Hizo story zenu za ufisadi na nini sijui wananchi wa kawaida hata hawaelewi ni kitu gani! Wao mradi kawajengea bwawa moja la kunyweshea ng'ombe wao basi ni mbunge mzuri. Kama kawapa vijana wafanya biashara ndogo ndogo mtajiwa wa shs kama laki moja kila mmoja kwa vijana 100 (Total 10m) hizo wao wanaona ni pesa nyingi sana. Hawajui ameiba rasimali kiasi gani!
Hivi ni kweli Rostam kazaliwa Mwisi - Igunga?? Mbona anasemekana ni raia wa Irak aliyekuja nchini miaka ya karibuni?
Ndio maana nilishauri CHADEMA wasije waka-risk wabunge wao maarufu kugombea urahisi na kukosa vyote. 2010 bado ni ya CCM labda litokee kubwa lingine. Mabadiliko ndani ya CCM ndo yatakayoweza tu kubadilisha raisi wa 2011. Wake up people.
HUYo mbunge ni mzee ndesamburoTatizo ni kwamba wengi wa wabunge hawatimizi yale wanayopaswa kutimiza, kuna Mbunge mmoja wa jimbo nadhani Moshi mkopo wa Magari ya wabunge yeye alijitolea kununulia gari la kubeba wagonjwa! wengine wakichaguliwa wanabadilisha wanawake kama nguo sasa inapotokea mbunge kugawa mtaji wa M10 na kuchimba bwawa Moja, kusambaza maji hadi vijijini, umeme hadi vijijini unategemea wana Igunga wafanyeje zaidi ya kuona kuwa RA angalau anafaa kuliko wabunge wanaohamia Dar na kukimbia majimbo yao! Msiwashangae Igunga wana manufaa sana na RA kama ana hitilafu za kitaifa nadhani wana Igunga hawaguswi sana na hilo fika Igunga umseme vibaya RA uone utakavyoshambuliwa kama paka mwizi