Rostam katika tope jipya

Rostam katika tope jipya

Hee hee hee heee heee heee,

Rostam kapatikana na ufisadi mwingine? Lazima hapa kutakuwa na sababu ya msingi kabisa ya kumtetea Rostam. Fundi Mchundo atasema kuwa kuna typo error hapo (na hizo pesa sio nyingi kiasi hicho au ..) huku companero akisema kuwa huyo CAG ni mfuasi wa Mwanakijiji.

kwi kwi... weekend imeanza vyema,
Jamani huyu fisadi hata umkogeshe kwa mapipa kumi ya jiki, hatakati, jamaa ni fisadi fisai wa kutupwa, kila uchafu yumo!

Haya tusubili Mkuchika na Sofia wamwambie CAG naye ana mamlka gani? yeye kama nani?
 
Hili tope jipya ama la zamani/la siku zote? Huwa najiuliza sana kama jitihada za wana JF hapa zina manufaa gani kwenye kuleta mabadiliko,maana wengi wenye uwezo wa kusoma hapa si ni mafisadi? Mtanzania gani wa kawaida atakajisumbua kufuatilia hata wakati mlo wenyewe tabu?

Tuombe Mungu tu Rostam na wenzake wawaonee huruma wajomba zetu na ndugu zetu kwa ujumla ili waweze kuisaidia Taifa Stars na UVCCM ili taifa liendelee kupata maendeleo ya soka na mbinu mpya za ufisadi. Tuweni wavumilivu tu,labda tutaweza kushinda kombe la Afrika na kuweza kushiriki kombe la dunia. Naamini JK na RA na kina Manji watatufikisha uko,mengine yote muyaache kwani hamyajui na mnajisumbua tu kwani amani itapotea kabla hata hatujashinda kombe lolote lile,wala kabla Yanga na Simba hazipata kombe la klabu bingwa ya Afrika.

Hivyo basi watanzania ni bora mjikite kwenye issues ambazo mnaweza kuzi handle,mengine yote waachieni viongozi wao wanajua njia sahihi za kutupatia maendeleo.
Ni maoni tu.
 
Mnajua hapa mnamfanya Kubenea kuwa ni Mungu na kila analosema ni kweli,mimi nakwambieni kuwa Rostam hajawahi kufanya kazi ya kuuza mahindi,tena hio kampuni wala haijapata kuwa na jina lake......lakini kwa kuwa wamedanganya kuwa ripoti ya CIG imesema hivyo kabla ya kuchangia hapa wngapi mnaweza kusema mmeiona ripoti hio au mnamsikiliza tu kubenea wenu kilaza namba moja
 
Hongera we kipanga namba moja wa kumtetea Fisadi papa Rostamu Azizi.

Angalizo, Bora niwe kilaza kuliko kuwa kipanga wa kutetea mafisadi
 
Mnajua hapa mnamfanya Kubenea kuwa ni Mungu na kila analosema ni kweli,mimi nakwambieni kuwa Rostam hajawahi kufanya kazi ya kuuza mahindi,tena hio kampuni wala haijapata kuwa na jina lake......lakini kwa kuwa wamedanganya kuwa ripoti ya CIG imesema hivyo kabla ya kuchangia hapa wngapi mnaweza kusema mmeiona ripoti hio au mnamsikiliza tu kubenea wenu kilaza namba moja

Fisadi Mtoto,muda umeshapita sana tu toka uzaliwe,na ni wazi kwamba sasa umeshakuwa na Mafisadi wakubwa wanaweza kukutuma,wanasema kua utumwe.

Nani ailkwambia kuwa wanaotoa tenda wanaangalia eti kama anafanya biashara ya mahindi? Kuna biashara fisadi asiyofanya? Angalia...Utaanza kusema ooh hafanyi biashara ya ngozi na viuongo vya Albinos kwasababu hana historia ya kuuza viungo hivyo.

Hii mijadala hapa inachosha,sijui ni kwasababu kiswahili bado ni lugha inayokua ama ni lugha ngumu,sijui. Ila kwasababu ya lugha hii hii,bado tunaweza kuona common sense inazidiwa nguvu na porojo.
Kwamba kampuni haina jina la RA,hilo bado linatoa nguvu kubwa sana hapa na fursa kwa wale wenye mwelekeo wa kifisadi pamoja na viongozi wenye kuwalinda.

Na kwasababu tumezoea kuomba omba,basi tusisahahu kuomba Mungu ili at least hata ale ambayo tunayajua sana kama mpira wa miguu na kusafiri ili tuweze kupata maendeleo.
Tuweke mshikamano kwenye Taifa Stars na uvccm ili tuweze kupata maendeleo kama vile kupata wachezaji wa kulipwa,Yanga ama Simba zitwae makombe ya Afrika na pia tuweze kushiriki kombe la dunia,Ni rais ama kiongozi ama fisadi gani atakayewahakikishia watanzania hayo mambo na asipendwe?

