asante kwa maelezo yako. Una uhakika gani kama habari hii ni ya kupikwa ilihali hauko nyumbani Tz? je ukigeukiwa na kuambiwa kuwa habari uliyotoa wewe ndio ulipika?
I dont know ila kama maelezo ya PM ni kweli, basi Chacha ni mtu hatari sana, hafai kuwa kiongozi!
Hebu nipatie hiyo habari ambayo si ya kupikwa!
Mimi nimeshakubali mkuu
Lakini kwa vitendo vya CHACHA kuendelea kua mwanachama na mbunge wenu ni hatari sana ,HUyu anastahili kutimuliwa uanachama na kuchukuliwa hatua za kisheria
Mama
tuachane na hiyo habari tuongee kwa uwazi zaidi
Mama mie nafikiri tuhuma zidi ya chacha kutoka chadema zinajitosha kabisa kumufuta jamaa uanachama wewe unaona je? ktk hilo??
Na kwanini unadhani chadema wanasita kumfukuza uanachama wakati jamaa baada ya kusimamishwa uongozi na kuonywa na uongozi bado anaendelea na mikakati ileile ya kukiharibu chama??
mimi hilo la kumfuta uanachama sioni kitu kabisaaaaa to be honest. Lakini kwa kufikiri nadhani its not the right time, they should have known better before! je walimpa uanachama kwa hiyo character yake iliyomwezesha kupata ubunge na kuwaangusha sisiemu? katika kumwangusha sisiemu walimshangilia pia?
Nilikuwa sijui kama chadema wanasita kumfukuza chama, hapa ndio unanihabarisha. Je kuna taratibu zozote zinatakiwa kufuatwa ili kumfukuza chama au wanaweza kukurupuka tu na kumfukuza? Je ikitokea chacha kuomba msamaha na kukiri makosa anastahili kusamehewa?
kweli ukurupukaji sio mzuri
Nadhani ni halimashauri moja tu kama sikosei chadema ndio wanaiongoza nayo ni hiyo ya Tarime ya chacha na nafikiri chadema wanafurahia kitu hiyo.
Mama
kinachonishangaza ni uongozi wa chadema kubishana na chacha kama vile wanabishana na ccm yani mbowe ,lisu anakwenda kwenye vyombo vya habari anasema hivi chacha naye anakwenda anasema vile.
Kumbuka chacha ni mwanachama wao badala ya kubishana na kupakana matope waitane kwenye vikao na wawekane sawa ama muovu atakeyezidi kuchukuliwa hatua za kichama.
Yanayosemwa kuhusu chacha ni makubwa mno kwa uhai wa chama na hata hivyo jamaa bado anaendelea na mikakati ile ile ya kukutana na akina kabouru na Azizi yakuhakikisha chama kinapotea,wewe unafikiri hatua mhimu ni ipi?
wewe wala usishangae ya chadema na wangwe,hayo madogo tu na yataisha soon, wanagombana mke na mume au wazazi na mtoto ije kuwa chadema na wangwe. Watamalizana ndani ya familia yao ya chadema. Cha muhimu wewe shangaa ya ufisadi na sisiemu na ujadili suluhisho, je unafikiri ufisadi utaisha vipi tanzania?
haya mama
Mimi nafikiri Ufisadi utaisha tu mara baada ya kuuingia Rais kwa tiketi ya ugombea binafsi.Maana saizi kulazimmisha fisadi apelekwe mahakamani ni sawa na tumbili akahukumu kesi ya ngedele .
Na haya mavyama yote ni mafisadi tu ni sawa na mtanzania kuna sehemu amesema kuku yuleyule lakini kapakwa rangi tofauti.
wewe wasema je?
kweli ukurupukaji sio mzuri
Nadhani ni halimashauri moja tu kama sikosei chadema ndio wanaiongoza nayo ni hiyo ya Tarime ya chacha na nafikiri chadema wanafurahia kitu hiyo.
Mama
kinachonishangaza ni uongozi wa chadema kubishana na chacha kama vile wanabishana na ccm yani mbowe ,lisu anakwenda kwenye vyombo vya habari anasema hivi chacha naye anakwenda anasema vile.
Kumbuka chacha ni mwanachama wao badala ya kubishana na kupakana matope waitane kwenye vikao na wawekane sawa ama muovu atakeyezidi kuchukuliwa hatua za kichama.
