RPC Singida Badilika, wape ushirikiano Waandishi wa Habari

RPC Singida Badilika, wape ushirikiano Waandishi wa Habari

Mliogwa

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
41
Reaction score
47
Huwa ninashangaa ninapoona baadhi ya MaRPC nchini wanavyoshirikiana na wanahabari linapotokea jambo linalohitaji taarifa ya Jeshi la Polisi.....hali hii tofauti sana hapa Singida.

RPC SACP Amon Kakwale hapendi na hataki kbs ushirikiano na waandishi. Mara kadhaa amekuwa akikwamisha shughuli za kihabari kwa kukataa kutoa ushirikiano. Mara kadhaa amekuwa mzito kutoa habari na anawaambia waandishi wasitoe hadi atakaposema akisema hivyo ndo imeenda. Kulikuwa na tukio la maafisa wa TFS kuuwawa kwa mishale huko Mgori RPC hakuita press ukiuliza wanakwambia wanashughulikia had jambo linaishia hewani.

Hii tena nimeiona kewnye ajali ya waliofariki kwa maji huko Mang'onyi juzi Machi26, 2026 had inafika jion RPC anapgiwa anasema atatujulisha na story inatakiwa kwenda hewani. Tunaomba kamanda badilika tunafanya kazi na ww kwny mazingira magumu sn ya kihabari kulinganisha na Makamanda waliopita.
 
We ni mwandishi wa chombo gani, cha umma au binafsi, cha mtandaoni au cha kawaida? Vyombo vya mtandaoni huripoti tukio on the spot bila kusubiri taarifa za kipolisi. Hiyo habari ya Mang'onyi tuliishaipata haraka kabla ya kuthibitishwa na polisi. Siku hizi ni ngumu kudhibiti habari zisienee kwa haraka, kuna mitandao inafanya kazi masaa yote!
 
Hii tena nimeiona kewnye ajali ya waliofariki kwa maji huko Mang'onyi juzi Machi26, 2026 had inafika jion RPC anapgiwa anasema atatujulisha na story inatakiwa kwenda hewani. Tunaomba kamanda badilika tunafanya kazi na ww kwny mazingira magumu sn ya kihabari kulinganisha na Makamanda waliopita.
Hivi mnashindwa kumchapa makofi au kwasababu anaitwa RPC ndio mnamuogopa?
 
Kwanza hata mimi waandishi wa habari siwaamini kabisa..
Niliwahi kuwapa taarifa mwaka 2004 dec mahali fulani na walinihoji, walichokirusha hewani ni kitu kingne tofauti..
Walikuwa wakiongozwa na mabele makubi..
Popote nilipo sitaki mawasiliano na waandishi wa habari..
Shindwa kabisa
Waliripoti uongo?
 
waandishi wasitoe hadi atakaposema
Kwenye uandishi wa habari Kuna source nyingi za habari nenda eneo la tukio hoji mashuhuda, viongozi wa mtaa/kijiji kisha mtafute RPC atakachosema ripoti hicho hicho tena mpigie simu umrekodi kabisa, kisha mtafute mwenyekiti wa kamati ya usalama wilaya au mkoa ano wasipotoa ushirikiano andika hivyo hivyo kwamba wamekataa kutoa ushirikiano cha msingi tu uwe na ushahidi kwamba walikataa hivyo kama ni simu rekodi kama umeenda ofisini kwake washa mic yako ili asije kukukana.

Hiyo ndio Dawa yao
 
Kwanza hata mimi waandishi wa habari siwaamini kabisa..
Niliwahi kuwapa taarifa mwaka 2004 dec mahali fulani na walinihoji, walichokirusha hewani ni kitu kingne tofauti..
Walikuwa wakiongozwa na mabele makubi..
Popote nilipo sitaki mawasiliano na waandishi wa habari..
Shindwa kabisa
Naungana na wewe ,hawa watu sio kabisa ,kuna sehemu fumanizi ilifanyika ila mfumaniwaji alichoropoka salama salmini ila walipokuja kutoa taarifa nilishangaa sana ni uongo mtupu kuhusu yule mwamba mara kapigwa ,mara kanyanganywa silaha nikajua hii midude inacheza na biti za raia
 
Hilo tifu lake sio dogo huko ndio wanaita kuchongeana
Mbona ITV waliripoti hivyo hivyo na sauti ya RPC alisema yupo kikaoni badae simu yake ikaita bila kupokelewa.

Miaka hiyo ya nyuma RPC boazi wa Kilimanjaro alikuwa hatoi ushirikiano kama ajali imetokea waandishi wanampigia wanamwambia kamand kuna taarifa ya watu 10 wamefariki kwenye ajali je ukweli wa taarifa ukoje??? Akisikia tu anajibu hapana sio watu kumi ni watu wawili tu akishajibu hivyo unapata wasaa wa kumdodosa hayo maswali mengine.

au kama jambazi amevamia duka moja unamuuliza kuna taarifa kuwa mj wa moshi Maduka zaidi ya Kumi yamevamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto anakanusha fasta anakupa taarifa sahihi Story inapanda hewani ikiwa ya moto.
 
Hio ndio inavyokua ila ulivyoeleza pale juu na ulivyoeleza hapa ni tofauti
tofauti yake ni nini Mkuu?? mimi si nimesema akigoma kutoa ushirikiano Ripoti alichokuambia??? kama yupo bize RC AU DC pia anweza kuthibitisha mfano ajali, majanga kama amfuriko nk. Nyingine daktari au watu wa zimamaoto. Maana kumtegemea RPC tu anaweza asikupe ushirikiano au akakupa kwa kuchelewa
 
Hapana unakumbuka walichofanya BBC kwa Muliro kipindi kile cha mauaji sasa wewe ndio unasema wafanye hivyo yaan wachukue maelezo yake kisha wayasambaze anavyosema sis ndio?
 
Back
Top Bottom