinachonishangaza ni uongozi wa chadema kubishana na chacha kama vile wanabishana na ccm yani mbowe ,lisu anakwenda kwenye vyombo vya habari anasema hivi chacha naye anakwenda anasema vile.

Kumbuka chacha ni mwanachama wao badala ya kubishana na kupakana matope waitane kwenye vikao na wawekane sawa ama muovu atakeyezidi kuchukuliwa hatua za kichama.

Yanayosemwa kuhusu chacha ni makubwa mno kwa uhai wa chama na hata hivyo jamaa bado anaendelea na mikakati ile ile ya kukutana na akina kabouru na Azizi yakuhakikisha chama kinapotea,wewe unafikiri hatua mhimu ni ipi?
 
Wakimfukuza uanachama atapoteza ubunge na hiyo itaamanisha kuwa ruzuku ya CHADEMA inapungua.they just cant afford that!
 
Kwa wote wale waliokurupuka kuishitumu CHADEMA na uongozi wake wakati habari za kusimamishwa Wangwe zilivoibuka nadhani ni wakati wa kuchukua a "deep breath," kama hizi ripoti za Paparazi Muwazi ni za kweli. Mafisadi hawatapumzika mpaka waiteke Tanzania nzima jamani. That is the truth. Si mumemwona Rostam kanisani jana? What the hell was he doing there?
 
kweli ukurupukaji sio mzuri
Nadhani ni halimashauri moja tu kama sikosei chadema ndio wanaiongoza nayo ni hiyo ya Tarime ya chacha na nafikiri chadema wanafurahia kitu hiyo.

Mama
kinachonishangaza ni uongozi wa chadema kubishana na chacha kama vile wanabishana na ccm yani mbowe ,lisu anakwenda kwenye vyombo vya habari anasema hivi chacha naye anakwenda anasema vile.

Kumbuka chacha ni mwanachama wao badala ya kubishana na kupakana matope waitane kwenye vikao na wawekane sawa ama muovu atakeyezidi kuchukuliwa hatua za kichama.

Yanayosemwa kuhusu chacha ni makubwa mno kwa uhai wa chama na hata hivyo jamaa bado anaendelea na mikakati ile ile ya kukutana na akina kabouru na Azizi yakuhakikisha chama kinapotea,wewe unafikiri hatua mhimu ni ipi?

wewe wala usishangae ya chadema na wangwe,hayo madogo tu na yataisha soon, wanagombana mke na mume au wazazi na mtoto ije kuwa chadema na wangwe. Watamalizana ndani ya familia yao ya chadema. Cha muhimu wewe shangaa ya ufisadi na sisiemu na ujadili suluhisho, je unafikiri ufisadi utaisha vipi tanzania?
 
haya mama
Mimi nafikiri Ufisadi utaisha tu mara baada ya kuuingia Rais kwa tiketi ya ugombea binafsi.Maana saizi kulazimmisha fisadi apelekwe mahakamani ni sawa na tumbili akahukumu kesi ya ngedele .

Na haya mavyama yote ni mafisadi tu ni sawa na mtanzania kuna sehemu amesema kuku yuleyule lakini kapakwa rangi tofauti.
wewe wasema je?
 
hata huyo mgombea binafsi atawezaje kuondoa ufisadi. Kumbuka kuwa ufisadi haufanywi na rais peke yake, bali watendaji wake haswaaaa ambao wengine si wabunge wala wanachama wa chama chochote.
 
Paparazi Muwazi,

Kwanza napenda kutanguliza shukrani zangu kwa uchambuzi yakinifu , kusema ukweli mambo yanayoendelea Chadema yanahuzunisha lakini nahisi haya yote yatakifanya chama kiwe strong siku za usoni. Nilikuwa naomba unielezee Rostam alizungumza nini haswa Kinondoni KKKT , jee alialikwa kama nani ? na jee ni tamko gani limetolewa na KKKT so far ?

Ni hayo tuu...
 
kweli ukurupukaji sio mzuri
Nadhani ni halimashauri moja tu kama sikosei chadema ndio wanaiongoza nayo ni hiyo ya Tarime ya chacha na nafikiri chadema wanafurahia kitu hiyo.

