PostGE2025 RPC Mbeya: Msishawishiwe kushiriki maandamno yasiyo halali

PostGE2025 RPC Mbeya: Msishawishiwe kushiriki maandamno yasiyo halali

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamini Kuzaga, ametoa wito kwa Vijana wanaojihusisha na shughuli za bodaboda kutojihusisha au kushawishiwa kuingia kwenye maandamano yasiyo halali, akisisitiza kuwa vitendo hivyo vinaweza kuhatarisha amani, usalama na ustawi wa maeneo yao.

Amesema jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa elimu kwa vijana ili kuwakinga dhidi ya vitendo vinavyoweza kuwaweka kwenye mazingira ya uvunjifu wa sheria, huku akibainisha kuwa uelewa sahihi wa sheria za barabarani na nidhamu ni nyenzo muhimu za kujilinda na kuepuka ushawishi hatarishi.

Kamanda Kuzaga ametoa kauli hiyo jana Desemba 07, 2025 wakati akizindua mafunzo maalumu ya udereva salama kwa madereva wa bodaboda katika Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Mafunzo hayo yanatolewa na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mbeya na yamelenga kuwaongezea ujuzi, umahiri na uelewa wa kanuni za usalama barabarani.

Amesisitiza kuwa kuwajengea uwezo madereva wa bodaboda ni hatua muhimu katika kupunguza ajali, kuimarisha nidhamu barabarani na kuboresha utoaji wa huduma salama kwa jamii.

Kwa upande wao, baadhi ya madereva wa Bodaboda walioshiriki mafunzo hayo wamesema wanayapokea kama fursa ya kuboresha huduma wanazotoa, kuongeza uelewa wa sheria za barabarani na kujiepusha na mambo yanayoweza kuathiri kazi zao.

Aidha, wameeleza kuwa mafunzo hayo yataongeza usalama wao na wa Wananchi wanaowahudumia katika maeneo ya Kiwira na jirani.
1765187182772.png
 
Maandamano kuwaondoa watekaji na wauaji ccm na polisi ni halali.

Wanaosema si halali ni polisi na ccm.
 
Angesema kwanza mdude nyagali chadema mpaluka Yuko wapi ndio huo wito wake ungekuwa na maana.
 
Mkuu wa mkoa aliyekuwa mbeya somebody HOMERA wakati mdude anatekwa ndio alikuwa RC akaongea ongea ujinga kuhusu tukio lile. Leo hii RC kapewa zawadi ya uwaziri. Hivyo watu wakiandamana wana haki maana hawana mtetezi. Kwahiyo hili ni vuguvugu kati ya nyie wenye shibe vs walalahoi wanaotekwa Kila siku na huku nyie mmekaa kimya. Imagine Tulia Akson akiwa spika alizuia hata mijadala ya utekaji bungeni Leo hii mnataka kuwanyamazisha ndugu jamaa na marafiki wa mdude? Noooo kuweni wakweli nyie ndio mmepuyamga kiuongozi.
 
Back
Top Bottom