Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

GT umekosea sana, hatuwezi kuhalalisha ubaradhuli eti kwa vile kuna manyang'au nchi jirani wanaiba zaidi.

Huyo Rostam na mafisadi wenzake dawa yao iko jikoni inachemka, kama JK ataendelea kuwaonea aibu wananchi sio mabwege tena na wanapokatishwa tamaa hujichukulia sheria mikononi.
 
sipendi kuamini kwamba gt unamtetea rostam kwa sababu
huko kenya nako wanaiba!
labda ndio maana rostam kafungua ofisi nairobi.
 
911,
Shukran mkuu wangu kumbe ndo hayo eeeeh!.. duh, mtani wa jadi ka smell!..
 
Unawaibia watu maskini wanaokufa kwa njaa--yet duniani ukipata kuishi miaka 70 au 80 ni bahati ya Mungu!
 
hatuwezi kuiga mambo ya kipumbavu na ujinga, RA at el muda wao utafika 2 na watakili kwa vinywa vyao, mambo ya kenya ni kenya na bongo ni bongo
 

acheni unafiki jamani..............UOZO NI UOZO TU.......hatu-justify uozo kwa uozo.......au kuna mtu kaiba password yako nini!!!
 

Huyu ni Alnoor Kassam wa Tanzania (aliyekuwa waziri wa fedha under Nyerere) au mwingine?
 
Huyu ni Alnoor Kassam wa Tanzania (aliyekuwa waziri wa fedha under Nyerere) au mwingine?

Afadhali kwa jirani zetu, wezi wao wakuu ni wanaKenya na watazikwa hapo hapo chini kwao. Wezi wetu ni wakuja wanaotumia migongo ya WaTanzania na wengi wao watazikwa Ulaya, Asia, na Marekani - nje kabisa la continenti la Afrika.

Kibaya zaidi afadhali hata hizo za jirani zina hesabika, za Bongo hazihesabiki. Uchumi wa Dunia unasemekana umechangiwa kwa asilimia si ndogo na hazina ya Tanganyika katika kipindi cha miaka 20 na ushee - cha mlevi huliwa na mgema.

Jamhuri ya Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu - ukijua inavyoliwa na wageni utalia. Mara mia heri kwa jirani zetu - asilimia kubwa wanawekeza humo humo nchini. Wageni huingia Bongo wakiwa masikini, lakini huondoka mamilionea wakituachia mahandaki !!
 

Hamna cha afadhali wala nini, ufisadi ufisadi tu.Ukiisoma hiyo KTM report utaona wahindi wanatawala East Africa.
 
Nyerere hakuwa mdini haslani isipokuwa wewe "Game Theory" ndio mdini na maandiko yako mengi yanaonyesha hivyo; kuwa waislamu wameonewa katika vipindin vyote vya utawala nchini mwetu na ndio maana muungwana amekuteuwa wewe na wenzio muwatafute waislamu " Waliosoma" na majina umpelekee Ghasia ili nafasi za uteuzi zikitokea priority wapewe waislamu; ndio maana wewe ukatunukiwa hata uenyekiti wa Benki fulani; sasa huo ndio udini kwasababu uislamu ndio kilikuwa kigezo cha kwanza na sio elimu wala uwezo wako. Nyerere hakuwa anafanya hivyo ama sivyo asingetaifisha shule za wakisto ili waislamu wapate nafasi za kusoma badala ya kung'ang'ania madrasa tu!! Itakuwa dhambi kubwa kama tutalinganisha wezi wetu na wa hao nyang'au jirani zetu; wezi wetu wakina Roatam, Lowassa, Karamagi etc lazima tuwakabili vilivyo mpaka kieleweke ingawa muungwana anawalinda!!
 



Kwanza una uhakika gani Mafisadi wa Tanzania hawana hizo ranch za mahekta huko Austaralia !!!!!!!!!!!!!!!???

Mzee ongeza nguvu ya kufichua mafisadi hali ni mbaya kuliko unavyofikiri!!!
 
Jasusi,
Kuna taarifa nimezipata kuwa jumba alopewa (zawadiwa na serikali) Alnoor Kassam ni moja kati ya majengo ya kushtua matano (5) in Dar!..
 
Kwanza mtacompare vipi na wa Kenya their economy is worth 10Billion Dollars more than ours.. It makes no sense.. They, in effect, have more money to steal..lol.. SO Rostam is no better... And this thing about waislam kuonewa, its absolute rubbish.. For one, there has not been enough evidence to support this in the terms referred to above, ie Presidential administrations. There have been a grand total of 4, (the 4th ongoing).. SO no accurate conclusion can be derived from this. (wait another 40 years then ongea)..

It is a fact that the Catholic Church supports any administration that is headed by its own for the reason that their motives can be protected... Lakini Nyerere japokuwa initially atakuwa alikuwa supported na hawa watu, and he was one of them, he saw that nationalism is the only way that Tanzania could have a lasting or maybe semi-lasting peace. So if he did anything on religious grounds, it was to a minimal extent perhaps in a clandestine fashion..
 
Naomba Wana JF mnielimishe na kunifahamisha.
Mhe Rostam Aziz aliwekeza sana ili JK aingie ikulu...na sasa ni wakati wake wa kuvuna...Kwa nini mnamlaumu.????..Je ingekuwa wewe umewekeza hivyo ungepeleka mambo yaendaje???
Je alaumie RA au JK au WaTanzania waliomchagua JK???

NAOMBA JIBU BILA JAZBA....
 
Ndiyo maana kuna kila sababu ya kuhakikisha Kikwete harudi tena madarakani. Maana kiongozi aliyeweka mbele maslahi ya mafisadi waliomkirimu ili kuingia IKULU hatufai kabisa Watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…