Mama
kinachonishangaza ni uongozi wa chadema kubishana na chacha kama vile wanabishana na ccm yani mbowe ,lisu anakwenda kwenye vyombo vya habari anasema hivi chacha naye anakwenda anasema vile.

Kumbuka chacha ni mwanachama wao badala ya kubishana na kupakana matope waitane kwenye vikao na wawekane sawa ama muovu atakeyezidi kuchukuliwa hatua za kichama.

Yanayosemwa kuhusu chacha ni makubwa mno kwa uhai wa chama na hata hivyo jamaa bado anaendelea na mikakati ile ile ya kukutana na akina kabouru na Azizi yakuhakikisha chama kinapotea,wewe unafikiri hatua mhimu ni ipi?

Chacha aliashaitwa kwenye vikao vingi tu vya wazee, na hicho cha kamati kuu. Lakini ukweli ni kwamba yeye lengo lake si hayo mambo yaishie kwenye vikao vya chama. Wakati anasimamishwa CHADEMA inalekea haikuwa na dhamira ya kuanika kwa nini haswa zimepigwa kura ya kutokuwa na imani naye. Lakini tayari Ballile alikuwa ameshamwaga sumu kali kuhusu ukabila na ruzuku kupitia Mtanzania. Ilibidi Mbowe na Tundu Lissu waeleze ukweli, waanike baadhi ya mambo. Binafsi nimepata wasaa wa kusikiliza recording aliyofanya mzee Halimoja kuhusu Kamati Kuu yao.

Jasusi

Niliposema kwa mara ya kwanza hapa nini kitatokea kuhusu Chacha watu waliuita udaku mtupu. Na haikukaa sana ikapelewa kwenye udaku. Halafu nikaandika ile habari nyingine ya CHADEMA kugawanyika makundi matatu. Nayo ikapelekwa katika udaku. Sasa kilichokea baadaye mpaka yakawa 'makundi' mawili badala ya matatu ni kwamba Ndesamburo naye alikuwa na tatizo na chama hicho, alikikopesha chama fedha wakati wa kampeni takribani milioni 100 lakini katika kudai akaleta na madeni ya fedha alizowasaidia wagombea mbalimbali wa chama hicho katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Arusha. Baraza Kuu la Chama likakataa kulipa madeni yao kwa kuwa sio fedha ambazo ziliruhusiwa kwenye kikao cha mwaka 2005. Mzee Ndesa akasusa mambo yote ya chama kwa kuona amedharaulika. Akaanza kujenga genge lake baada ya watu kupandikiza pia hoja kwamba Grace Kiwelu anataka kumng'oa Moshi Mjini akisaidiwa na Dr Slaa. Hapo ndipo lilipotokea tishio la kuwepo kwa kundi la Tatu na niliandika hapa pia. Rostam Aziz baada ya kupewa habari hizo akamtuma Chacha Wangwe akazungumze naye ili awe kwenye kundi lake. Na baadaye akaenda pia Mziray. Lakini Mzee huyu kama alivyomfanyia umafia Lowassa katika sakata la Manji na Mengi akachukua tu habari zote na kwenda kuzimwaga kwa Dr Slaa na baadaye kwa Mbowe. Dr Slaa akaachana na suala la kuwa na kundi baada ya kubaini kwamba kumbe ilikuwa atumike bila kujijua kuihujumu CHADEMA na kwa kadiri ya Chacha Wangwe Mzee Ndesa aliiliza Kamati ya Wazee kuwa yeye Chacha alimfuata. Kwa hiyo Mzee Ndesa sasa yuko upande wa CHADEMA, na kutokana na hali hii Chacha ameweka bayana kuwa atalipa kisasi kwa mzee Ndesa. Katika mashambulizi ya Majira, Mtanzania na Rai imepangwa kwamba baada ya Mbowe, Dr Slaa, Mnyika na Tundu Lissu baadaye atashambuliwa Mzee Ndesa. Katika mkakati huo wameacha makusudi kumshambulia Zitto ili kujenga uhalali wa mkakati wao wasionekane wanamshambulia kila mtu. Zitto bado hajatoa msimamo wake hadharani kwa nguvu zote kupinga mambo ya Wangwe, hata hivyo wamekubaliana kuwa kama Zitto atajiotokeza na kumshambulia Wangwe basi Chacha atamshambulia Zitto pia kama ambavyo aliwashambulia Selasini wa NCCR na Hamad wa CUF walipojitokeza na kumshambulia wazi wazi. Ndio maana nasema kwamba mengi yatajitokeza kwa kuwa hali ndani ya CHADEMA inaonyesha kuwa Zitto ni lazima atachukua msimamo wa kumshambulia Chacha Wangwe

