RPC Pwani akanusha mkuu wa kituo cha polisi Kongowe kuhusika kupotea kijana Hussein

RPC Pwani akanusha mkuu wa kituo cha polisi Kongowe kuhusika kupotea kijana Hussein

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani, kupitia kwa Kamanda wake ACP Salim Morcase limekanusha vikali taarifa zinazodai kuwa Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kongowe alishirikiana na askari Mgambo kumkamata kijana Hussein Abdallah Mkwame (26), ambaye kwa takribani miezi miwili (2) sasa hajulikani halipo tangu alipokamatwa na watu wasiojulikana Mei 19 mwaka huu eneo la Ungindoni -Kongowe, wilaya ya Kibaha

ACP Morcase ameieleza Jambo TV kuwa, mnamo Mei 21 mwaka huu Jeshi la Polisi mkoani humo lilipokea taarifa kutoka kwa Baba mzazi wa Hussein aitwaye Abdallah Omary Mkwame kuhusiana na kupotea kwa mtoto wake, ambapo haraka iwezekanavyo jalada la uchunguzi lenye namba KBA/CID/PE/31/2025 lilifunguliwa na kuanza ufuatiliaji ambapo hadi sasa watu kadhaa akiwemo Asia Mbonde ambaye ni Shemeji wa Hussein na Fatma Omary wamehojiwa

Soma Pia: Sitofahamu yaibuka! kijana adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana tangu Mei 19 mwaka huu Kibaha


Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani, limelazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia Jambo TV kupokea malalamiko kutoka kwa Baba mzazi wa Hussein aliyedai kuwa mashuhuda wa tukio hilo walimwambia kuwa kijana wake amekamatwa na askari Mgambo na maafisa wa Polisi kutoka Kituo kidogo cha Polisi Kongowe walioambatana na Mkuu wa Kituo hicho, lakini katika ufuatiliaji wake Polisi walikanusha kuhusika, na kwamba licha ya kufuatilia kwenye vituo mbalimbali vya Polisi na Hospitali (Wodini na Mochwari) za Kibaha lakini hadi sasa hawajamuona,

 
Back
Top Bottom