Yanayosemwa kuhusu chacha ni makubwa mno kwa uhai wa chama na hata hivyo jamaa bado anaendelea na mikakati ile ile ya kukutana na akina kabouru na Azizi yakuhakikisha chama kinapotea,wewe unafikiri hatua mhimu ni ipi?
hata huyo mgombea binafsi atawezaje kuondoa ufisadi. Kumbuka kuwa ufisadi haufanywi na rais peke yake, bali watendaji wake haswaaaa ambao wengine si wabunge wala wanachama wa chama chochote.
Chacha aliashaitwa kwenye vikao vingi tu vya wazee, na hicho cha kamati kuu. Lakini ukweli ni kwamba yeye lengo lake si hayo mambo yaishie kwenye vikao vya chama. Wakati anasimamishwa CHADEMA inalekea haikuwa na dhamira ya kuanika kwa nini haswa zimepigwa kura ya kutokuwa na imani naye. Lakini tayari Ballile alikuwa ameshamwaga sumu kali kuhusu ukabila na ruzuku kupitia Mtanzania. Ilibidi Mbowe na Tundu Lissu waeleze ukweli, waanike baadhi ya mambo. Binafsi nimepata wasaa wa kusikiliza recording aliyofanya mzee Halimoja kuhusu Kamati Kuu yao.
Jasusi
Niliposema kwa mara ya kwanza hapa nini kitatokea kuhusu Chacha watu waliuita udaku mtupu. Na haikukaa sana ikapelewa kwenye udaku. Halafu nikaandika ile habari nyingine ya CHADEMA kugawanyika makundi matatu. Nayo ikapelekwa katika udaku. Sasa kilichokea baadaye mpaka yakawa 'makundi' mawili badala ya matatu ni kwamba Ndesamburo naye alikuwa na tatizo na chama hicho, alikikopesha chama fedha wakati wa kampeni takribani milioni 100 lakini katika kudai akaleta na madeni ya fedha alizowasaidia wagombea mbalimbali wa chama hicho katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Arusha. Baraza Kuu la Chama likakataa kulipa madeni yao kwa kuwa sio fedha ambazo ziliruhusiwa kwenye kikao cha mwaka 2005. Mzee Ndesa akasusa mambo yote ya chama kwa kuona amedharaulika. Akaanza kujenga genge lake baada ya watu kupandikiza pia hoja kwamba Grace Kiwelu anataka kumng'oa Moshi Mjini akisaidiwa na Dr Slaa. Hapo ndipo lilipotokea tishio la kuwepo kwa kundi la Tatu na niliandika hapa pia. Rostam Aziz baada ya kupewa habari hizo akamtuma Chacha Wangwe akazungumze naye ili awe kwenye kundi lake. Na baadaye akaenda pia Mziray. Lakini Mzee huyu kama alivyomfanyia umafia Lowassa katika sakata la Manji na Mengi akachukua tu habari zote na kwenda kuzimwaga kwa Dr Slaa na baadaye kwa Mbowe. Dr Slaa akaachana na suala la kuwa na kundi baada ya kubaini kwamba kumbe ilikuwa atumike bila kujijua kuihujumu CHADEMA na kwa kadiri ya Chacha Wangwe Mzee Ndesa aliiliza Kamati ya Wazee kuwa yeye Chacha alimfuata. Kwa hiyo Mzee Ndesa sasa yuko upande wa CHADEMA, na kutokana na hali hii Chacha ameweka bayana kuwa atalipa kisasi kwa mzee Ndesa. Katika mashambulizi ya Majira, Mtanzania na Rai imepangwa kwamba baada ya Mbowe, Dr Slaa, Mnyika na Tundu Lissu baadaye atashambuliwa Mzee Ndesa. Katika mkakati huo wameacha makusudi kumshambulia Zitto ili kujenga uhalali wa mkakati wao wasionekane wanamshambulia kila mtu. Zitto bado hajatoa msimamo wake hadharani kwa nguvu zote kupinga mambo ya Wangwe, hata hivyo wamekubaliana kuwa kama Zitto atajiotokeza na kumshambulia Wangwe basi Chacha atamshambulia Zitto pia kama ambavyo aliwashambulia Selasini wa NCCR na Hamad wa CUF walipojitokeza na kumshambulia wazi wazi. Ndio maana nasema kwamba mengi yatajitokeza kwa kuwa hali ndani ya CHADEMA inaonyesha kuwa Zitto ni lazima atachukua msimamo wa kumshambulia Chacha Wangwe
PM
Kama ni flip floppers...Basi humu ndani ni nambari wani!
Wale waliokuwa wakimpigia debe Wangwe na kuleta UKABILA sasa eti na wao wanamwona ni Mbaya na ana jazba!
Hii kali.
