Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mwakilishi wa Sekta Binafsi, Rostam Azizi, ametoa wito kwa wadau wa maendeleo ya uchumi kufanya mabadiliko makubwa katika sekta ya kifedha ili kuhakikisha wafanyabiashara wa Kitanzania wanapata mitaji ya kutosha kwa ajili ya kuwekeza na kukuza biashara zao.
Amesema mfumo wa sasa wa benki nchini umekuwa kikwazo kikubwa kwa wafanyabiashara wa ndani, kwani hauwapi nafasi ya kukua na kushindana katika soko la kimataifa.
Rostam amesisitiza umuhimu wa kuwepo sera na sheria zinazolenga kuwapendelea wafanyabiashara wa Kitanzania, badala ya mazingira ya sasa yanayowabana na kuwanyima fursa za upatikanaji wa fedha.