Akili kumkichwa,ukila na kipofu usimshike mkono na mijinga ndiyo iliwayo.

Hivyo Fisadi Mtoto,uwanja wako....Sisi tutaandika Historia na kuwasimulia tu ili wajukuu zetu nao wasipitwe na historia hii muhimu.
 
...mimi nakwambieni kuwa Rostam hajawahi kufanya kazi ya kuuza mahindi,tena hio kampuni wala haijapata kuwa na jina lake......kwa kuwa wamedanganya kuwa ripoti ya CIG imesema hivyo

Hivi hizi ripoti za CIG ziko ngapi? Ile iliyowasilishwa bungeni April 27 mbona mambo haya ya Rostam haina? Wala hiyo kampuni ya Tanzania Packages haimo, wala habari ya kuagiza mahindi. Kuna ripoti ngapi zaidi ya hii:
 
Attachments

CIG..... Bwa ha ha hahaha ha
 
2005 watu walivumisha kwa nguvu zote kwamba Rostam Aziz amepata fedha kutoka Iran kusasidia CCM ishinde.MWaka fulani kule nyuma niliwahia mabiwa Salim A Salim alipata msaada kutoka MArekani kusaidia jeshi na nchi.MWaka mwingine kabla ya uchaguzi wa 1995 niliambiwa Malecela amabadili jina na kuwa Mufti na kapewa Mamillion kutoka nchi fulani ya kiarabu ili kusaidia CCM. Wenyeviti wote wa CCM wa mikoa na wilaya walifaidika moja kwa moja na fedha hiyo.Stori zote hizo zilikuwa ni kwajili ya kutuacha kwenye mataa.Hakuna mtu wala kikundi cha watu wala serikali ya kighaibhu iwezayo kuleta fedha Tanzania kusaidia chama bila maharti ya kuivisha serikali yetu ushungi.Fedha zote za hawa watu asili yake ni wizi wa Kimafia ndani ya serikali.Hivi tuongeavyo lazima kuna mipango mia kidogo ya kiibilisi chini ya utawala wa CCM ya kutafuta fungu la kushinda uchaguzi mwakani.Za mwizi ni 39, 40 ni pingu tu.Haya MH Mkuchika unalo, Mkuu wa Ideology ya CCM MH Rostamu Aziziz yu anapigishwa mbizi ndani ya matapishi yake tena, longa tusikie kilongeo si unacho??
 
Mnajua hapa mnamfanya Kubenea kuwa ni Mungu na kila analosema ni kweli,mimi nakwambieni kuwa Rostam hajawahi kufanya kazi ya kuuza mahindi,tena hio kampuni wala haijapata kuwa na jina lake.....

Of course.. kampuni gani nyingine yenye kufanya biashara ambayo ina jina lake?

.lakini kwa kuwa wamedanganya kuwa ripoti ya CIG imesema hivyo kabla ya kuchangia hapa wngapi mnaweza kusema mmeiona ripoti hio au mnamsikiliza tu kubenea wenu kilaza namba moja

sasa hii ni hoja.. kwamba hiyo ripoti haipo na haijasema inachodaiwa kusema..
 
Kuna mtu anaweza kutu wekea hiyo ripoti ya CAG anayo iongelea Kubenea? Ingewekwa mjadala ungekua factual zaidi maana hakuta kuwa na mambo ya "what if". Hapa mtu mmoja kauliza kama tumeiona hiyo report au tuna fuata tu. Ingekuwa vyema report ikawekwa tujue nini kilichopo ndani ili mwenye kubisha ajionee kwa macho yake mwenyewe. Ila so far we are going by the assumption that what is being said is what is in the report.
Hata mimi huyu RA kani chosha ila for the benefit of thoughs who continue to support him bora report iwekwe tujue moja ili tujadili what is important siyo if the report said so or not.
 
EDITORIAL: CAG reports on govt financial management must not be taken lightly

EDITORIAL
DAR ES SALAAM

THE auditing watchdog, Controller and Auditor General (CAG), has once again detected serious discrepancies in the government accounts for 2007/08. This is yet another indicator that public money is not properly managed and spent to good effect so as to contribute to improvements in public administration.

The latest CAG report has rapped the government and public bodies for misappropriation of funds amounting to millions of shillings.

Among disturbing revelations in the CAG report is how the controversial Dowans Tanzania Limited was wrongly paid a staggering $ 4,865,000 (approx. 6.7bn/-) by state-owned Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) under dubious circumstances.

