Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kuhusu Utekaji Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ASP Philemon Makungu amesema baadhi ya taarifa zinazoripotiwa kwa watu kutekwa ni uzushi kwani sio kila mtu anatekwa, baadhi yao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi halafu wanazusha kwamba wametekwa.
Philemon amesema aliyetekwa ndio anatakiwa kutoa taarifa, kwasababu polisi akimkamata mtu kikawaida, atamwambia amemkamata na kumuonyesha kitambulisho. Ameongeza kuwa, mtuhumiwa anaweza kupiga kelele na kusema anatekwa baada kuona nguvu ya kumkamata ni ndogo ili wananchi wasogee na kumdhuru polisi, ili yeye aweze kukimbia.
Pia amesema wahalifu ni wajanja, wakisikia wanatafutwa hukimbia, na ndio maana polisi huvaa kiraia!
Akitolea mfano wa matukio hayo, amesema hata kiongozi wa dini wanayesema alitekwa, yeye mwenyewe hakusema ametekwa, bali ni mtu aliyeamua kusema hayo kwa kusikia bila ya kuwa na uhakika.
Philemon ametoa wito kwa wananchi kutokimbilia mambo, wakiona tukio watoe taarifa sehemu inayohusika na haki itapatikana, na kuacha mambo ya kuzua taharuki kwenye jamii. Ameongeza pia sheria ipo kwa wanaozua taharuki kwenye jamii, na kuwataka waache kuiga mambo kwa kuamini watu ambao hawawajui, kwani mtu anaweza kuwa mwongo au mkweli.