DOKEZO RPC Mara,OCD Wilaya ya Bunda tupieni jicho askari hawa,wanaharibu taswira ya jeshi la polisi...

DOKEZO RPC Mara,OCD Wilaya ya Bunda tupieni jicho askari hawa,wanaharibu taswira ya jeshi la polisi...

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Yakki Kadaf

Member
Joined
Jan 8, 2023
Posts
29
Reaction score
107
Wasaalam wanajamvi naendelea na namna maskari Eli eli, afande zawadi na mgambo ajulikanae kwa jina Samwel wanavyoharibu sifa nzuri ya jeshi la polisi wilayani Bunda.

Huyu mgambo ambaye vijana wa mjini wanamuita "Mundu" wa afande li eli kapewa mamlaka ya kutembea na pingu ambazo amekuwa akizitumia kwa maslahi yake pamoja na wanufaikaji wengine eli eli na zawadi kama ifuatavyo:

Wilayani Bunda hasa halmashauri ya mji wa Bunda kuna kundi maarufu la vijana ambao hurusha mabunda ya pesa feki "mrimba" ambapo mtu wa kuja anapoliokota lile bunda vijana wapatao wawili au zaidi wanakuwa eneo la karibu humfuata aliyeliokota na kujifanya wote wameliona ambapo hujifanya kumshawishi kwenda pembeni ili wagawane ambapo mhusika huishia kutapeliwa.

Sasa Mgambo Samweli anahusikaje hapa? Jibu ni kwamba mgambo huyu ana orodha yote ya vijana hawa na maeneo ambayo huenda kufanya uhalifu ikiwemo kuuza dhahabu feki nk. Mgambo huyu ana ratiba za hawa vijana zote za wiki nzimana alishawapa utaratibu hawa vijana ambapo kila kijana anayefanikisha dili lake humpatia ten percente(10%)ambapo mhusika huipeleka kwa eli eli ambaye huigawanyisha.

Njia nyingine anayoitumia huyu mgambo ni pale anapomuona mtu au kusikia ana kitu cha thamani mfano Godoro, Tv, radio, woofer nk atamfuata na kumuomba amuonyeshe risti(kiuhalisia ni ngumu kutunza risti kwa kila mali unayoimiliki) inapotokea mhusika akadai hana risti huwekwa chini ya ulinzi na endapo akieleweka kutoa hongo ataachiwa huru na mali itataifishwa. Nguvu ya kuidai hatakuwa nayo maana hana risti. Akikosa risti na wakati huo huo hataki kutoa hongo atapelekwa "lock up" ambapo akiwa huko kuna uwezekano mkubwa wa kubambikiwa kesi za uvunjaji na uporaji!

Yapo mambo mengi sana ya kuudhi yanayofanywa na hawa wahusika ila naliomba jeshi la polisi kupitia RPC Mara, OCD Bunda kufuatilia hizi tuhuma maana wanatumia mamlaka yao vibaya sana! Jeshi linachafuliwa na watu wachache wasio na maadili ya kazi!
 
Huwezi kujua maana unaposema hivyo ina maana hii kazi imeendelea kwa mda mrefu
Je kama hao wakubwa ndio wako nyuma?

Haiwezekani watu wanawekwa ndani huku mabulungutu yanatupwa eti wa kuokota wanae

Wazee wapo wanayaona haya na wananchi wapo, mashushushu wapo
Serikali ya mitaa wapo
Yaani mkuu wa kituo hana habari kabisa kinachoendelea mji wake?

Mimi hii haiingii akilini kabisa mkuu
Kazi yake ni nini kama hayajui mambo haya?

Hao wakubwa watolewe hapo na hii boss alione
 
Wezi wanamajungu Sana.Wewe Ni tapeli miaka yote unatupa mabunda na pia unanunua vitu vya wizi Sasa ukiotewa ndiyo unakuja Jamii forums .Sasa Mundu akupeleke tu Gerezani maana umechoka favour
 
Waharifu walio wengi hutumia skendo ili kudhoofisha utendaji kazi wa askari mahiri, hatukatai mawazo yako lakini ningelitarajia ungelikuja na vithibitisho bayana si kuandika andika kwa kuunga nukta. Nadhani ungelikuja na taarifa hata moja ambayo inathibitisha ukwel huo, sawa yawezekana michezo kama hiyo ipo lakini tunawezaje kukuamin kama wewe ni raia mwema au ni mmoja wapo ya waharifu mliojipanga kuwachafua maaskari waadilifu na jeshi la polisi kwa ujumla
 
Back
Top Bottom