Royal Tour ft Mama Samia: Wanaopinga wasome makala hii

"Kukuza sekta za huduma hususan utalii ili kutumia fursa zilizopo kikamilifu na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa. (Uk.14)"

Ndiyo! Imetajwa hivyo katika ilani, lakini utekelezaji wa wake ni lazima Mheshimiwa mwenyewe ndiye aende "front line" ama hili ni jukumu la wizara yenye dhamana ya utalii kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya nje.

Urais ni taasisi yenye majumu makubwa sana kiuendeshaji. Tunategemea Rais atumie zaidi "abstract skills" zaidi ya "administrative & technical skills" katika suala kama vile ambavyo inaonekana yupo "field" akifanya.

Matumizi ya "administrative & technical skills" ni jukumu la wizara na wataalamu wake kuhakikisha linatekelezwa kwa ukamilifu na umakini mkubwa chini ya maelekezo ya ofisi ya Rais. Rais ni lazima ahakikishe yale yote anayoyaelekeza yanafanyika kupitia kwa wale aliowaamini na kuwapa majukumu hayo. Si sahihi kwa yeye kwenda mwenyewe "field" kufanya kazi za wasaaidizi wake.
 
Haipingwi bali ni muhimu hiyo tour ikisha kamilika mahesabu yake ya shushwe ijulikane itagharimu billioni ngapi? Hii baadaye itasaidia kuiona value for money ya huu mradi.
Unawashwa sana mkuu
 
Haipingwi bali ni muhimu hiyo tour ikisha kamilika mahesabu yake ya shushwe ijulikane itagharimu billioni ngapi? Hii baadaye itasaidia kuiona value for money ya huu mradi.
Mkuu, ukitaka kula vizuri lazima ukubali gharama. Huwezi kuwa unaacha pesa ya matembele na ugali wa matamba ukitegemea kula pilau na kuku.
Sometimes tunatakiwa kuwa 'risk takers'.
 
Mkuu, ukitaka kula vizuri lazima ukubali gharama. Huwezi kuwa unaacha pesa ya matembele na ugali wa matamba ukitegemea kula pilau na kuku.
Sometimes tunatakiwa kuwa 'risk takers'.

Sitaki kuongea sana. Utalii unaotangazwa na Msafara wa Rais na Rais mwenyewe inaonesha ni mufilisi wa good practice on resources management. Msafara uongezewe na wazungu wengi na mikamera yao. Sijui gharama za production ya movie kule Hollywood ziko za kiwango gani na zinatofautia kwa kiwango gani na hawa Royal tour movie? Hatutaki Tanzania ije kuwa na kiongozi ambaye timu kubwa ya mpira wa miguu au kikapu wengereza au Marekani ikifungwa anakuwa mkali kwenye vyombo vya habari.
 
Jordan ni nchi ya kifalme ndio maana wana "Royal", mimi nauliza hapa kwetu hiyo "royal" ni ya nini? Au maana yake ni kumpa mtu "royal treatement"?
 
Jordan ni nchi ya kifalme ndio maana wana "Royal", mimi nauliza hapa kwetu hiyo "royal" ni ya nini? Au maana yake ni kumpa mtu "royal treatement"?
MKUU SOMA HIZZO

Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu and King Abdallah of Jordan are two of heads of state who previously starred in Greenberg's series; Kagame is the first from this continent.

Greenberg said that tourism went up almost 20 percent in Jordan after his “Royal Tour” with King Abdullah II aired, and 10% in Mexico, Peru and Jamaica after filming in those countries.
 
Viongozi wa hii nchi hawana vipaumbele kabisa , nchi Ina matatizo chungu mbovu rais anazungukazunguka for nothing
Greenberg said that tourism went up almost 20 percent in Jordan after his “Royal Tour” with King Abdullah II aired, and 10% in Mexico, Peru and Jamaica after filming in those countries.
 
Sasa kukuza utalii siyo jukumu la rais? KumbuKa utalii ndicho chanzo namba moja cha kuingiza fedha za kigeni halafu rais anayejali akipuuze KWELI?
 
Sasa nimeelewa.... hii ni show kama zilivyokuwa na kina Anthony Bourdain(RIP)
 
Wenzetu wanatangaza utalii lakini sisi tunawatangazia wawekezaji kuwa sasa tunademokrasi, tunawaonesha madini n.k. ili wawekezaji waje. Maswali muhimu ya kujiuliza:-

(1) Je Tanzania tuliwahi kutokuwa na amani?

(2)Bado tunalia na mikataba mibovu ya madini, je mama ataingia mikataba hiyo kwa sheria zilex2 za sisi kupata asilimia 3% au zero na misamaha lukuki ya kodi huku madini yote yakichukuliwa na wageni?

(3)Nchi haitaingizwa kwenye migogoro?

NB:-
(a) Wawekezaji halisi ni wazawa, hawa watu weupe ni wafanyabiashara kwa maslahi makubwa ya mataifa yao!

(b) Maendeleo ya nchi huletwa na wananchi wa taifa husika, siyo wageni.

(c) Wapo watanzania wenye uwezo, wapewe fursa hizi & the government should empower/support them.
 
Sasa nimeelewa.... hii ni show kama zilivyokuwa na kina Anthony Bourdain(RIP)
Mkuu umeua- waamue tu kutoelewa
In death, as in life, Anthony Bourdain brought us closer together.
On his award-winning series, "Parts Unknown," Bourdain brought the world home to CNN viewers. Through the simple act of sharing meals, he showcased both the extraordinary diversity of cultures and cuisines, yet how much we all have in common.
 
Mimi ni mtazamaji sana wa hizi mambo..... ila nilikuwa sijawahi kuzioa hizi Royal Tours.. pengine kwa sababu huwa napenda kuangalia non official films.
 
Sasa kukuza utalii siyo jukumu la rais? KumbuKa utalii ndicho chanzo namba moja cha kuingiza fedha za kigeni halafu rais anayejali akipuuze KWELI?
Mkuu naomba utambue kuwa ni aina gani ya "skill" inapaswa kutumika pale unapokuwa upo katika "specific level of management" juu ya rasilimali zilizopo chini ya mtu ikijumuisha "human resources". "Positioning" ni suala muhimu sana ili kusimamia matokeo chanya.

Ni kwamba imetokea mapungufu makubwa ya kumuona Rais wetu kuwa ni "semi god" kutokana na nguvu alizokuwanazo kupitia katiba yetu iliyopo sasa. Kinyago tunakichonga wenyewe wakati wa uchaguzi, lakini mungu mtu pindi ashikapo madaraka anakuwa mtu mwingine kabisa licha ya uwepo wa makosa yake yaliyo dhahiri ya kiuongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…