RPC Kilimanjaro na Arusha wapuuza agizo la Mzee Kinana


Baada ya CCM kupoteza ushawishi kwa umma, wameamua kuja na mbinu ya kufanya siasa za kiki ili kuhadaa umma kuwa wanastahili kuendelea kukaa madarakani. Ndio hapo unaona viongozi wa CCM wakiingilia moja kwa moja watendaji wa serikali. Ni kama wanalazimisha kurudi mfumo wa chama kushika hatamu.

Ni hatari unapokuwa na chama kimoja kukaa madarakani muda mrefu, maana mambo mengi yataanza kutekelezwa kinyume na utaratibu ili kuhalalisha uwepo wa hicho chama madarakani.
 
Hivi kama gari imekamilika trafiki ana kosa cha kukuambia? Au nawe ni mtembea na miguu kama mimi?
Hawezi kusema chochote, atakuacha uendelee zako.

Wanaolalamika ni wale wanaoendesha mangarangara!
 
Wengi wa Madereva wanaolalamika ni wale wasiofuata Sheria na Taratibu zilizowekwa, ukiwa na gari lililokamilika na wewe mwenyewe umekamilika ikiwemo kuendesha gari kwa kufuata Sheria za uendeshaji hakuna trafiki atakayekusumbua.
Askari akiamua kutafuta kosa kwenye gari Loko hakosi, 98% hayakamilika.
 

Kuna kauli ya kinana na miongozo ya kisheria
 
Kinana siyo kiongozi wa kiserikali; hana mamlaka ya kutoa maagizo kwa RPC. Kama anachukizwa kazi na polisi, basi atoe malalamiko yake huko ndani ya CCM kwa mwenyekitri wake ambaye ndiye rais na ana mamlaka najuu ya polisi. Hii kuchukulia kuwa CCM ni juu ya serikali ni makosa na matumizi mabaya ya madaraka ambayo viongoiz wa CCM hawana.
 
ni kweli wamerudi aisee wengi hao ila sometimes wanasidia dreva kujitathmini
 
Wamekuwa kama nyuki! Yani ni kama vile ile kauli ya Kinana wameichukulia kinyume!
#BureKabisa
 
Ni nchi nzima Mkuu, majuzi tumetoka Mbeya kuja Dar, tumesumbuliwa sana njiani na hasa Mafinga hadi Iringa tumesimamishwa zaidi ya mara 6, shida ni kwamba wanatafuta rushwa for 0 offenses
Hata kama hauna kosa lazima waombe pesa. Kuna kitu hakiko sawa hii Serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…