PM
 
hata huyo mgombea binafsi atawezaje kuondoa ufisadi. Kumbuka kuwa ufisadi haufanywi na rais peke yake, bali watendaji wake haswaaaa ambao wengine si wabunge wala wanachama wa chama chochote.

Mimi sijasema Rais anafanya ufisadi ila nasema Rais kutoka ktk vyama ndio utasikia kuna maamuzi ya kulinda maslahi ya chama.

Rais binafsi wala usingesikia kelele za kurudishiwa ASP na TANU, wala usingesikia muafaka wa miezi 14 unayokula pesa za wananchi wakati pale mwananyamara hata grovu za wakunga hawana.

Hii system ya vyama mimi naona ndio ufisadi wenyewe
 
Hii stori yako inanikumbusha stori moja ya kwamba
mama mmoja mjamzito alikwenda kwa mganga wa kienyeji akiwa mjamzito akataka kujua kichanga kilicho tumboni ni kisichana ama kivulana

sasa basi baada ya yule jamaa kuzungusha vimbuyu vyake alimwambia hivi yulee mama
Hakika hiki kichanga kama si kuvulana basi ni kisischana
 
Kama ni flip floppers...Basi humu ndani ni nambari wani!
Wale waliokuwa wakimpigia debe Wangwe na kuleta UKABILA sasa eti na wao wanamwona ni Mbaya na ana jazba!
Hii kali.
 
ukweli utasimama daima, na honest people huwa dynamic kufuata ukweli.
 
Jmushi
kama una mwanao anasoma sekondari kule mkoa jirani ,basi jirani yako ana mtoto anayeitwa Juma basi huyu juma alipewa karo na mzazi wake yeye hiyo fee akainunua bangi na akarudushwa nyumbani.

Siku ya siku ilipofika mwanao kwenda shule ukamkabidhi karo na kumwambia maneno haya na "nakupa fee hii na wewe ukanunue bangi na urudishwe kama alivyofanya Juma"

usipoelewa maneno haya basi
 
Mimi sijasema Rais anafanya ufisadi ila nasema Rais kutoka ktk vyama ndio utasikia kuna maamuzi ya kulinda maslahi ya chama.

Rais binafsi wala usingesikia kelele za kurudishiwa ASP na TANU, wala usingesikia muafaka wa miezi 14 unayokula pesa za wananchi wakati pale mwananyamara hata grovu za wakunga hawana.

Hii system ya vyama mimi naona ndio ufisadi wenyewe

Mie nimetaja rais baada ya mwenzangu kusema kuwa ufisadi utaisha pale tutakapokuwa na rais ambaye ni mgombea binafsi.
 
ukweli utasimama daima, na honest people huwa dynamic kufuata ukweli.

Uzuri tumepewa macho ya kuona ,masikio ya kusikia na akili ya kutambua mema na mabaya.
 
Chacha aliashaitwa kwenye vikao vingi tu vya wazee, na hicho cha kamati kuu. Lakini ukweli ni kwamba yeye lengo lake si hayo mambo yaishie kwenye vikao vya chama. Wakati anasimamishwa CHADEMA inalekea haikuwa na dhamira ya kuanika kwa nini haswa zimepigwa kura ya kutokuwa na imani naye. Lakini tayari Ballile alikuwa ameshamwaga sumu kali kuhusu ukabila na ruzuku kupitia Mtanzania. Ilibidi Mbowe na Tundu Lissu waeleze ukweli, waanike baadhi ya mambo. Binafsi nimepata wasaa wa kusikiliza recording aliyofanya mzee Halimoja kuhusu Kamati Kuu yao.