According to the report, TANESCO paid Dowans the amount as reimbursement for costs incurred by the private company in airlifting electric power generation equipment and accessories to Dar es Salaam. However, the CAG report notes that the government and TANESCO made the huge payment to Dowans without actually being contractually obliged to do so.

The CAG has been pointing out such anomalies every year without fail, showing clearly how public funds have been poured down the drain. All these reports are being tabled in Parliament, but nothing seems to be coming out of them other than just getting shelved.

We just cannot continue to watch as these reports are being forgotten as if nothing of consequences has ever been mentioned or revealed. Is this not the sign of corruption which has taken roots and entrenched itself.

Misappropriation of public funds is bad enough but what is equally bad if not worse, is the manner in which an important institution of the democratic establishment, meant as a vital checking and regulating mechanism of the power structure, has been systematically reduced to a caricature. Its annual reports have also been reduced to a mere official formality essential only to complete a constitutional obligation.

The government does not seem to take the CAG reports seriously, and because of the scant respect they have been showing these reports, the public also do not any longer take them seriously.

Despite all the rhetoric of fighting corruption and introducing transparency in the government, the inescapable fact is, nobody who has had a scent of executive power ever remains interested in translating words into action.

Perhaps even the CAG too has come to treat the job of coming out with annual reports as nothing more than completing an official necessity, without ever believing or hoping more action would follow.

In his last New Year address, President Jakaya Kikwete had called for immediate handing over to law enforcement organs of any public servant found by a government auditor to have stolen or misappropriated public money. He went on to call on the CAG to work hand in hand with the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB).

How far has this presidential directive been heeded? How many culprits are under probe by PCCB as a result of these anomalies revealed in the CAG reports It is up to the authorities concerned to answer these pertinent questions.

The president wanted the involvement of PCCB because he knows it is not the task of CAG to investigate what led to the discrepancies, but to point out the specificity of what happened.

It is high time a tough law was enacted to make sure nobody takes the CAG’s annual reports on the government's financial management, lightly.
 
Je jamii forum huyu mtu anayeitwa RA hamchoki kusoma habari zake ?Kila kukicha lazima tusome habari zake.Sasa tumechoka naye kwanini mtu mmoja asijitoe muhanga achukue yale yaliyobakia pale mbagala amsogezee kwenye gari lake ili tubadilishe discussion yake.Kwani wale ndugu zetu waliokufa pale na yale mabomu wanatofauti gani nayeye anatakiwa atafutiwe ajali.Mtu mmoja hawezi akawanyo na kuwadharau watu hiyo ndio ushauri wangu .
 
Masahihisho

Mtu mmoja hawezi kuwanyonya na kuwadharau watu million 40 huo ni upuuzi.
 
Je uko tayari kujitoa muhanga?
 
Masahihisho

Mtu mmoja hawezi kuwanyonya na kuwadharau watu million 40 huo ni upuuzi.

Ni Upuuzi zaidi pale inapokuwa wazi kabisa kwamba hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kupiga domo...Haiwezekani kabisa,lazima tutakuwa tuna matatizo serious ambayo wala haiitaji mzungu wala mwarabu kutuambia,Nyani Ngabu tu anatosha,sema na yeye yumo ndani ya tope hilo hilo.NO WAY OUT!

Ndio maana nikatoa ushauri kuwa watanzania wajikite kwanza kwenye mambo rahisi kabisa ambayo wameshindwa kuyafanya kwa miaka nenda rudi,mambo ambayo ukiyashughulikia basi unapendwa na hata kura unapata na wananchi kusahahu kila kitu,kuhakikisha Taifa Stars inashinda na Yanga na Simba zinanyakua kombe la klabu bingwa ya Afrika.
Akili ya maendeleo bado sana tu.
 
Ndugu wange fanya yote hayo kama wangekua na nia ya kweli na wananchi. Wao shida yao biashara, wafanye yote hayo wakati shida yao waingie tu na waibe.

HAWAIBI WAPATE KURA WANATAFUTA KURA WAPATE KUIBA
 
Ndugu wange fanya yote hayo kama wangekua na nia ya kweli na wananchi. Wao shida yao biashara, wafanye yote hayo wakati shida yao waingie tu na waibe.

