RPC Dodoma atumbuliwa baada ya kutoa taarifa tata ya binti kulawitiwa anaweza kuwa anajiuza

RPC Dodoma atumbuliwa baada ya kutoa taarifa tata ya binti kulawitiwa anaweza kuwa anajiuza

Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari yenye kichwa cha habari kinachosema, "RPC; ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KULAWITIWA ALIKUWA KAMA ANAJIUZA", kauli inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hayo yametokana na mazungumzo kwa njia ya simu na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi ambaye miongoni mwa maswali aliyomuuliza kamanda (mwandishi huyo), Je upelelezi wa kesi umekamilika? na swali lingine alilomuuliza inadaiwa alikuwa anajiuza? Majibu ya kamanda aliyomjibu mwandishi huyo ni kwamba hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.



Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza



Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa kauli hiyo kama inavyoonekana kwenye hicho kichwa cha habari siyo msimamo wa Jeshi la Polisi kauli sahihi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4,6 na 9,2024. Vilevile tungependa kujulisha kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo Agosti 19,2024.



Jeshi la Polisi lingependa kuomba radhi kwa kila mmoja aliyeguswa na kuchukizwa na kauli hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake. Aidha wakati uchunguzi huo wa kupata usahihi wa kauli hizo, Mkuu wa Jeshi la Polisi amefanya mabadiliko madogo kwa kumhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Theopista Mallya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP George Katabazi.



"Askari" huko àlipo anazidi kuhaha tu maana jinamizi la binti bado linawaandama na mpaka hapa naona halitawaacha salama!
 
Huyu RPC kangolewa kiboya sana
Yote kutaka kulindana

Ova
 
Kufa kufaana. 😄😄😄😄
Mdomo umemponza, uchunguzi ule ni wa kihuni sana.

Natamani kuona Serikali kupitia jeshi la Polisi libadilishe mfumo wa maombi, wazingatie ufaulu mzuri kujiunga na jeshi hilo na sio kufanya kama wafanyavyo sasa.
 
Achana na cheo alicho nacho. Being RPC anakua na mamlaka makubwaa katika mkoa husika(kuna kuona onwa ili kulainisha mambo), kuna posho zinazo ambatana na hio nafasi tofauti na ma commissioners walio head office haswa ukute hana kitengo pale HQ....Atasona sana magazeti kusubiria mshahara
 
Hawa nao ni binadamu tu tulionao mitaani
Wanaweza fanya chochote kila kama wengine
Wapo wenye nidhamu na maadili ila mmoja mmoja anakuwa katereza

Kuna kupindi ulaya kinaitwa " To catch a Copper"
Hawana utani hawa jamaa, kama una kesi lazima uwajibike tu
 
Back
Top Bottom