Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Safia Jongo akizungumza.
Mmoja wa Wakaguzi akiwa katika shughuli zake alibaini Kibanda kilichokuwa karibu na maduara hayo kimeanza kutitia, akatoa taarifa kwa wenzake haraka waliokuwa ndani ya eneo hilo na wote walifanikiwa kutoka nje wakiwa salama.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa hakuna madhara ya kibinadamu kwani hakuna mtu aliyekuwa ndani ya maduara hayo kwa wakati huo, kwa sababu hayakuwa katika shughuli za uzalishaji yalikuwa yanafanyiwa ukarabati.
Hatua za kiusalama zimechukuliwa kwa kushirikisha Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara na mamlaka nyingine za Serikali pamoja na wananchi.
Taarifa ya Jeshi la Polisi iliyosainiwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, imetoa rai kwa wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zenye kuleta taharuki zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii, kwani halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kusambaza taarifa hizo
Soma pia Tetesi: - Wachimbaji zaidi ya 200 wahofiwa kufariki huko Geita Machimbo ya Msasa baada ya maduara kuanguka