Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Mwanahalisi usiogope, huyo Rostam tumbo la kuhara linamkabili maana alianza kampeni ya kujisafisha na sasa matokeo yake yanamwelemea maana nguvu za wanaompinga ni kubwa kupita kiasi. Asipokuwa mjanja ataanguka mapema, wewe kazi uzi Kamanda wetu, sisi tuko nyuma yako. Kwa namna yeyote atakayojaribu kujitetea kwa nguvu atakuwa amekoleza moto na kuongeza mafuta anayoyagharamia mwenyewe. Na kwa jinsi nimjuavyo huyo mjinga kutumia pesa kuvuruga mambo si tatizo, lakini kwa sasa uwezo wa kugeuza mambo ni kama kuongelea kugeuza bahari juu chini, ni NGUMU.
 
Ndio nasema hilo haliwezekani Ni kazi ya serikali kutengeneza mazingira mwafaka kwa sekta binafsi na wafanyabiashara kufanya biashara zao na wakati huohuo kuhakikisha kwamba inaziba mianya yoyote, kwa njia ya sheria, kanuni, n.k., ya kuliingiza hasara taifa na kupoteza mapato halali kwa njia ya kodi. Inavyoonekana ni kama vile tulitaka Rostam asitumie mianya iliyokuwepo na ambayo ipo ya kumfanya apate faida haraka na kubwa, I bet hili haliwezekani kwa mfanyabiashara yeyote, simply because hiyo sio kazi yake!

CCM walipoamua kuwakumbatia wafanyabiashara waliamua pia kukumbatia utapeli na ujanjaujanja wa wafanyabiashara kama akina Rostam. Rostam anasema wazazi wake walianza biashara tangu 1852, sasa cha kujiuliza ni kwa nini yeye amejulikana kuanzia kipindi cha wakati wa Mwinyi na kushamirisha biashara zake kipindi cha kampeni za urais wa 2005? Ni kwamba huko nyuma hapakuwa na loop holes za kijinga kama zilivyo sasa.

Tuache kuwa simplistic because simplicity is the enemy of truth. Hatuwezi kuishinda vita ya ufisadi kwa kuwashambulia mawakala wa ufisadi; ifike mahala tuamue ama kuwashambulia wazalisha ufisadi CCM au kama, hatuwawezi, tukae kimya na tukubaliane kwamba hayo ndiyo maisha yetu!

Kitila.
Rostam Familia yake inajulikana miaka mingi kutomjua kwako RA hadi 2005 haina maana alikuwa hayupo.

Familia ya Rostam inatamba kwenye biashara toka awamu ya kwanza ya nchi yetu usitake kumtukana mzee Mwinyi kwa sababu zako.

Wakati wa Mwalimu Nyerere Familia ya kina Manji ilivuna pesa nyingi sana kupitia QUALITY GROUP ilikuwa ikitengeneza mabody ya mabus nchi nzima kama kampuni pekee, jee wewe ulikuwa unaijua familia ya Manji? ungemjua vipi wakati magazeti yalikuwa mawili tu.

Mwanamboka alikuwa Mwarabu aliyefanikiwa sana kibiashara kipindi cha Mwalimu Nyerere, kipindi hicho walitumia pembe za ndovu na nyara mbali mbali za nchi kujinufaisha. ukienda Tunduru utakutana na waburushi waliofanikiwa sana kipindi cha Nyerere.

Ni kama vile wewe ulivyokuwa huijui Chadema hadi ilipokuja na helikopta 2005 haina maana kuwa Chadema haikuwepo prior to 2005.

kipindi cha Nyerere Rostam asingeweza kugombea ubunge umri wake ulikuwa mdogo na alikuwa akisoma. si kila mwanafamilia anapenda siasa, kwenye familia yao katokea Rostam.

waasia walikuwepo wengi tu kwenye siasa kipindi cha Nyerere mfano Shamim Khan,Kassam n.k
wafanyabiashara wengi walikuwepo kipindi cha mwalimu Scandinavia,Abood bus service n.k
 
Hivi Rostam alizaliwa wapi na wazazi wake wako wapi?

