Rosh Hashannah
JF-Expert Member
- Sep 13, 2017
- 3,415
- 2,043
Muunganiko wa wakali wawili wa muziki wa Rap kutoka Tanzania, Roma na Stamina ‘ROSTAM’ umeshika nafasi ya juu baada ya sifa na pongezi kusambaa zaidi zinazowataja kuwa ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri kwa umoja wao pindi wanapokwea jukwaa lolote la kiburudani.
Kupitia taarifa rasmi inayoonekana kupitia mtandao wa YouTube, video ya ngoma ya muunganiko wa wakali hao inayokwenda kwa jina ‘Kiba 100’ wakiwa wameshirikisha Maua Sama, chini ya uongozwaji wa Director Nicklass imeendelea kufanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza(#1 Trending Video) nchin Tanzania.
Hata hivyo wawili hao mbali na kuwa wako katika muunganiko wao wa pamoja, hawajai kukubali kuitwa kundi kwakuwa waliutambulisha umoja wao kama hatua pekee yenye lengo la kuleta burudani ndani ya ushirikiano wao tu huku wakiwaachia mashabiki nafasi ya kufurahia kazi ya msanii mmoja mmoja pindi zinapoandaliwa na kutoka nje ya muungano wao.
Source: DizzimOnline