RPC Arusha: Kundi la Wadudu ni kama Wasanii, wanafanya Sanaa sio Wahalifu

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linao wajibu wakisheria wa kuwalinda raia na mali zao huku likibainisha kuwa limepokea maelekezo ya Mwenyekiti wa Ulinzi Mheshimiwa Paul Makonda aliyoyatoa hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo kufuatia maagizo ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo alilitaka Jeshi la Polisi Mkoani humo kuimarisha ulinzi na usalama ili kuwezesha biashara na shughuli nyingine za utalii kufanyika kwa ndani ya saa 24.

Akiwazungumzia vijana maarufu jijini Arusha, Wadudu OG, Kamanda Masejo amesema kuwa vijana hao siyo wahalifu bali ni kionjo cha Jiji la Arusha.

Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameendelea kufunga kamera na taa kwenye maeneo yaliyokuwa na wingi wa matukio ya kiuhalifu ili kusaidia kubaini uhalifu na wahalifu wa katikati ya Jiji la Arusha na Mkoa huo ambao ni kitovu cha Utali hapa Nchini.

Vilevile kamanda Masejo amebainisha kuwa lengo ni kuhakikisha mkoa mzima unakuwa na Kamera katika maeneo yote ili kusaidia katika doria na ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Aidha amehimiza suala la Maadili kwenye ngazi za familia na kuwalea vyema vijana ambao wana hofu ya Mungu ili kusaidia katika kupunguza matukio ya kiuhalifu katika jamii.

Pia soma

- Makonda: Watalii hawaji Arusha kulala wanakuja kula starehe, ni lazima Arusha iwe salama saa 24. Hao wadudu nitaongea nao
 
Kweli ni vionjo. Majuzi kuna wale bodaboda walijikabidhi kwenye TAKO LA NYANI.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linao wajibu wakisheria wa kuwalinda raia na mali zao huku likibainisha kuwa limepokea maelekezo ya Mwenyekiti wa Ulinzi Mheshimiwa Paul Makonda aliyoyatoa hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo kufuatia maagizo ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo alilitaka Jeshi la Polisi Mkoani humo kuimarisha ulinzi na usalama ili kuwezesha biashara na shughuli nyingine za utalii kufanyika kwa ndani ya saa 24.

Akiwazungumzia vijana maarufu jijini Arusha, Wadudu OG, Kamanda Masejo amesema kuwa vijana hao siyo wahalifu bali ni kionjo cha Jiji la Arusha.

Pia soma
- Makonda: Watalii hawaji Arusha kulala wanakuja kula starehe, ni lazima Arusha iwe salama saa 24. Hao wadudu nitaongea nao
Niliwaambia waliukuwa wanategemea makonda atumie nguvu ku deal na hao jamaa , mhe makonda atawashangaza
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linao wajibu wakisheria wa kuwalinda raia na mali zao huku likibainisha kuwa limepokea maelekezo ya Mwenyekiti wa Ulinzi Mheshimiwa Paul Makonda aliyoyatoa hivi karibuni.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo kufuatia maagizo ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo alilitaka Jeshi la Polisi Mkoani humo kuimarisha ulinzi na usalama ili kuwezesha biashara na shughuli nyingine za utalii kufanyika kwa ndani ya saa 24.
WhatsApp Image 2024-04-17 at 15.34.43_523142a6.jpg

WhatsApp Image 2024-04-17 at 15.34.40_55a58ccc.jpg
Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameendelea kufunga kamera na taa kwenye maeneo yaliyokuwa na wingi wa matukio ya kiuhalifu ili kusaidia kubaini uhalifu na wahalifu wa katikati ya Jiji la Arusha na Mkoa huo ambao ni kitovu cha Utali hapa Nchini.

Vilevile kamanda Masejo amebainisha kuwa lengo ni kuhakikisha mkoa mzima unakuwa na Kamera katika maeneo yote ili kusaidia katika doria na ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Aidha amehimiza suala la Maadili kwenye ngazi za familia na kuwalea vyema vijana ambao wana hofu ya Mungu ili kusaidia katika kupunguza matukio ya kiuhalifu katika jamii.
 
Hongera mkuu wa mkoa PCM kwa kuifanya Arusha na wadudu wafuate utaratibu wako....🤣
 
Wakiwa wengi ni Wadudu, akiwa mmoja ni Mdude..... ni vijana wacheshi sana.
 
Hao wadudu ni wa kukaa nao kwa tahadhari kubwa maake wengi wao wanavuta sana bangi na baadhi yao ni watumia madawa ya kulevya (unga)~miongoni mwao ni vibaka ,wakabaji na wezi
 
Tatizo unakuta li mtu kutoka sijui mwanza au kinondoni limeshiba dagaa na bando linaichafua Arusha!!
Arusha Iko poa sana kuhusu hao wadudu ni machalii wanatafuta ugali kwenye mitandao,Arusha sio ya kindezi hivyo labda zamani!!
Miaka mi 5 Arusha itaipiku mwanza na itakua level zingine mi niko hapa zaidi ya miaka 30 hao wadudu siwajui ni utamaduni wa Arusha tu kuvaa na kuongea kama vile msukuma na ugali wa samaki
 
Umemaliza kila kitu 👏
 
Back
Top Bottom