HAWAIBI WAPATE KURA WANATAFUTA KURA WAPATE KUIBA

Taifa letu ni taifa lenye utamaduni wa kupiga soga. Hapo we are the BEST.
Kama ni utumwa wa kifikra unaopelekea umasikini,njaa na maradhi, ni wazi tumeuchagua wenyewe,kama kuna wananchi masikini kabisa hawajui lolote kuhusu utajiri wa nchi yao na ufisadi unavyosababisha umasikini wao,halafu plus wana JF wenye upeo mkubwa wakiendelea kuwatetea hao mnaowaita maadui wa Taifa hapa hapa JF,TENA KWA NGUVU! Watashindwa vipi kupata wanachokitaka!
Utakuwa vipi omba omba na bado kudai uko HURU? How come? Yani uniombe nikusaidie halafu unipangie cha kufanya? Kwa utaratibu tunaoufuata si kila mtu keshapigwa bei kuanzia viongozi wakuu?
Hata hayo yote hawayafanyi kwa manufaa ya wananchi bali kwa maslahi ya kibiashara pamoja na kuendelea kutawala kwa upuuzi wa ushabiki wa mambo yasiyokuwa ya msingi kama vile mpira wa miguu nk.
Na ndiyo maana nikasema kama watanzania wanaamini kuwa hayo ndiyo maendeleo,basi acha wapate wanachokitaka.
Huwezi kuwalazimisha watanzania waone kuwa kuumaliza ufisadi ni maendeleo zaidi ya Stars kushinda ama Simba na Yanga.
Huo ni ukweli kizazi hiki ni bure na tusijisumbue. Ntabadili mawazo baada ya 2010,kwani sina imani na watanzania walio wengi.
 
Umesema ukweli. Tanzanians we can talk the talk but we can't walk the walk. Siasa za jukwaani tunaweza ila utekelezaji sasa. Ndiyo maana kuna miradi mingi iki tangazwa mpaka mwenyewe utapenda ila ikija kwenye kutekeleza misaada hiyo hakuna chochote. Tatizo Tanzania rushwa kila sehemu. Hata hela zilizo lengwa kusaidia wagonjwa, masikini na watu wenye shida zinaliwa.
Hapa wengi tuta piga kelele ila 2010 matokeo yale yale na ni kwa sababu wenye kuongea tu ni wengi kuliko wanao tenda. Tanzania ufisadi siyo tatizo pekee, hata mentality ya what inatia wasi wasi.
Ndiyo maana Dewji yeye kajiamulia kufadhili zake mpira katulia. Wengi wana lalamika oh tuna wabagua tuna wabagua mbona wakina Dewji hawaja tajwa kama mafisadi papa.
Lakini you can't control others, the best you can do is control yourself & hope others do the same. Tuta jaribu kubadilisha taifa lakini watu wenyewe wasipo taka kubadilika kazi ipo.
 
Hii ingekuwa ni vita ya Risasi, sisi walala hoi tungekuwa karibia kwisha na pengine jeuri yetu kutupwa lupango ioze huko.
Kwa sababu hii bado ni vita ya maneno, ni heri kwetu walala hoi wa ndani na wa ughaibhuni kwa sababu kibano kinazidi kuwaandama Mafisadi kila dakika.
Mafisadi hawawezi kukwepa kibano hiki kwa sababu kila liibukapo jambo kazi kubwa kwao siyo kurekebisha mambo, kazi yao kubwa ni kulinda heshima yao isipinde wala kuingia ukungu kwa gharama ya kuvunja taratibu na kusema uongo pia kulazimisha hoja. Kwa kufanya hivyo tu, kuvunja taratibu, wanajitengenezea kashfa za kesho kiulaini.
Mafisadi walikaa chini pale ikulu kuandaa mikakati ya kuiba na kugawana kisicho chao, hata siku moja hawakuwahi kuota kwamba siku itafika siku ambayo watawajibika kwa wananchi na kutakiwa kutoa maelezo ya kina juu ya wizi uharamia na uuaji wao.
Mafisadi bado wanaamini kwamba Utawala wao ni wa kudumu kwani hawaoni kati yetu nani mwenye uwezo wa kukali viti vyao na makalio yake madogo.
Mafisadi hawana plan yeyote ya maana ya kujikinga na mashambulizi yetu kwa sababu plan hiyo haijawahi kuwekwa mezani kwani haikuwa ni plan ya lazima.
kila liibukapo jambo, kila mmoja hutoka kivyake na kusema mbovu na kuishia kimya kimya.
Ni juzi tu hapa wamesema mengi sana kwa vile tu Kanda mkuu na Bosi wa Idiologi ya CCM MH Rostam Aziz alipakwa tope la usoni.
Ni haki yao kumlinda mtu mwenye IQ kubwa ya kujenga umoja wa Chama kama Rostam Aziz. Huyo ni Juche mshauri mkuu wa MaoTse Tung.

Endelezeni mapambano yenu.
Vita ya maneno nayo ni vita.
 
Back
Top Bottom