Hakuna anaejua vitu vya ndani vya watu kama hivyo Tanzania.

Wakati ule umezuka mtafaruku wa uraia wa Rostam, mpaka uhamiaji wakaulizwa wakasema wataangalia, you would think the press would dig deeper and follow up. Lakini hakuna.

Sasa just imagine Mbunge wa Jamhuri hakuna anaejua anatoka wapi.

Website ya Bunge sehemu ya background, Rostam, kama Wabunge wengi, kaacha blank sehemu karibu zote.

Unagombea Ubunge halafu hakuna kiumbe kwenye press kinakuuliza we kwenu wapi.

Hamna anaejua kitu kuhusu mtu yeyote hapa.

Huyu Mtikila huyu, ambae kila siku yuko mahakamani kutangua masheria makubwa makubwa ya Katiba, hakuna anaejua kama kasoma sheria na kasomea wapi. Kuna kigazeti kiliwahi kiliandika ni mwanasheria. Lakini hakuna mwenye uhakika.

Hatuna press. Hakuna press hapa kwetu hapa. Tanzania.

Ingekuwepo tungejua au kungekuwa na inquiry kuhusu background ya Mbunge wa Jamhuri!
 
Hakuna anaejua vitu vya ndani vya watu kama hivyo Tanzania.

Wakati ule umezuka mtafaruku wa uraia wa Rostam, mpaka uhamiaji wakaulizwa wakasema wataangalia, you would think the press would dig deeper and follow up. Lakini hakuna.

Sasa just imagine Mbunge wa Jamhuri hakuna anaejua anatoka wapi.

Website ya Bunge sehemu ya background, Rostam, kama Wabunge wengi, kaacha blank sehemu karibu zote.

Unagombea Ubunge halafu hakuna kiumbe kwenye press kinakuuliza we kwenu wapi.

Hamna anaejua kitu kuhusu mtu yeyote hapa.

Huyu Mtikila huyu, ambae kila siku yuko mahakamani kutangua masheria makubwa makubwa ya Katiba, hakuna anaejua kama kasoma sheria na kasomea wapi. Kuna kigazeti kiliwahi kiliandika ni mwanasheria. Lakini hakuna mwenye uhakika.

Hatuna press. Hakuna press hapa kwetu hapa. Tanzania.

Ingekuwepo tungejua au kungekuwa na inquiry kuhusu background ya Mbunge wa Jamhuri
!

Sio press tu....hakuna mengi!! Tulichonancho ni ujinga wa hali ya juu na ufisadi uliokithiri.....hivi ndivyo vipo.....
 
Sio press tu....hakuna mengi!! Tulichonancho ni ujinga wa hali ya juu na ufisadi uliokithiri.....hivi ndivyo vipo.....

Press ndio inanisumbua zaidi kwa sababu kufundishana hii taalam haihitaji maendeleo kama ya Nuclear Technology au biomedical advancement. Ni kiasi cha kuangalia kusoma New York Times au kuangalia Watangazaji wa BBC tu unajifunza wengine wanavyofanya hii kazi. Hii taaluma haitakiwei kutushinda jamani.

Disclaimer of clarity:

Nyani Ngabu, I am not conceding, or hinting at agreeing whatsoever, to your underlying belief that our wretched state of poverty, disease, despair, death and disaster is due to inherent mental handicap.

If we are wantonly stupid it is because of nurture, not nature. Pursuant to the science of genetics.
 
VERY well put Kuhani
 
Samahani kwakuvamia hili jikwaa mimi sio mwanasiasa ila imenibidi niseme kidogo maana naona sasa ni KERO KUBWA,Napenda mzidi kutambua majukumu ya mlinziwetu,Baba mwenye Muji eeeh! maana Yupe na mali inapo potea mlinzi ndio anajibu kwa boss wake muajili yaani mwajili ni mwananchi.