Jasusi

Niliposema kwa mara ya kwanza hapa nini kitatokea kuhusu Chacha watu waliuita udaku mtupu. Na haikukaa sana ikapelewa kwenye udaku. Halafu nikaandika ile habari nyingine ya CHADEMA kugawanyika makundi matatu. Nayo ikapelekwa katika udaku. Sasa kilichokea baadaye mpaka yakawa 'makundi' mawili badala ya matatu ni kwamba Ndesamburo naye alikuwa na tatizo na chama hicho, alikikopesha chama fedha wakati wa kampeni takribani milioni 100 lakini katika kudai akaleta na madeni ya fedha alizowasaidia wagombea mbalimbali wa chama hicho katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Arusha. Baraza Kuu la Chama likakataa kulipa madeni yao kwa kuwa sio fedha ambazo ziliruhusiwa kwenye kikao cha mwaka 2005. Mzee Ndesa akasusa mambo yote ya chama kwa kuona amedharaulika. Akaanza kujenga genge lake baada ya watu kupandikiza pia hoja kwamba Grace Kiwelu anataka kumng'oa Moshi Mjini akisaidiwa na Dr Slaa. Hapo ndipo lilipotokea tishio la kuwepo kwa kundi la Tatu na niliandika hapa pia. Rostam Aziz baada ya kupewa habari hizo akamtuma Chacha Wangwe akazungumze naye ili awe kwenye kundi lake. Na baadaye akaenda pia Mziray. Lakini Mzee huyu kama alivyomfanyia umafia Lowassa katika sakata la Manji na Mengi akachukua tu habari zote na kwenda kuzimwaga kwa Dr Slaa na baadaye kwa Mbowe. Dr Slaa akaachana na suala la kuwa na kundi baada ya kubaini kwamba kumbe ilikuwa atumike bila kujijua kuihujumu CHADEMA na kwa kadiri ya Chacha Wangwe Mzee Ndesa aliiliza Kamati ya Wazee kuwa yeye Chacha alimfuata. Kwa hiyo Mzee Ndesa sasa yuko upande wa CHADEMA, na kutokana na hali hii Chacha ameweka bayana kuwa atalipa kisasi kwa mzee Ndesa. Katika mashambulizi ya Majira, Mtanzania na Rai imepangwa kwamba baada ya Mbowe, Dr Slaa, Mnyika na Tundu Lissu baadaye atashambuliwa Mzee Ndesa. Katika mkakati huo wameacha makusudi kumshambulia Zitto ili kujenga uhalali wa mkakati wao wasionekane wanamshambulia kila mtu. Zitto bado hajatoa msimamo wake hadharani kwa nguvu zote kupinga mambo ya Wangwe, hata hivyo wamekubaliana kuwa kama Zitto atajiotokeza na kumshambulia Wangwe basi Chacha atamshambulia Zitto pia kama ambavyo aliwashambulia Selasini wa NCCR na Hamad wa CUF walipojitokeza na kumshambulia wazi wazi. Ndio maana nasema kwamba mengi yatajitokeza kwa kuwa hali ndani ya CHADEMA inaonyesha kuwa Zitto ni lazima atachukua msimamo wa kumshambulia Chacha Wangwe

PM

Zitto amsuta Wangwe

na Salehe Mohamed

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amesema uamuzi wa kumsimamisha uongozi Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Chacha Wangwe, ni mzito na mgumu, lakini ulikuwa lazima ufanyike ili kukinusuru chama kilichokuwa kinaelekea kusambaratika.

Alisema CHADEMA iliogopa yasije yakawafika yaliyowafika ndugu zao wa NCCR-Mageuzi ambao walisambaratika kutokana na baadhi ya viongozi kutumiwa kukivuruga chama hicho kilichokuwa na nguvu zaidi miaka kumi iliyopita.

Kauli hiyo aliitoa juzi jioni mkoani hapa, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara ambao ulikuwa na lengo la kuwapongeza wanachama wa CHADEMA kwa kufanikiwa kunyakua viti vitano vya Serikali ya Mtaa wa Msikiti.

