Rostam Aziz, ndiye tajiri namba moja Tanzania kwa sasa!!!

kenyatta mbona siajmuona
Hii list nadhani ni kwa mujibu wa 'audited reports' za wafanyabiashara ishara ya kuwa wengi wao hawatoi hesabu halisi, ukwepaji mkubwa wa uwajibikaji na ukwepaji kodi.
Kama mambo yangelikuwa kwa uwazi basi hata huyo Rostam huo utajiri wake ungelikuwa mara zaidi ya nne ya huu uliotajwa. Lakini pia kuonekana kwa majina ya Azam namba 38 nyuma ya Mengi ni ushahidi wa hili ninaloandika.
Yot neema ila nina uhakika wakitafuta pia masikini wa mwisho huenda tukakutikana wengi pia hapa tz.

 
LOWASA VP? maana tunaskia ameliibia sana taifa au za kwake nyingi zimefichwa ughaibuni hivyo hazijulikani?

ndugu hao n wale ambao mamb yao yapo waz kw kiwango fln,hao unaowataja ww hawajaanka,pengne n zaid ya hao unaowajua,na ambao 2mewaona kwenye list.....
 
Ni kwa muujiza wa Mwenyezi Mungu tu matajiri wataingia mbinguni!
 
Uhuru Kenyatta last year alikuwa WA 26 lakini hii simuoni kunani? [TABLE="class: asiaTable"]
[TR]
[TH]Net Worth[/TH]
[TD]$500 Million [/TD]
[TH]Source of Wealth [/TH]
[TD]land[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH]Age[/TH]
[TD]50[/TD]
[TH]Marital Status[/TH]
[TD]Married[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH]Country[/TH]
[TD]Kenya[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Inamana dangote kampita hadi abramovic? kwa hiyo pesa dangote alitakiwa kuwepo top 15 ya dunia.
 
samahani, utajiri wa rostam umetokana na nini vile?
 
Riz Moko wa Angola kawakilisha number 7. simshangai riz moko
 
huyu mzee wa azam hadi wamekosa picha yake? hii kali
 
Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz (49), ametajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania kwa sasa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Marekani la Forbes na kutoa taarifa yake juzi, Rostam amekamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni moja (Sh1.6 trilioni).

Mbunge huyo wa zamani wa Igunga, ameingia kwa mara ya kwanza katika orodha ya matajiri 50 wa Afrika ya jarida hilo, pamoja na wafanyabiashara wengine wa Tanzania, Reginald Mengi na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji ‘Mo’. Katika orodha hiyo pia yumo Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma.

Rostam, ambaye aliachana na siasa mwaka 2011, amempiku Bakhresa, ambaye mwaka jana Jarida la Ventures Africa la Nigeria lilimtaja kuwa ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania. Bakhressa katika kipindi hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620 milioni (Sh971 bilioni).

Katika orodha hiyo ya Ventures Africa, Bakhresa alifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali Mufuruki.

Mengi anashika nafasi ya pili kwa Tanzania na ya 34 Afrika akiwa na utajiri wa Dola 550 milioni (Sh861 bilioni).

Forbes linaonyesha kuwa Bakhresa amefungana na Mo katika nafasi ya tatu ya orodha ya matajiri wa Tanzania na ya 38 kwa Afrika, wote wakiwa na utajiri wa Dola 500 milioni (Sh783 bilioni).

Rostam, Mengi na Bakhresa hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo huku Mo akisema kwamba asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa jana alikuwa katika mapumziko ya Sikukuu ya Ashura.

Tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote, ambaye anajenga Kiwanda cha Saruji huko Mtwara ndiye anayeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya Afrika, akiwa na utajiri wa Dola20 bilioni (Sh31.7 trilioni), akifuatiwa na familia ya Johanny Rupert ya Afrika Kusini yenye utajiri wa Dola7 bilioni (Sh10.7 trilioni) na Nick Oppenheimer, pia wa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 6.6 bilioni (Sh10.3 trilioni).

chanzo: Mwananchi

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…