Rostam Aziz Tanzania First Billionaire sells his Vodacom Shares (Forbes Magazine)

Hizo kampuni zote uliambiwa hazilipi kodi? au unakurupuka tu?
Unajua maana ya registered Holding company na characteristics zake abroad (ndio sababu ya kukuuliza hizo biashara zingine zipo chini ya mwamvuli gani), unafahamu sheria za tax UK, sababu za makampuni kufunguliwa Jersey.

Rostam makazi yake permanent ni wapi na kwanini akafungue a Holding company in Jersey. Huyu bwana si mlipa kodi na huko ni kukosa uzalendo, maendeleo hayawezi kuja kwa walipa kodi waaoendesha biashara ya ma-guest na faida zao tia maji maji (wafanya biashara ambao kutwa ulikuwa ukiwananga kwenye sakata la machine za edf), nchi za wenzetu wafanyabiashara kama hao hawana ata mpango nao hila hawa wenye kulipa mabillioni ndio mpango mzima. Kodi ya Rostam ya mwaka ingekuwa sawa na maelfu ya wafanyabiashara wadogo halafu tunaulizana sababu za umaskini.

Hakuna mtu mwenye dhambi kubwa kwenye uislamu kama mtu mnafiki wewe bibi inabidi uji chunguze maana utaungua vibaya sana siku hiyo.
 
Huyu rostam amesajili kampuni yake njee huko jersey .ni kampuni hio ya nje ndio ili nunua shares za vodacom.
Sasa ni company hio hio ndio imeuza baadhi ya share zake...no bid deal hapa ni mali yake na wao kama shareholders waliingiza capital na nguvu zao kuifikisha vodacom hapa ilipo.
Mambo ya kawaida tu.
Tungekua tuna policy isiyo yumba ya uwekezaji hawa wasinge kwenda jersey kuusajili company. Lakini kutokua na policy madhubuti ya kulinda vitega uchumi ndio maana watu wanakwenda nje kufungua company then wakija hapa wanalindwa na sheria za kimataifa za uwekezaji.
Ibrahim Mo ni billiinare ambaye alikua anaanzisha makamouni ya simu then baada ya muda anauza share zake na ammetajirika sana na leo ni mmoja ya matsjiri wakubwa afrika.
Tuache uchoyo mtu akipata ni chake...na wewe kione mavi.
 

Watanzania ni watu wa ajabu sana walewale ambao ndio wa kwanza kupayuka kwenye ukuaji wa deni la taifa upande mwengine utakuta wanatetea wakwepa kodi wakubwa sasa serikari itaacha vipi kukopa kama matajiri si walipa kodi. Halafu kwa kuangalia Rostam share zake akununua bali alikuwa ni mmbia from day one wa vodacom, kinachofanyika ni vodafone kujaribu kuongeza share katika vodacom through internal acquisition.

Kwa upande wangu sijali Rostam aliingia ingia vipi ubia kama aliwaalika yeye Tanzania nakuweka terms zake, ama la.

Tatizo lilipo hata kama kweli kuna matatizo ndani ya taifa ya kimfumo ni wao na genge lao la wafanya biashara ndio wanatakiwa ku-lobby jamani siasa zetu kwa sasa azimlindi mfanyabiashara, mazingira ya kufanya biashra si mazuri, siasa za visasi na kukomoana si nzuri watu tutaogopa kuwekeza. Wafanya biashara wakubwa ni watu wenye nguvu, na wana huwezo wa ku-influence policies, hila wao kwa sasa ndio kikwazo cha kupewa sera nzuri sidhani hata kama wanaishauri serikari kisera else tungesikia ukosoaji wa sera na ulinzi wa biashara zao. Ndio kwanza wapo busy na tamaa za kupewa vitalu.

Lakini zoezi la kukimbia kulipa kodi kwa visingizio ambavyo havina ushahidi siafiki, wao ndio wapo juu wasipo lobby kubadilika kwa mazingira hatarishi ya biashara na assets zao nani afanye kazi hiyo, mbona Bakhresa analipa kodi na kasajiri kampuni zake Tanzania.

Kulipa kodi ni uzalendo, khaa na tuache kudhani kila mwenye kukosoa ana lake jambo, kupata si bahati bali ni jitihada tu.
 

Wewe wacha porojo, sababu ziko nyingi sana. Kumbuka kuna Tax evasion ambayo ni dhambi na kuna TAX avoidance ambayo si dhambi. Kama unaongelea kuhusu TAX avoidance, hiyo ni wazi na ni mbinu ya biashara kubwa kubwa zenye msingi mkubwa. Huwezi kujiona unalipa double taxation kwa sababu tu hujatumia mbinu za ku avoid. Utakuwa ni punguani.

Ku evade tax ndio dhambi, sasa wewe tuwekee ushahidi kuwa Kampuni za Rostam zime evade TAX si Tanzania tu na kwingine kokote zilipowekeza. Kumbuka Rostam anawekeza nchi nyingi na si Tanzania pekee.

Kama huna huo ushahidi, wewe kaa kimya wacha wanaojuwa kuicheza hiyo game waicheze, huna ulijualo zaidi ya kuhororoja tu.
 

