Rostam Aziz Kung'atuka!

Rostam Aziz Kung'atuka!

watu wengine wa ingunga tunawaelewa kwa kusema hivyo, umasikini na kutowahi kutendewa haki yao na wabunge waliopita imewafanya waone rostam ni mtu pekee anayewafaa wao.
ila kama kiongozi wa upinzani wilayani hapo, kwa kweli inasikitisha. hivi kwa miajili haya upinzani utafanikiwa kweli!
 
Hizo story zenu za ufisadi na nini sijui wananchi wa kawaida hata hawaelewi ni kitu gani! Wao mradi kawajengea bwawa moja la kunyweshea ng'ombe wao basi ni mbunge mzuri. Kama kawapa vijana wafanya biashara ndogo ndogo mtajiwa wa shs kama laki moja kila mmoja kwa vijana 100 (Total 10m) hizo wao wanaona ni pesa nyingi sana. Hawajui ameiba rasimali kiasi gani!

Hivi ni kweli Rostam kazaliwa Mwisi - Igunga?? Mbona anasemekana ni raia wa Irak aliyekuja nchini miaka ya karibuni?

Mhh hii mpya!
 
Mgombea binafsi inaweza ikaja kuwa sln.
Kwasababu kwa makusudi kabisa..ccm imewatega wananchi!
 
inajulikana wazi kwamba baadhi ya viongozi wa vyama katika ngazi za wilaya na hata mkoa humyenyekea yeyote ili mradi wapate vifedha kwa njaa zao. unakuta wananchi hawana lolote wanalofaidika nalo bali ni kwa viongozi hawa wachache.huyo mwandishi mbona kaficha jina, its all about spin doctors
 
Ndio maana nilishauri CHADEMA wasije waka-risk wabunge wao maarufu kugombea urahisi na kukosa vyote. 2010 bado ni ya CCM labda litokee kubwa lingine. Mabadiliko ndani ya CCM ndo yatakayoweza tu kubadilisha raisi wa 2011. Wake up people.
 
Na hapa unaongea kama mwana ccm au kama mwana chadema?
 
Tatizo ni kwamba wengi wa wabunge hawatimizi yale wanayopaswa kutimiza, kuna Mbunge mmoja wa jimbo nadhani Moshi mkopo wa Magari ya wabunge yeye alijitolea kununulia gari la kubeba wagonjwa! wengine wakichaguliwa wanabadilisha wanawake kama nguo sasa inapotokea mbunge kugawa mtaji wa M10 na kuchimba bwawa Moja, kusambaza maji hadi vijijini, umeme hadi vijijini unategemea wana Igunga wafanyeje zaidi ya kuona kuwa RA angalau anafaa kuliko wabunge wanaohamia Dar na kukimbia majimbo yao! Msiwashangae Igunga wana manufaa sana na RA kama ana hitilafu za kitaifa nadhani wana Igunga hawaguswi sana na hilo fika Igunga umseme vibaya RA uone utakavyoshambuliwa kama paka mwizi
 
Last edited:
Hawa watu wa Igunga kweli elimu ndogo inawaponza, hawa eliwi kwamba Jamaa anawarudishia kidogo kile alicho waibia.
 
Hii Ni Moja Ya Maigizo Mengi Anayofanya Huyu Fisadi Ra Kujaribu Kujionyesha Anapendeka Na Anahitajika. Huu Mchezo Umepangwa Kifundi.. Kwanza Akawanunua Hawa Viongozi Akawapa Maelekezo Ya Nini Cha Kufanya. Kujenga Democracy Sehemu Yenye Njaa Ni Ngumu Sana..
 
Tatizo ni kwamba wengi wa wabunge hawatimizi yale wanayopaswa kutimiza, kuna Mbunge mmoja wa jimbo nadhani Moshi mkopo wa Magari ya wabunge yeye alijitolea kununulia gari la kubeba wagonjwa! wengine wakichaguliwa wanabadilisha wanawake kama nguo sasa inapotokea mbunge kugawa mtaji wa M10 na kuchimba bwawa Moja, kusambaza maji hadi vijijini, umeme hadi vijijini unategemea wana Igunga wafanyeje zaidi ya kuona kuwa RA angalau anafaa kuliko wabunge wanaohamia Dar na kukimbia majimbo yao! Msiwashangae Igunga wana manufaa sana na RA kama ana hitilafu za kitaifa nadhani wana Igunga hawaguswi sana na hilo fika Igunga umseme vibaya RA uone utakavyoshambuliwa kama paka mwizi
HUYo mbunge ni mzee ndesamburo
 
Sijafika hukoIgunga na kujua alichofanya RA. Lakini from the gist of this story, nadhani RA anaweza kuwa alitumia sehemu ya fedha zake za ufisadi kumwaga mapesa jimboni huko. Unadhani wananchi hawa wa vijijini, ambao habari za ufisadi wanazisikia kijuujuu wanaweza kudhani mbunge wao ni mbaya kiasi hicho? Wananchoona wao ni ile misaada ambayoameimwaga na hayomenginme, kwa sababu wanayasikia kijuujuu, wanayaona kama uzushi tu
 
Back
Top Bottom