Imeandikwa usihukumu maana utahukumiwa. Na jambo usilolijua, ni kama usiku wa giza. Kinachonipa faraja ni kuwa Mwenyezi Mungu sio mnafiki na wala haonei mtu.
Tunaweza kumbebesha mtu matatizo ambayo wala sio yake. Ndio ubinadamu wetu. Ukweli ni kuwa wapo wengi walitumia sana vibaya nafasi zao. Na siamini kama wote walitumwa kufanya hivyo.