Royal Family wadhibitiwe, watavunja NDOA za watu!

Nimesoma nimeishia kucheka tu, mtu ana asset za karibia bilioni kadhaa huko aje kuhangaika na manyarugusu..mkeo atagongwa na bodaboda na type za mafukara ..sio.level za hao , huo muda hawana na wanajali na kuheshimu ndoa zao.....akiamua labda kutaka kuonja ladha tofaut atapanda ama kukodi private jet impeleke spain huko ama visiwa vya ibiza au private islands kwa watoto wakali wasio na hata kipele mwilini
 
Kwa namna wake zetu walivyo macho juu na tamaa aisee hii ni hatari tupu
Mwingine huyu huku👇 huenda nguvu yao imeshika kasi
 
Badala ya kudhibiti hao Royal Family, dhibitini wake zenu!
 
Ni kweli lkn serekali yetu imezubaa kudhibiti vitu kama hivi. Kamwe msiruhusu makundi yanye ukwasi mwingi bila kuyadhibiti ni hatari kwa nchi.

Fisiemu jitahidini kubaki kuwa wakubwa.

Msiruhusu kundi jingine lijiinue mkawa wakubwa wawili
Hauwezi kutoboa bila ya kuwa na team nzuri ya watu, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Nenda ka-google ''Paypal Mafia''. Mitandao inatudangayna kuwa unaweza ukatoboa wewe peke yako . Au kuwa kuna mabilionea ni self made. Hakuna kitu kama hicho kuna watu inabidi mshikane mikono muinuane. Umesema wadhibiti makundi ya watu wenye ukwasi mwingi. Hawa watu wametengeneza ajira na hela yao wanaiwekeza hapa hapa nyumbani. Nenda Upanga , na Masaki ukajionee wahindi na waarabu wenye ukwasi. Hapa Tanzania wana nyumba moja au mbili na kiwanda lakin hela zao zote wanazirudisha makwao. Hata ukiangalia wanaongoza kutembelea Magari ya mabilioni ya hela ni wahindi na waarabu.Je unajua wafanyakazi wao wnawalipa shilingi ngapi ? Kuna wahindi wanapewa tenda za mabilioni na serikali huku wana wafanyakazi chini ya 200 na wanawalipa 250000 mpaka 300000 kwa mwezi. Mpaka unajiuliza serikali ipo wapi ? Hawa wana makundi makali zaii ambayo ni ya kiukoo(Kwa waarabu) au ki-caste (Kwa Wahindi). Haya makundi yao hauwezi kuingia kama sio wao au jaamii yao. Hata matajiri wa kiarabu hawafanyi bishara na kila mwarabu kuna ukoo hawatakiwi kujishusisha nazo. Vivyo hivyo pia kwa wahindi, Mo hawezi kufanya bishara na Mtu wa Punjabi Kwa sababu yupo caste tofauti na yeye ambaye ni Mtu wa Gujirati. Hivi vitu Royal family hawajavianzisha wameiga kutoka kwa hawa jamaa. Lakini Royal family haina kikwazo cha asili au jamii ni uwezo tu wa kuwa na mawazo yanayofanana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…