RPC Mtwara hatakiwi kuwa kazini kwa uzembe aliofanya

Mkuu huko Polisi wapo wenye degree na ni wapumbavu wakubwa tu. Transformation ni zaidi ya kuwa na graduates. Tunahitaji kuundwe chombo huru kitachoisimamia Polisi, pia wapunguziwe majukumu. Fikiria Polisi huyohuyo akamate, achunguze, atoe ushahida. Kuna kitabu nimekisahau jina, kilitoa mapendekezo mazuri mno juu ya mageuzi ya Jeshi la Polisi nchini. Bahati mbaya si taifa la watu wenye kusoma, kuanzia watawala wenyewe na watawaliwa.
 
RPC aunganishwe kwenye kesi, Waziri na IGP waachie ofisini na wasipofanya hivyo, Mama anapaswa kuwatumbua...tuache kulea uzembe.
 
Ni hatari sana kuwa na askari njaa njaa, wako majeshini kutafuta maisha na sio kulinda viapo vyao..
 
Hatuna majeshi ndugu zangu, sio polisi, uhamiaji, jw nk Ni vile tu hatujawahi pata changamoto za kiusalama kama wenzetu Kenya na Uganda.
Usiombee changamoto za kiusalama ziwe kama za wenzetu ila kumbuka kuwa serikali inatumia gharama kubwa kuilinda amani hii iliyopo na haya mambo wanayofanya baadhi ya watumishi wa idara hizo yasikupelekee ww kutoa kauli nzito na tata kuhusu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.Kila kitu kinacho fanyika hapa ni kwa sababu ya amani iliyopo,kuwa mzalendo sana kwa nchi yako,hayo mambo yanayo tokea ni changamoto tu za kiutendaji tu
 
Acha jazba, tulia kabla ya kupost.
 
ZOMBE yupo mahali anacheka tuu........inatia hasira.......na huyu chui JIKE yuko ziarani kuvishwa U-Chief.....kweli wanasema pata fedha au pandishwa cheo tujue TABIA zako........hawa polisi hawa inabidi tuanze kuwafyatua kimya kimya....
 
Yule RPC kimaadili hatakiwi kuendelea kuwa RPC hata kwa dakika tano maana nae ni mtuhumiwa na uchunguzi ufanyike haraka apate stahiki yake.
 
Nasikia na yule njagu aliemtisha nape na pisto naye ndani ya mkumbo[emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…