Mimi sijasema Rais anafanya ufisadi ila nasema Rais kutoka ktk vyama ndio utasikia kuna maamuzi ya kulinda maslahi ya chama.
Rais binafsi wala usingesikia kelele za kurudishiwa ASP na TANU, wala usingesikia muafaka wa miezi 14 unayokula pesa za wananchi wakati pale mwananyamara hata grovu za wakunga hawana.
Hii system ya vyama mimi naona ndio ufisadi wenyewe
ukweli utasimama daima, na honest people huwa dynamic kufuata ukweli.
Chacha aliashaitwa kwenye vikao vingi tu vya wazee, na hicho cha kamati kuu. Lakini ukweli ni kwamba yeye lengo lake si hayo mambo yaishie kwenye vikao vya chama. Wakati anasimamishwa CHADEMA inalekea haikuwa na dhamira ya kuanika kwa nini haswa zimepigwa kura ya kutokuwa na imani naye. Lakini tayari Ballile alikuwa ameshamwaga sumu kali kuhusu ukabila na ruzuku kupitia Mtanzania. Ilibidi Mbowe na Tundu Lissu waeleze ukweli, waanike baadhi ya mambo. Binafsi nimepata wasaa wa kusikiliza recording aliyofanya mzee Halimoja kuhusu Kamati Kuu yao.
Jasusi
Niliposema kwa mara ya kwanza hapa nini kitatokea kuhusu Chacha watu waliuita udaku mtupu. Na haikukaa sana ikapelewa kwenye udaku. Halafu nikaandika ile habari nyingine ya CHADEMA kugawanyika makundi matatu. Nayo ikapelekwa katika udaku. Sasa kilichokea baadaye mpaka yakawa 'makundi' mawili badala ya matatu ni kwamba Ndesamburo naye alikuwa na tatizo na chama hicho, alikikopesha chama fedha wakati wa kampeni takribani milioni 100 lakini katika kudai akaleta na madeni ya fedha alizowasaidia wagombea mbalimbali wa chama hicho katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Arusha. Baraza Kuu la Chama likakataa kulipa madeni yao kwa kuwa sio fedha ambazo ziliruhusiwa kwenye kikao cha mwaka 2005. Mzee Ndesa akasusa mambo yote ya chama kwa kuona amedharaulika. Akaanza kujenga genge lake baada ya watu kupandikiza pia hoja kwamba Grace Kiwelu anataka kumng'oa Moshi Mjini akisaidiwa na Dr Slaa. Hapo ndipo lilipotokea tishio la kuwepo kwa kundi la Tatu na niliandika hapa pia. Rostam Aziz baada ya kupewa habari hizo akamtuma Chacha Wangwe akazungumze naye ili awe kwenye kundi lake. Na baadaye akaenda pia Mziray. Lakini Mzee huyu kama alivyomfanyia umafia Lowassa katika sakata la Manji na Mengi akachukua tu habari zote na kwenda kuzimwaga kwa Dr Slaa na baadaye kwa Mbowe. Dr Slaa akaachana na suala la kuwa na kundi baada ya kubaini kwamba kumbe ilikuwa atumike bila kujijua kuihujumu CHADEMA na kwa kadiri ya Chacha Wangwe Mzee Ndesa aliiliza Kamati ya Wazee kuwa yeye Chacha alimfuata. Kwa hiyo Mzee Ndesa sasa yuko upande wa CHADEMA, na kutokana na hali hii Chacha ameweka bayana kuwa atalipa kisasi kwa mzee Ndesa. Katika mashambulizi ya Majira, Mtanzania na Rai imepangwa kwamba baada ya Mbowe, Dr Slaa, Mnyika na Tundu Lissu baadaye atashambuliwa Mzee Ndesa. Katika mkakati huo wameacha makusudi kumshambulia Zitto ili kujenga uhalali wa mkakati wao wasionekane wanamshambulia kila mtu. Zitto bado hajatoa msimamo wake hadharani kwa nguvu zote kupinga mambo ya Wangwe, hata hivyo wamekubaliana kuwa kama Zitto atajiotokeza na kumshambulia Wangwe basi Chacha atamshambulia Zitto pia kama ambavyo aliwashambulia Selasini wa NCCR na Hamad wa CUF walipojitokeza na kumshambulia wazi wazi. Ndio maana nasema kwamba mengi yatajitokeza kwa kuwa hali ndani ya CHADEMA inaonyesha kuwa Zitto ni lazima atachukua msimamo wa kumshambulia Chacha Wangwe
PM
Zitto amsuta Wangwe
na Salehe Mohamed
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amesema uamuzi wa kumsimamisha uongozi Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Chacha Wangwe, ni mzito na mgumu, lakini ulikuwa lazima ufanyike ili kukinusuru chama kilichokuwa kinaelekea kusambaratika.
