Rostam: Umejibu na watanzania wamekusikia

Rostam: Umejibu na watanzania wamekusikia

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Upo usemi kuwa usihukumu kabla ya kusikia upande wa pili. Kwa aliyepata bahati ya kumsikia Polepole kuhusu sakata Rostam kujinyakulia mgodi wa makaa ya mawe na ule wa almas atakubaliana na mimi kuwa maelezo ya Rostam kujibu tuhuma hizo, hata kama humpendi vipi, yamezififisha sana hoja hizo.

Binafsi sina urafiki na Rostam, lakini kwenye hili, kama aliyoyasema ni ukweli, nitakuwa mtu wa mwisho kununa mtanzania mwenzangu akifanikiwa kununua hisa kwenye kampuni za kigeni zilizowekeza hapa nchini.

Ni muhimu tukajiuliza, kama Rostam ambaye ni mtanzania amenunua hisa kutoka kwa wawekezaji wageni tunanuna, Je, tulitaka hisa hizo anunue nani? Waendelee kubaki nazi wawekezaji wa kigeni, au wanunue wageni wengine? Nadhani tunapaswa kujifunza kujivunia mafanikio ya watanzania wenzetu pale wanapokuwa wameyapata katika njia halali.


View: https://vm.tiktok.com/ZMArWB2Sm/
 
Mnalazimisha asikie huku akiwa hana cha maana ?

Ni swala la muda tu wote hao makazi yao yatakuwa gerezani
 
Mnalazimisha asikie huku akiwa hana cha maana ?

Ni swala la muda tu wote hao makazi yao yatakuwa gerezani
Comrade naomba kujifunza kutoka kwako, mtanzania kwenda nje ya nchi akanunua hisa kutoka kwenye kampuni ya kigeni anakuwa amefanya kosa gani?
 
Polepole aliposema mitungi ya gesi ya kilo kumi ni 2500 huko Cuba nikajua dishi limeyumba.
 
Back
Top Bottom