Nawapa pongezi wotee mnao post kuhusu Rostam,ila ukweli utabaki palepale maana mimi sielewi kabisa yaani watu wanaacha kuongelea mambo yanayo husu taifa wizi unafanyika waziwazi na wezi wenu wanajulikana wezi wa EPA mnakaa eti Rostam kaiba Nadhani tunashida tena kubwa kama mambo ya EPA tumeamu kuya samehe nakuanza kumfuatilia huyu Muhindi MTZ nawashangaa Hii nyumba inamwenyewe bwana eeeh! kama Ropstam Mwizi hii nyumba inamlinzi na Baba mwenye nyumba Pia yupo.

Kwani ninani kati yetu ambaye ajui kuwa watu weupe ni wajanja eeh! naamini Rostam anafanya kwakutumia akili ndio maana utasikia Richmond yake,Mara Voda lakini anayo haki yakuwa navyo hivyo vitu maana si ni akili Yake ndio anaotumia kutafuta.

Mimi nadhani sisi tufatilie yetu tuachane na huyu Muhindi maana atatupotezea muda Ukweli hatuwezi kumfanya chochote tutaishia tu kumchafulia jina ila Watu wa Igunga wamemzimikia sana hawaambiwi wala hawasikii wanampenda mtu wao.

Hata kama ungekuwa wewe Hauwezi kukaa sehemu kijinga wakati opportunity yakupata mshiko ipo eti ukaacha kupata pesa eti kisa watu watachonga hiyo haisaidii mimi nadhani huyu jamaa aendelee tu na mabusiness yake kama NMyumba haina mlinzi Basi ijulikana kama tumempa jukumu la kulinda nyumba alafu tunamlipa itakuwa je mali ziibiwe sizitalipwa na huyo mlinzi wasiwasi nininini?

Mimi nasema tena kama KKKT wangetulia tu hiyo pesa wafanyie kazi ya Mungu,Maana Mungu anainua watu kwa njia mbalimbali kutegemeza kazi yake mimi nadhani hapo hakuna jipya ni huyo Rostam akae kimya tu kama Ben,
Maana inakuwa Kero sasa jamaa anakuwa kama DILI sasa tunasahau mpaka mambo ya muhimu.

hamna jipya.
 
Mchungaji ameshakwisha kisiasa 3m zimemponza! ukweli ni kuwa watanzania huhongwa fedha kidogo sana, sijui ni njaa au upumbavu tu!! nakumbuka hotuba ya Dr. Omary Juma alisema watz huhongwa fedha kidogo sana na kufanya maamuzi yenye hasara kubwa kwa taifa.

Sio ajabu trafiki kupokea hongo ya elfu moja kutaka kwa dereva wa daladala, na afisa uhamiaji kuhongwa elfu ishirini na kutoa work permit.

inasikitisha 5m zimelidhalilisha kanisa kubwa kama kkkt, fedha hizi nisawa na sadaka za misa moja tu ya kanisa moja la kkkt.

Huko vijijini ndo balaa watu wanahongwa glass ya gongo, kibaba cha chumvi, kipande cha sabuni, kilo ya nyama.
 
Press ndio inanisumbua zaidi kwa sababu kufundishana hii taalam haihitaji maendeleo kama ya Nuclear Technology au biomedical advancement. Ni kiasi cha kuangalia kusoma New York Times au kuangalia Watangazaji wa BBC tu unajifunza wengine wanavyofanya hii kazi. Hii taaluma haitakiwei kutushinda jamani.

Disclaimer of clarity:

Nyani Ngabu, I am not conceding, or hinting at agreeing whatsoever, to your underlying belief that our wretched state of poverty, disease, despair, death and disaster is due to inherent mental handicap.

If we are wantonly stupid it is because of nurture, not nature. Pursuant to the science of genetics.

Nianze kwa kusema kwamba haihitaji hata kuangalia BBC wala kusoma New York Times ili kujua namna au jinsi ya kuandika habari na kuripoti. Hao BBC na New York Times walijifunza toka kwa nani? Hapa kinachohitajika ni akili (maarifa) ya kawaida tu, ujasiri, na kufanya kazi kwa kutokupendelea. Upendeleo unaotakiwa ni wa ukweli tu.