Tatizo lako unakuja hapa kubwabwaja kwa kulishwa maneno usiyoyajua umejiuliza kwanini nilitumia maneno tax evasion, kulipa kodi ni uzalendo na sio maneno kama tax avoidance au kusema kavunja sheria.

Kukusaidia Rostam Aziz ni raia wa Tanzania hakuwa na sababu nyengine yeyote ya kufungua kampuni yake ya 'Calvary Holdings' in Jersey zaidi ya kukwepa kulipa kodi (hiyo ndio tax evasion) si kila mara lazima uvunje sheria kama ulivyokaririshwa na ndio sababu ya kusema kulipa kodi ni uzalendo maana at times it is just a moral issue.

Tofauti na tax avoidance ambapo mara nyingi ni international firms wanapoamua kuvuruga mahesabu yao ya ndani such as in transfer pricing ama kuweka head quarters of their businesses on lower corporate taxes nations, those of which are within tax treaty nations (huwezi kujua sana kuhusu hili mpaka upate accounts zao). Lakini hata hayo makampuni utakuta yana home-base ambapo mwanzilishi/waanzilishi wanalipa corporate tax fully ni during expansions tu ndio wanavuruga kupunguza tax.

Sasa wewe mtanzania unapoenda kufungua kampuni yako straight up in Jersey, automatically unakuwa a scrupulous character, in the midst avoiding paying taxes and reducing the amount of tax you have to pay where necessary.

Nyie ndio watetezi wa chama tawala humu ndani hiko chama kina maadili kweli umo ndani? maana issue hapa ni maadili than anything, ambapo wewe unatetea uvunjifu wake, ama kweli shibe mwana malevya njaa mwanamalegeza.
 

Ewee punguani, unaleta porojo bila ushahidi. Ni nini kinachomzuia Rostam au raia mwingine yeyote wa Tanzania kufunguwa kampuni Jersey, au kwingine kokote kwenye tax havens duniani?

Wacha kuwa punguani, tax havens haziko Jersey tu, zipo nyingi sana duniani. Hizo ni mbinu tu za kuweza kuhamisha mitaji na kuepuka kihalali Tax zisizokuwa na tija kwa biashara wala nchi.

Tanzania ni wapi inapowazuia raia wake kufunguwa makampuni au akaunti nje ya Tanzania?

Usiwe -----, kuwa na muono mpana. Biashara ya kwako ndani unayoifanya wewe na mkeo na mkweo na wajukuu zako hata iweje haiwezi kukuwa, itabaki inazunguka hapo hapo. Ni lazima utoke nje ya himaya yako ukitaka kujiongezea mapato.

Faflukhta hundi Ulaya Ng'ombe Mwitu. Usiyesikia la muazini wala mteka maji msikitini.

Unachobisha ni nini? ewe punguani!
 
Nilisha kwambia ujui unachokiongea tax evasion ndio inaweza kuwa kosa au lisiwe kosa depending on the act.

Tax avoidence sio kosa, kwa sababu vitu hivi vinafanyika within the required boundaries of the law, hila hata serikari za wazungu zinaanza kuingilia kati be it softly kwa sababu na wao wanapata faida za ajira na PAYE na faida zingine ukitoa corporate tax, sasa usidhani watu wanajiendea sehemu yeyote yenye tax haven bila ya kuzingatia sheria za hizo nchi na sehemu wanazofanyia biashara kama wanaruhusiwa. Kama utaiangalia biashara ya mfadhili wako kwajicho hili sawa ana makosa hila halimfuti sifa ya uhuni wakutotaka kulipa kodi.

Lakini kama utarudi kwa Rostam kufungua biashara Jersey ilihali yeye ni mtanzania tayari hiyo ni tax evasion, hata kama ajavunja sheria Obama na Marekani wameivaa 'Cayman Island' kwa upuuzi huu maana the motive of the practice is clear Kukwepa kodi largely unapoishi. Kuna tofauti kubwa sana hapo na Tax avoidance practices, sio mwalimu wako mie. Hila Rostam Aziz anakimbia kodi anapoishi.

Kwa sasa ingawa hakuna kosa kutokana na kukosekana sheria za kudhibiti raia kukwepa kodi kwa nchi maskini, lakini Rostam ni mkwepa kodi he should be named and shamed, who know may be one day Sheria uchwara iliyopo ya "Maadili ya Viongozi wa Umma' itapewa meno na watu kufungwa au kutozwa faini za nguvu vinginevyo utakuwa mwanya wa wafanyabiashara matajiri kukimbia na kwenda hizo nchi ambazo zipo tayari kuchukua kitu kidogo kuwalinda, Marekani wanabadilisha, UK huwezi unless uhame na nchi kabisa kama walivyofanya hakina Lewis Hamilton, hila wajue wakitua tu sheria hipo palepale mwisho wa kukaa UK ni miezi sita tu kwa mwaka sijui miaka miwili or else you pay the tax kama raia wengine.

Halafu wewe bibi sijui una matatizo gani, yaani kila mara upo upande wa maovu: kama sio kugombana udini, utaki muungano na sasa utaki raia walipe kodi. Nakukumbusha tu unafiki ni zambi kushinda mchawi ukizingatia wewe ni vyote subiri siku yako ndio utajua.
 

ewe dada una maneno makali sana,. Jaribu kupunguza kidogo,,
 
Naona umeishiwa hoja unaleta viroja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…