Hali ya gumzo imetanda kwa baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Songea mjini Mkoani Ruvuma baada ya Mwanamke mmoja katika Ofisi za Shirika la Umeme TANESCO Mkoani humo akiwa hana nguo huku baadhi ya Mashuhuda wakisema alianguka na ungo wa kichawi wakati akipita juu ya Ofisi hizo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma Marco G Chilya ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kupigiwa simu na Meneja wa TANESCO baada ya Mwanamke huyo kukutwa kwenye Ofisi hizo ambapo hata hivyo RPC Chilya amekanusha taarifa za ungo na kusema Mwanamke huyo sio Mchawi bali ana tatizo la akili.