Alisema CHADEMA iliogopa yasije yakawafika yaliyowafika ndugu zao wa NCCR-Mageuzi ambao walisambaratika kutokana na baadhi ya viongozi kutumiwa kukivuruga chama hicho kilichokuwa na nguvu zaidi miaka kumi iliyopita.
Kauli hiyo aliitoa juzi jioni mkoani hapa, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara ambao ulikuwa na lengo la kuwapongeza wanachama wa CHADEMA kwa kufanikiwa kunyakua viti vitano vya Serikali ya Mtaa wa Msikiti.
Alisema kauli ya Chacha na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kwamba kuna mgogoro si ya kweli, kwani hali ni shwari ila ni mageuzi ya kawaida katika vyama vya siasa, hasa inapoonekana kuna watu wanakwenda kinyume cha maadili pamoja na madaraka waliyonayo.
Alisema CCM mwaka 1967 ilikuwa ikienda mrama, na walipokaa na kuchunguza, ilionekana kuna baadhi ya wanachama walikuwa wakienda kinyume, hivyo wakaamua kuwaengua.
Zitto alisema mwaka 1984, Zanzibar ilikuwa imechafuka sana, hivyo CCM ikalazimika kumsimamisha Aboud Jumbe na wenzake na chama kikaendelea vizuri.
Jamani nyinyi ni mashahidi, NCCR-Mageuzi ilifia hapa mwaka 1995, hii yote ilitokana na kutowaengua viongozi waliokuwa wakikigawa chama, sisi tumewahi kuwadhibiti watu hao, alisema Zitto huku akishangiliwa na watu waliofurika katika mkutano huo.
Alisema hivi sasa kuna watu wanatumiwa kuihujumu CHADEMA baada ya kugundua kuwa ina watu makini wanaojua kujenga hoja na zikakubalika kwa wananchi.
Zitto alisema watu hao walianza kuibomoa CUF kwa madai kuwa ni chama cha kidini, na hivi sasa wamehamia kwa CHADEMA, na wameanzisha sera ya kuwa chama hicho ni cha kikabila (Wachaga).
Alibainisha wazi kuwa dhana ya ubaguzi ni mbaya zaidi na ilishakemewa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Nyerere kwani baada ya kuwabagua Wachaga watahamia kwa Wahaya, Wasukuma, Wasambaa na makabila mengineyo.
Mwalimu Nyerere alituambia dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, kamwe ukishaanza huwezi kuiacha, leo utasema simtaki Mchaga, kesho Msukuma na kadhalika, alisema Zitto.
Alisema ubaguzi huo ndio ulioifanya Tanzania kukosa mtu makini na mwenye uzoefu zaidi kwenye Umoja wa Nchi za Afrika (AU), baada ya CCM kumuengua Dk. Salim Ahmed Salim kwa madai ya kuwa ni Mwarabu.
Alisema CHADEMA wameshazijua mbinu chafu zinazotumiwa na watu wenye lengo la kukivuruga, na wapo makini kusafisha wote wanaotumiwa kukisambaratisha ili waweze kutekeleza matendo yao ya kifisadi ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na watu wengi zaidi.
Alisema nchi hivi sasa imeingia katika hali ngumu, hasa kwa kila mtu anayeshughulikiwa anakimbilia kwenye ukabila, hivyo ni vema wananchi wakaacha kudanganyika kirahisi.
Naye Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, John Mnyika, alisema hoja kubwa inayopaswa ishikiliwe na wananchi hivi sasa mbali na kupambana na ufisadi ni kudai mabadiliko ya katiba.
Alisema mabadiliko ya katiba yataweza kutoa mwanya mpana zaidi kwa vyama kuelekea katika chaguzi zilizo huru na haki kuliko ilivyo hivi sasa ambapo CCM wameonekana kunufaika zaidi na katiba iliyopo.
Katibu Mwenezi wa CHADEMA, Erasto Tumbo, alisema nchi itakombolewa na wanyonge kwani walioshiba hata siku moja hawawezi kumkumbuka mwenye njaa, hivyo ni vema wananchi wakaamka na kudai haki zao.
Alisema ni aibu kwa Manispaa ya Tanga kuwa katika hali mbaya namna hiyo ili hali ndiyo iliyokuwa manispaa ya kwanza Tanzania, lakini kadiri siku zinavyosonga mbele, ndivyo inavyodidimia kimaendeleo.
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/7/habari2.php