Alisema kauli ya Chacha na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kwamba kuna mgogoro si ya kweli, kwani hali ni shwari ila ni mageuzi ya kawaida katika vyama vya siasa, hasa inapoonekana kuna watu wanakwenda kinyume cha maadili pamoja na madaraka waliyonayo.

Alisema CCM mwaka 1967 ilikuwa ikienda mrama, na walipokaa na kuchunguza, ilionekana kuna baadhi ya wanachama walikuwa wakienda kinyume, hivyo wakaamua kuwaengua.

Zitto alisema mwaka 1984, Zanzibar ilikuwa imechafuka sana, hivyo CCM ikalazimika kumsimamisha Aboud Jumbe na wenzake na chama kikaendelea vizuri.

“Jamani nyinyi ni mashahidi, NCCR-Mageuzi ilifia hapa mwaka 1995, hii yote ilitokana na kutowaengua viongozi waliokuwa wakikigawa chama, sisi tumewahi kuwadhibiti watu hao,” alisema Zitto huku akishangiliwa na watu waliofurika katika mkutano huo.

Alisema hivi sasa kuna watu wanatumiwa kuihujumu CHADEMA baada ya kugundua kuwa ina watu makini wanaojua kujenga hoja na zikakubalika kwa wananchi.

Zitto alisema watu hao walianza kuibomoa CUF kwa madai kuwa ni chama cha kidini, na hivi sasa wamehamia kwa CHADEMA, na wameanzisha sera ya kuwa chama hicho ni cha kikabila (Wachaga).

Alibainisha wazi kuwa dhana ya ubaguzi ni mbaya zaidi na ilishakemewa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Nyerere kwani baada ya kuwabagua Wachaga watahamia kwa Wahaya, Wasukuma, Wasambaa na makabila mengineyo.

“Mwalimu Nyerere alituambia dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, kamwe ukishaanza huwezi kuiacha, leo utasema simtaki Mchaga, kesho Msukuma na kadhalika,” alisema Zitto.

Alisema ubaguzi huo ndio ulioifanya Tanzania kukosa mtu makini na mwenye uzoefu zaidi kwenye Umoja wa Nchi za Afrika (AU), baada ya CCM kumuengua Dk. Salim Ahmed Salim kwa madai ya kuwa ni Mwarabu.

Alisema CHADEMA wameshazijua mbinu chafu zinazotumiwa na watu wenye lengo la kukivuruga, na wapo makini kusafisha wote wanaotumiwa kukisambaratisha ili waweze kutekeleza matendo yao ya kifisadi ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na watu wengi zaidi.

Alisema nchi hivi sasa imeingia katika hali ngumu, hasa kwa kila mtu anayeshughulikiwa anakimbilia kwenye ukabila, hivyo ni vema wananchi wakaacha kudanganyika kirahisi.

Naye Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, John Mnyika, alisema hoja kubwa inayopaswa ishikiliwe na wananchi hivi sasa mbali na kupambana na ufisadi ni kudai mabadiliko ya katiba.

Alisema mabadiliko ya katiba yataweza kutoa mwanya mpana zaidi kwa vyama kuelekea katika chaguzi zilizo huru na haki kuliko ilivyo hivi sasa ambapo CCM wameonekana kunufaika zaidi na katiba iliyopo.

Katibu Mwenezi wa CHADEMA, Erasto Tumbo, alisema nchi itakombolewa na wanyonge kwani walioshiba hata siku moja hawawezi kumkumbuka mwenye njaa, hivyo ni vema wananchi wakaamka na kudai haki zao.

Alisema ni aibu kwa Manispaa ya Tanga kuwa katika hali mbaya namna hiyo ili hali ndiyo iliyokuwa manispaa ya kwanza Tanzania, lakini kadiri siku zinavyosonga mbele, ndivyo inavyodidimia kimaendeleo
.

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/7/habari2.php
 
hii baada ya kuandika si ndio nikampa mfano wa mama mjamzito na mpiga vibuyu
 
Back
Top Bottom