Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Kama upepo ulivyo, habari za Royal Tour zishaanza kupita.
Watanzania tushahamia kwenye habari za Lengai Sabaya.
Toka mwanzo, mimi nilikuwa na shaka sana juu ya hiyo filamu.
Kama lengo lake lilikuwa ni kuitangaza Tanzania, mbona wahusika wake hawajafanya yale yanayopaswa kufanywa ili kuitangaza filamu hiyo pamoja na Tanzania?
1. Kwa nini Hangaya na waigizaji wenzake hawajaenda na kwenye nchi zingine? Kwa nini wameenda Marekani tu?
2. Na huko Marekani walikoenda, ni nani hasa mwenye habari na hiyo filamu?
3. Matangazo ya hiyo filamu yako wapi? Sasa hivi kuna playoffs za ligi mbili kubwa, NBA na NHL, mbona matangazo ya hiyo filamu hayapo kwenye chaneli za TNT, TBS, ABC, wala ESPN?
Michezo hii ya playoffs huangaliwa na watu wengi sana. Hapo ndo ilikuwa pazuri pa kuitangaza Tanzania na vivutio vyake.
Lakini hamna kitu. Sasa Mmarekani atajuaje kuhusu hiyo filamu?
4. Hiyo filamu ina kipi kipya ambacho hakijulikani kuhusu Tanzania hadi kumshawishi Mmarekani aje?
Documentaries zote kuhusu vivutio vya Tanzania ambazo zimewahi kuonyeshwa na PBS, National Geographic, A&E, YouTube, n.k., zina tofauti gani na Royal Tour?
5. Hii Royal Tour sidhani kama italeta chochote kipya na zaidi. Watu wamepata tu fursa ya kupiga hela.
Na kama ilivyo jadi yetu Watanzania, tushaanza kuisahau na ndani ya muda mfupi tutaisahau kabisa na hakuna hata mmoja wetu atayekuja kuuliza mafanikio yake huko mbeleni.
6. Ni nani atayekuja kumhoji Samia juu ya mafanikio ya hiyo filamu ifikapo 2024, kwa mfano?
Sisi ni watu wa ajabu kweli.