Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Kwa mjibu wa gazeti la The Citizen tajiri Rostam Aziz amenunua hisa nyingi za Coastal ambayo ni Kampuni inayojishughulisha na usafiri wa anga.
Kwa umafia wa kibiashara wa Rostam Aziz Air Tanzania itapona kweli?!
======
Mfanyabiashara Rostam Aziz ameingia kwenye sekta ya usafiri wa anga baada ya kununua hisa za kampuni ya Coastal Travels Company Limited, hatua ambayo inatajwa kuleta ushindani kwenye sekta hiyo.
Kupitia Kampuni yake ya Taifa Aviation, Rostam amenunua 51% ya hisa za Coastal Travels kutoka kwa mwekezaji wa Kiitaliano Carolina Colangelo na kumfanya kuwa mwanahisa na mwekezaji mkuu wa Shirika hilo la Ndege.
Takwimu za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) zinaonesha Coastal Travels inachukua 3% ya Usafiri wa Anga ikishika nafasi ya 4 huku AirTanzania ikiongoza sokoni kwa 52.9%, Precision Air na Auric Air zikishika nafasi ya pili na 3 kwa asilimia 22.8 na 10.3, As Salaam Air nafasi ya 5 kwa 2.8% na mashirika mengine yakigawana 8.6% ya soko.