Now back to your disclaimer. I have never said anywhere that black Africans have an "inherent mental handicap" and nor do I believe that to be the case. If I have, please show me and I will humbly apologize for affronting a whole community of people for something that has already been debunked many moons ago. Black Africans can go toe to toe with anybody of any race in any academic field. I think what led you to say that is my signature. But my signature doesn't refer to "inherent mental" or intellectual shortcomings as many of you think. If you want me to, I'd happy to expound on it at great length on what I mean by it.
 
Ukiondoa IPTL, Ndege na Rada ambazo bado hatujapata ushahidi wa kutosha, kila suala linalohusu Hujuma za kiuchumi Tanzania ambalo limezaa Ufisadi na Rushwa ya kuvunja na Shoka jina la Rostam lipo.

Kwenye mikingamo ya Uongozi na kukosekana uimara ndani ya Serikali au CCM, jina la Rostam linatawala.

Kwenye masuala ya jamii na matatizo mengine hata yale yaliyochukua uhai wa wanasiasa, jina lake lipo.

Iweje yeye awe common denominator, prime factor na hata SI unit ya kila ovu Tanzania na tuendelee kuwambiwa tusimtilie shaka?
 
Mbona hakuna mwenye ushahidi, au kende, za kumpeleka mahakamani ?
 
Mbona hakuna mwenye ushahidi, au kende, za kumpeleka mahakamani ?

Unamtetea? au ni kuleta kwako mizani?

Ukweli ni kuwa kama hata vyombo vya usalama na sheria vimenunuliwa na vinafanya kazi kwa matakwa yake, unatarajia ni vipi ushahidi na kende zitafanya kazi?

Kuna njia nyingi katika vita hii, na hii ya kutokumuonea haya na kumtaja kuwa ni mhimili wa maovu ni moja wapo, iko siku mhimili utazidiwa na kuanguka!
 
Bubu,
Ni kwanini Kikwete anayaruhusu haya?

Bubu,

Pamoja na U-Superstar wa Kikwete, udhaifu wake unatokana na madhambi yake aliyofanya ili kupata uraisi.

Sasa hivi Kikwete ni mpweke na mkiwa, wale wote ambao eti walikuwa marafiki zake, wanapeta na wanaendelea kujifanyia mambo wakijua wazi kuwa hana uwezo wa kuwachukulia hatua.

Uwoga wa Kikwete na kukwepa kusimika sime chini au kudindia uanaharamu ni dalili tosha kuwa yeye ni Raisi jina bali hana nguvu au mamlaka.

Ndiyo maana kabakia kuwa mtalii!
 
Unamtetea? au ni kuleta kwako mizani?

Ukweli ni kuwa kama hata vyombo vya usalama na sheria vimenunuliwa na vinafanya kazi kwa matakwa yake, unatarajia ni vipi ushahidi na kende zitafanya kazi?

Sijui na sitaraijii kama zitafanya au hazitafanya kazi mpaka tuone atavyokuwa treated na vyombo vya sheria siku atakapojitokeza mtu mwenye ushahidi, au kende, za kumfikisha huko.
 
Bubu,
Ni kwanini Kikwete anayaruhusu haya?

Kikwete kachukua mapesa mengi sana toka kwa RA, hasa wakati wa kampeni zake za kugombea nafasi ya mgombea Urais toka CCM. Kiasi hasa alichukua watakuwa wanakijua wao wawili au at least RA maana inaelekea anaandika kila pesa anayoitoa.

Sasa Kikwete anajua akimgusa tu na kumuudhi, jamaa anaweza kumuanika hadharani. Ndiyo matatizo ya kuwa na kiongozi ambaye si msafi maana inafika wakati anashindwa kutenda hata wajibu wake kama kiongozi wa nchi kwa kuwaogopa watu waliomfikisha hapo alipo.

Kiongozi ambaye si msafi na amepata nafasi ya uongozi kimizengwemizengwe bila ya kuwa na sifa yoyote kamwe hawezi kuwa kiongozi mzuri. Na Kikwete ni ushahidi hai wa hili
 
Back
Top Bottom